Ayubu 42 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Ayubu 42:1-17

Sehemu Ya Tano

(Ayubu 42)

Ayubu Anamjibu Bwana

1Ndipo Ayubu akamjibu Bwana:

242:2 Mwa 18:14; Yer 32:17; Mt 19:26; 2Nya 20:6; Efe 1:11“Ninajua ya kuwa unaweza kufanya mambo yote,

wala hakuna mpango wako unaoweza kuzuilika.

342:3 Ay 34:35; 38:2; Za 40:5Uliuliza, ‘Ni nani huyu afichaye mashauri yangu bila maarifa?’

Hakika nilisema juu ya mambo niliyokuwa siyaelewi,

mambo ya ajabu mno kwangu mimi kuyajua.

442:4 Ay 38:3; 40:7“Ulisema, ‘Sikiliza sasa, nami nitanena;

nitakuuliza swali, nawe yakupasa kunijibu.’

542:5 Ay 26:14; Rum 10:17; Amu 13:22; Mt 5:8Masikio yangu yalikuwa yamesikia habari zako,

lakini sasa macho yangu yamekuona.

642:6 Eze 6:9; Rum 12:3; Kut 10:3; Ezr 9:6Kwa hiyo najidharau mwenyewe,

na kutubu katika mavumbi na majivu.”

Mwisho: Marafiki Wa Ayubu Wanafedheheshwa

742:7 Yos 1:7; Ay 32:3, 8; 9:15Baada ya Bwana kusema mambo haya yote na Ayubu, akamwambia Elifazi Mtemani, “Nina hasira juu yako na juu ya rafiki zako wawili, kwa sababu hamkusema yaliyo sawa kwa habari yangu, kama alivyosema mtumishi wangu Ayubu. 842:8 Hes 23:29; Eze 45:23; Mwa 20:17; Yak 5:15-17; Ay 22:30Basi sasa chukueni mafahali saba na kondoo dume saba mkamwendee mtumishi wangu Ayubu nanyi mkatoe sadaka za kuteketezwa kwa ajili yenu wenyewe. Mtumishi wangu Ayubu ataomba kwa ajili yenu, nami nitayakubali maombi yake ili nisiwatendee sawasawa na upumbavu wenu. Ninyi hamkusema yaliyo sawa kwa habari yangu, kama alivyosema mtumishi wangu Ayubu.” 942:9 Ay 2:11; Mwa 19:21; 20:17; Eze 14:14Kwa hiyo Elifazi Mtemani, Bildadi Mshuhi, na Sofari Mnaamathi wakafanya kama Bwana alivyowaambia; naye Bwana akayakubali maombi ya Ayubu.

1042:10 Kum 30:3; Za 14:7; 126:5-6; Yak 5:11Baada ya Ayubu kuwaombea rafiki zake, Bwana akamwondoa kwenye uteka, akamfanikisha tena naye akampa mara mbili ya vile alivyokuwa navyo hapo mwanzoni. 1142:11 Ay 19:13Ndipo ndugu zake wote waume kwa wake na kila mtu aliyemfahamu mwanzoni, wakaja wakala pamoja naye katika nyumba yake. Wakamfariji na kumtuliza moyo juu ya taabu yote Bwana aliyoileta juu yake, nao kila mmoja akampa kipande cha fedha na pete ya dhahabu.

1242:12 Yak 5:11Bwana akaibariki sehemu ya mwisho ya maisha ya Ayubu kuliko ile ya kwanza. Alikuwa na kondoo elfu kumi na nne, ngamia elfu sita, jozi za mafahali elfu moja, na punda wa kike elfu moja. 13Tena alikuwa na wana saba na binti watatu. 14Binti wa kwanza aliitwa Yemima, wa pili Kesia na wa tatu Keren-Hapuki. 15Hapakuwepo mahali popote katika nchi ile yote palipopatikana wanawake wazuri kama binti za Ayubu; naye baba yao akawapa urithi pamoja na ndugu zao.

16Baada ya hili Ayubu akaishi miaka 140; akawaona wanawe na wana wa wanawe hata kizazi cha nne. 1742:17 Mwa 15:15; 25:8Hivyo Ayubu akafa, akiwa mzee aliyekuwa ameshiba siku.