Ayubu 39 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Ayubu 39:1-30

139:1 Kum 14:5“Je, wajua ni wakati gani mbuzi wa mlimani wanapozaa?

Je, watambua ni wakati gani kulungu jike azaapo mtoto wake?

239:2 Mwa 31:7-9Je, waweza kuhesabu miezi hadi wazaapo?

Je, unajua majira yao ya kuzaa?

3Wao hujiinamisha na kuzaa watoto wao;

utungu wa kuzaa unakoma.

4Watoto wao hustawi na kuongezeka nguvu nyikani;

huenda zao wala hawarudi tena.

539:5 Mwa 16:12; Ay 6:5“Ni nani aliyemwachia punda-mwitu awe huru?

Ni nani aliyezifungua kamba zake?

639:6 Za 107:34; Yer 2:24; 14:6; Hos 8:9Nimempa nchi isiyokaliwa na watu kuwa masikani yake,

nchi ya chumvi kuwa makao yake.

739:7 Ay 5:22; 3:18Huzicheka ghasia za mji,

wala hasikii kelele za mwendesha gari.

839:8 Isa 32:20Huzunguka vilimani kwa ajili ya malisho

na kutafuta kila kitu kibichi.

939:9 Hes 23:22; Kum 33:17“Je, nyati atakubali kukutumikia?

Atakaa karibu na hori lako usiku?

1039:10 Ay 41:13; Za 32:9Je, waweza kumfungia kwenye matuta kwa kamba?

Je, atalima mabonde nyuma yako?

1139:11 Ay 40:16; 41:12, 22; Za 147:10Je, utamtumainia kwa ajili ya nguvu zake nyingi?

Utamwachia yeye kazi zako nzito?

12Utaweza kumwamini akuletee nafaka yako nyumbani

kutoka shambani na kuikusanya kwenye sakafu yako ya kupuria?

1339:13 Zek 5:9“Mbuni hupigapiga mabawa yake kwa furaha,

lakini hayawezi kulinganishwa

na mabawa na manyoya ya korongo.

14Huyataga mayai yake juu ya ardhi,

na kuyaacha yapate joto mchangani,

1539:15 2Fal 14:9bila kujali kuwa mguu waweza kuyaponda,

kwamba baadhi ya wanyama wa porini wanaweza kuyakanyaga.

1639:16 Ay 39:17; Mao 4:3Yeye huyafanyia makinda yake ukatili kama vile si yake;

hajali kwamba taabu yake inaweza ikawa bure,

1739:17 Ay 21:22; 39:16kwa kuwa Mungu hakumjalia hekima,

wala hakumpa fungu la akili njema.

1839:18 Ay 5:22Lakini akunjuapo mabawa yake kukimbia,

humcheka farasi pamoja na yeye aliyempanda.

1939:19 Ay 39:11“Je, wewe humpa farasi nguvu

au kuivika shingo yake manyoya marefu?

2039:20 Yoe 2:4-5; Ufu 9:7; Yer 8:16Je, wewe humfanya farasi aruke kama nzige,

akistaajabisha kwa tishio la mlio wake wa majivuno?

2139:21 Yer 8:6Huparapara bila woga, akizifurahia nguvu zake,

husonga mbele kukabiliana na silaha.

2239:22 Ay 5:22Huicheka hofu, haogopi chochote,

wala haukimbii upanga.

2339:23 Isa 5:28; Yer 5:16; Nah 3:3Podo hutoa sauti kando yake,

pamoja na mkuki unaongʼaa na fumo.

2439:24 Hes 10:9; Eze 7:14Bila woga na kwa ghadhabu huimeza nchi,

wala tarumbeta iliapo yeye hawezi kusimama.

2539:25 Yos 6:5; Yer 8:6; Amo 2:2Asikiapo sauti ya baragumu yeye hulia, ‘Aha!’

Hunusa harufu ya vita toka mbali,

sauti ya mtoa amri na ukelele wa vita.

26“Je, mwewe huruka kwa hekima yako

na kuyakunjua mabawa yake kuelekea kusini?

27Je, tai hupaa juu kwa amri yako

na kujenga kiota chake mahali pa juu?

28Huishi juu ya miamba mirefu na kukaa huko usiku;

majabali yenye ncha kali ndiyo ngome yake.

29Kutoka huko hutafuta chakula chake;

macho yake hukiona kutoka mbali.

3039:30 Mt 24:28; Lk 17:37Makinda yake hujilisha damu,

na pale palipo na machinjo, ndipo yeye alipo.”