Ayubu 35 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Ayubu 35:1-16

Elihu Analaumu Mtu Kujiona Kuwa Mwenye Haki

1Ndipo Elihu akasema:

235:2 Ay 33:32; 2:9; 32:2“Je, unadhani hili ni haki?

Wewe unasema, ‘Nina haki mbele za Mungu.’

335:3 Ay 21:15; 34:9Bado unamuuliza, ‘Ni faida gani nimepata,

na imenifaidi nini kwa kutokutenda dhambi?’

4“Ningependa nikujibu wewe

pamoja na marafiki zako walio pamoja nawe.

535:5 Kum 10:14; Mwa 15:5; Ay 22:12; Za 19:1-4Tazama juu mbinguni ukaone;

yaangalie mawingu yaliyo juu sana juu yako.

635:6 Ay 7:20; Mit 8:36Je, ukitenda dhambi, inamdhuruje Mungu?

Kama dhambi zako zikiwa nyingi,

hilo linamfanyia nini Mungu?

735:7 Rum 11:35; Mit 9:12; 1Kor 4:7; Lk 17:10Kama wewe ni mwadilifu, unampa nini,

au yeye anapokea nini mkononi kwako?

835:8 Eze 18:24; 18:5-9; Zek 7:9-10Uovu wako unamdhuru tu mtu mwingine kama wewe,

nayo haki yako inawafaa wanadamu tu.

935:9 Kut 2:23; Ay 5:15; 12:19; Lk 18:3-7“Wanadamu hulia kwa kulemewa na mateso;

huomba msaada kutoka mkono wenye nguvu.

1035:10 Ay 4:17; Isa 51:13; Za 77:6; Mdo 16:25; 1Pet 4:19Lakini hakuna asemaye, ‘Yuko wapi Mungu Muumba wangu,

yeye anifanyaye niimbe usiku,

1135:11 Za 94:12; Lk 12:24; Ay 32:8yeye atufundishaye sisi zaidi kuliko wanyama wa dunia,

na kutufanya wenye hekima kuliko ndege wa angani?’

1235:12 1Sam 8:18; Mit 1:1Yeye hajibu wakati watu waliapo

kwa sababu ya kiburi cha watu waovu.

1335:13 Kum 1:45; 1Sam 8:18; Ay 15:31; Mit 15:8Naam, Mungu hasikilizi maombi yao ya ubatili;

Mwenyezi hayazingatii.

1435:14 Ay 9:11; Yer 11:11Si zaidi sana kwamba hatakusikiliza

wewe usemapo humwoni,

tena ya kwamba shauri lako liko mbele zake

na wewe lazima umngojee,

15pia zaidi, kwamba hasira yake kamwe haiadhibu

wala haangalii uovu hata kidogo?

1635:16 Ay 34:35-37; 1Kor 4:20Hivyo Ayubu hufumbua kinywa chake kwa maneno yasiyo na maana;

anaongea maneno mengi bila maarifa.”