140:1 Ay 5:8; 13:3; 13:3; 9:15; 9:3; 11:8; 33:13Bwana akamwambia Ayubu:
240:2 Rum 9:20“Je, mwenye kushindana na Mwenyezi aweza kumsahihisha?
Mwenye kumlaumu Mungu na ajibu.”
3Ndipo Ayubu akamjibu Bwana:
440:4 Ay 42:6; Amu 18:19; Ay 29:9; Ezr 9:6; Zek 2:13“Mimi sistahili kabisa: ninawezaje kukujibu wewe?
Nauweka mkono wangu juu ya kinywa changu.
540:5 Ay 9:3; 9:15Nimesema mara moja, lakini sina jibu;
naam, nimesema mara mbili,
lakini sitasema tena.”
640:6 Kut 14:21; Ay 38:1Ndipo Bwana akasema na Ayubu kutoka upepo wa kisulisuli:
740:7 Ay 38:3“Jikaze kama mwanaume;
nitakuuliza maswali, nawe yakupasa unijibu.
840:8 Ay 15:25; Rum 3:3; Za 51:4“Je, utabatilisha hukumu yangu?
Utanilaumu mimi ili kujihesabia haki mwenyewe?
940:9 2Nya 32:8; Za 98:1; Kut 20:19; Za 29:3-4Je, una mkono kama wa Mungu,
nawe waweza kutoa sauti ya ngurumo kama yake?
1040:10 Za 29:1-2; 45:3; 93:1; 96:6; 104:1; 145:5Basi jivike mwenyewe utukufu na fahari,
nawe uvae heshima na enzi.
1140:11 Nah 1:6; Sef 1:18; Za 18:27; Isa 32:19Fungulia ukali wa ghadhabu yako,
mtafute kila mwenye kiburi umshushe,
1240:12 Za 52:5; 1Pet 5:5; Dan 5:20; Mal 4:3; Lk 18:14mwangalie kila mtu mwenye kiburi na umnyenyekeze,
waponde waovu mahali wasimamapo.
1340:13 Hes 16:31-34; Ay 4:9Wazike wote mavumbini pamoja;
wafunge nyuso zao kaburini.
1440:14 Kut 15:6; Isa 63:5Ndipo mimi mwenyewe nitakukubalia
kuwa mkono wako mwenyewe wa kuume unaweza kukuokoa.
1540:15 Ay 9:9; Isa 11:7; 65:25“Mwangalie mnyama aitwaye Behemothi,40:15 Huyu alikuwa mnyama wa nyakati za zamani ambaye hajulikani hasa ni gani.
niliyemuumba kama nilivyokuumba wewe,
anayekula majani kama ngʼombe.
1640:16 Ay 39:11; 41:9Tazama basi nguvu alizo nazo kwenye viuno vyake,
uwezo alio nao kwenye misuli ya tumbo lake!
1740:17 Ay 41:15Mkia wake hutikisika kama mwerezi;
mishipa ya mapaja yake imesukwa pamoja.
1840:18 Ay 41:12; Isa 11:4; 49:2Mifupa yake ni bomba za shaba,
maungo yake ni kama fito za chuma.
1940:19 Za 40:5; Isa 27:1Yeye ni wa kwanza miongoni mwa kazi za Mungu,
lakini Muumba wake anaweza kumsogelea kwa upanga wake.
2040:20 Za 104:14, 26Vilima humletea yeye mazao yake,
nao wanyama wote wa porini hucheza karibu naye.
2140:21 Mwa 41:2; Za 68:30; Isa 35:7; Ay 8:11Hulala chini ya mimea ya yungiyungi,
katika maficho ya matete kwenye matope.
2240:22 Za 1:3; Isa 44:4Hiyo mimea ya yungiyungi humficha kwenye vivuli vyake;
miti mirefu karibu na kijito humzunguka.
23Wakati mto ufurikapo, yeye hapati mshtuko wa hofu;
yeye yu salama, hata kama Yordani ingefurika hadi kwenye kinywa chake.
2440:24 2Fal 19:28; Isa 37:29Je, mtu yeyote anaweza kumkamata yeye akiwa macho,
au kumnasa kwa mtego na kutoboa pua yake?