Ayubu 41 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

Ayubu 41:1-34

141:1 Za 104:26; Isa 27:1“Je, waweza kumvua Lewiathani41:1 Lewiathani ni mnyama mkubwa wa baharini mwenye magamba anayefanana na joka kubwa, mwenye umbo la kutisha, asiyeweza kuvuliwa. kwa ndoano ya samaki,

au kufunga ulimi wake kwa kamba?

241:2 Isa 37:29; Eze 19:4; Isa 30:28Waweza kupitisha kamba puani mwake,

au kutoboa taya lake kwa kulabu?

341:3 1Fal 20:31Je, ataendelea kukuomba umhurumie?

Atasema nawe maneno ya upole?

441:4 Kut 21:6Je, atafanya agano nawe ili umtwae

awe mtumishi wako maisha yake yote?

5Je, utamfuga na kumfanya rafiki kama ndege,

au kumfunga kamba kwa ajili ya wasichana wako?

6Je, wafanyabiashara watabadilishana bidhaa kwa ajili yake?

Watamgawanya miongoni mwa wafanyao biashara?

741:7 Ay 40:24Je, waweza kuijaza ngozi yake kwa vyuma vyenye ncha kali,

au kichwa chake kwa mkuki wa kuvulia samaki?

841:8 Ay 3:8Kama ukiweka mkono wako juu yake,

utavikumbuka hivyo vita na kamwe hutarudia tena!

941:9 Ay 40:16Tumaini lolote la kumtiisha ni kujidanganya;

kule kumwona tu kunamwangusha mtu chini.

1041:10 Ay 3:8; 2Nya 20:6; Ufu 6:17; 1Kor 10:22Hakuna yeyote aliye mkali athubutuye kumchokoza.

Ni nani basi awezaye kusimama dhidi yangu?

1141:11 Ay 34:33; Yos 3:11; Rum 11:35; Mdo 4:24; Mwa 14:19; Kum 10:14Ni nani mwenye madai dhidi yangu ili nipate kumlipa?

Kila kitu kilicho chini ya mbingu ni mali yangu.

1241:12 Ay 40:18; 39:11“Sitashindwa kunena juu ya maungo yake,

nguvu zake na umbo lake zuri.

1341:13 Ay 30:11; 39:10Ni nani awezaye kumvua gamba lake la nje?

Ni nani awezaye kumsogelea na lijamu?

1441:14 Za 22:13Nani athubutuye kuufungua mlango wa kinywa chake,

kilichozungukwa na meno yake ya kutisha pande zote?

1541:15 Ay 40:17Mgongo wake una safu za ngao

zilizoshikamanishwa imara pamoja;

16kila moja iko karibu sana na mwenzake,

wala hakuna hewa iwezayo kupita kati yake.

17Zimeunganishwa imara kila moja na nyingine;

zimengʼangʼaniana pamoja wala haziwezi kutenganishwa.

1841:18 Ay 40:17Akipiga chafya mwanga humetameta;

macho yake ni kama mionzi ya mapambazuko.

1941:19 Dan 10:6Mienge iwakayo humiminika kutoka kinywani mwake;

cheche za moto huruka nje.

2041:20 Za 18:8Moshi hufuka kutoka puani mwake,

kama kutoka kwenye chungu kinachotokota kwa moto wa matete.

2141:21 Ay 4:9; Isa 11:4; 10:17; Yer 4:4Pumzi yake huwasha makaa ya mawe,

nayo miali ya moto huruka kutoka kinywani mwake.

2241:22 Ay 39:11Nguvu hukaa katika shingo yake;

utisho hutangulia mbele yake.

23Mikunjo ya nyama yake imeshikamana imara pamoja;

iko imara na haiwezi kuondolewa.

2441:24 Mt 18:6Kifua chake ni kigumu kama mwamba,

kigumu kama jiwe la chini la kusagia.

2541:25 Ay 39:20; 3:8Ainukapo, mashujaa wanaogopa;

hurudi nyuma mbele yake anapokwenda kwa kishindo.

2641:26 Ay 8:18; 40:24Upanga unaomfikia haumdhuru,

wala mkuki au mshale wala fumo.

2741:27 Ay 41:29Chuma hukiona kama unyasi,

na shaba kama mti uliooza.

2841:28 Za 91:5Mishale haimfanyi yeye akimbie;

mawe ya kombeo kwake ni kama makapi.

2941:29 Ay 41:27; 5:22Rungu kwake huwa kama kipande cha jani kavu;

hucheka sauti za kugongana kwa mkuki.

3041:30 Isa 28:27; Amo 1:3; Isa 41:15Sehemu zake za chini kwenye tumbo

zina menomeno na mapengo kama vigae vya chungu,

zikiacha mburuzo kwenye matope

kama chombo chenye meno cha kupuria.

3141:31 1Sam 2:14; Eze 32:2Huvisukasuka vilindi kama sufuria kubwa ichemkayo,

na kukoroga bahari kama chungu cha marhamu.

32Anapopita nyuma yake huacha mkondo unaometameta;

mtu angedhani vilindi vilikuwa na mvi.

3341:33 Ay 40:19Hakuna chochote duniani kinacholingana naye:

yeye ni kiumbe kisicho na woga.

3441:34 Ay 28:8Yeye huwatazama chini wale wote wenye kujivuna;

yeye ni mfalme juu ya wote wenye kiburi.”

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

约伯记 41:1-34

1“你岂能用鱼钩钓海怪,

用绳索绑住它的舌头?

2你岂能用绳子穿它的鼻子,

用钩子穿它的腮骨?

3它岂会向你连连求饶,

对你说柔和的话?

4它岂肯与你立约,

一生做你的奴隶?

5你岂能拿它当小鸟玩耍,

或拴起来给幼女取乐?

6渔夫们岂能把它当货物出售,

卖给商人?

7你岂能在它皮上戳满长矛,

头上插满鱼叉?

8你动手碰碰它,

就知道是场恶战,绝不会再碰。

9企图捕捉它的都会失望,

人看到它就会心惊胆战。

10再凶猛的人也不敢惹它。

这样,谁能在我面前站立得住?

11谁给过我什么,要我偿还呢?

天下万物都是我的。

12“关于它的四肢、大力和健美的身体,

我不能缄默不言。

13谁能剥去它的外皮?

谁能给它戴上辔头?

14谁能打开它的嘴巴?

它的牙齿令人恐惧。

15它的脊背覆着行行鳞甲,

牢牢地密封在一起,

16紧密无间,

连气也透不进去。

17鳞甲彼此相连相扣,

无法分开。

18它打喷嚏时,水光四射;

它的眼睛亮如晨光;

19口中喷出火炬,

迸出火星;

20鼻孔冒烟,

如沸腾的锅和燃烧的芦苇;

21呼气可点燃煤炭,

口中喷出火焰;

22颈项强而有力,

恐惧在它前面开路;

23身上的皱褶紧密相连,

牢牢地密封在一起;

24心坚如石,

硬如磨石。

25它一站起来,勇士都害怕,

见它冲来,他们慌忙退缩。

26刀剑挡不住它,

长矛、标枪、尖戟也无能为力。

27它视铁如干草,

视铜如朽木。

28利箭吓不跑它,

弹石在它看来只是碎秸;

29棍棒无异于秸秆,

它嗤笑投来的标枪。

30它腹部有锋利的瓦片,

在淤泥上留下道道耙痕。

31它使深渊如锅翻腾,

使大海如油锅滚动。

32它游过后留下一道波光,

使深渊仿佛披上银发。

33地上没有动物能与它相比,

像它那样无所畏惧。

34它藐视群雄,

在高傲的百兽中称王。”