Ayubu 34 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Ayubu 34:1-37

Elihu Anatangaza Haki Ya Mungu

1Kisha Elihu akasema:

234:2 Ay 32:10“Sikieni maneno yangu, enyi watu wenye hekima;

nisikilizeni mimi, ninyi watu wenye maarifa.

334:3 Ay 12:11Kwa kuwa sikio huyajaribu maneno

kama vile ulimi uonjavyo chakula.

434:4 1The 5:21Tujichagulie wenyewe yaliyo sawa,

nasi tujifunze pamoja yaliyo mema.

534:5 Ay 33:9; 6:29; 27:2; 9; 17“Ayubu anasema, ‘Mimi sina hatia,

lakini Mungu ameninyima haki yangu.

634:6 Yer 10:19; Ay 10:3Ingawa niko sawa,

ninaonekana mwongo;

nami ingawa sina kosa,

kidonda changu hakiponi.’

734:7 Ay 9:21; 15:16Ni mtu gani aliye kama Ayubu,

anywaye dharau kama maji?

834:8 Ay 22:15; Za 50:18Ashirikianaye na watenda mabaya

na kuchangamana na watu waovu.

934:9 Ay 9:29-31Kwa kuwa anasema, ‘Haimfaidi mwanadamu kitu chochote

anapojitahidi kumpendeza Mungu.’

1034:10 Mwa 18:25; Za 92:15; Rum 3:5“Hivyo nisikilizeni mimi, ninyi watu wenye ufahamu.

Kamwe Mungu hatendi uovu,

Mwenyezi hafanyi kosa.

1134:11 Ay 21:31; 2Kor 5:10; Yer 17:10; Eze 33; 20; Mit 24:12Humlipa mwanadamu kwa ajili ya lile alilotenda;

huleta juu yake kile ambacho matendo yake yanastahili.

1234:12 Za 9:16; Kol 3:25Ni jambo lisiloweza kufikiriwa kwamba Mungu angefanya makosa,

kwamba Mwenyezi angepotosha hukumu.

1334:13 Ay 36:23; Isa 40:14Je, ni nani aliyemtawaza juu ya dunia?

Ni nani aliyemweka kuwa mwangalizi wa ulimwengu wote?

1434:14 Hes 16:22; Za 104:29; Mhu 12:7Kama lilikuwa kusudi la Mungu,

naye akaiondoa Roho yake na pumzi yake,

1534:15 Za 90:10; Mwa 2:7wanadamu wote wangeliangamia kwa pamoja,

na mtu angerudi mavumbini.

1634:16 Ay 32:10; 34:30“Kama ninyi mnaufahamu, sikieni hili;

sikilizeni hili nisemalo.

1734:17 Mwa 18:23; 2Sam 23:3-4; Mit 20:8; Rum 3:5-7; Ay 10:7Je, yeye aichukiaye haki aweza kutawala?

Je, utamhukumu mwenye haki, Aliye na Nguvu Zote?

1834:18 Kut 22:28; Isa 40:24Je, si ni yeye awaambiaye wafalme, ‘Ninyi hamfai kitu,’

nao watu mashuhuri, ‘Ninyi ni waovu,’

1934:19 Kum 10:17; Mdo 10:34; Law 19:15; Yak 2:5yeye asiyependelea wakuu,

wala haonyeshi upendeleo kwa matajiri kuliko maskini,

kwa kuwa wote ni kazi ya mikono yake?

2034:20 Kut 11:4; 12:29; Ay 12:19Wanakufa ghafula, usiku wa manane;

watu wanatikiswa nao hupita;

wenye nguvu huondolewa

bila mkono wa mwanadamu.

2134:21 Mit 15:3; Ebr 4:13“Macho yake yanazitazama njia za wanadamu;

anaona kila hatua yao.

2234:22 Za 74:20; Ay 3:5; Amo 9:2-3Hakuna mahali penye giza nene, wala uvuli mkubwa,

ambapo watenda mabaya wanaweza kujificha.

2334:23 Ay 11:11; Ezr 9:13Mungu hana haja ya kumchunguza mtu sana,

ili apate kuja mbele zake kwa hukumu.

2434:24 Ay 12:19; Dan 2:21Bila kuuliza huwapondaponda wenye nguvu nyingi

na kuwaweka wengine mahali pao.

2534:25 Ay 11:11; Mit 5:21-23Kwa sababu huyaangalia matendo yao yote,

huwaondoa usiku, nao wakaangamia.

2634:26 Mwa 6:5; Ay 8:22; 28:24; Za 9:5; Yer 44:5Anawaadhibu kwa ajili ya uovu wao

mahali ambapo kila mmoja ataweza kuwaona,

2734:27 Za 14:3; Isa 5:12; 1Sam 15:11kwa sababu wameacha kumfuata Mungu,

nao hawakuiheshimu njia yake hata moja.

2834:28 Kut 22:23; Yak 5:4; Mhu 5:8Wamesababisha kilio cha maskini kifike mbele zake,

hivyo akasikia kilio cha wahitaji.

2934:29 Za 28:1; 83:1; 109:1; Rum 8:34; Za 13:1; 97:9; 83:18Lakini kama akinyamaza kimya,

ni nani awezaye kumhukumu?

Kama akiuficha uso wake,

ni nani awezaye kumwona?

Ikiwa ni taifa au mtu mmoja, kwake ni sawa,

3034:30 Za 25:15; Mit 29:2-12; 1Fal 12:28-30ili kumzuia mtu mwovu kutawala,

au wale ambao huwategea watu mitego.

31“Kama mwanadamu akimwambia Mungu,

‘Nimekosa lakini sitatenda dhambi tena.

3234:32 Kut 33:13; Za 27:11; Lk 19:8; Ay 33:27Nifundishe nisichoweza kuona;

kama nimekukosea, sitafanya hivyo tena.’

3334:33 Mit 17:23; Yn 3:8Je basi, Mungu atakulipa kwa masharti yako,

wakati wewe umekataa kutubu?

Yakupasa wewe uamue, wala si mimi;

sasa niambie lile ulijualo.

34“Wanadamu wenye ufahamu husema,

wenye hekima wanaonisikia huniambia,

3534:35 Ay 35:16; 38:2; 42:3; 26:3‘Ayubu huongea bila maarifa;

maneno yake hayana busara.’

3634:36 Ay 6:29; 22:15Laiti Ayubu angejaribiwa hadi kikomo cha mwisho,

kwa sababu anajibu kama mtu mwovu!

37Kwenye dhambi yake huongeza uasi;

kwa dharau hupiga makofi miongoni mwetu,

na kuzidisha maneno yake dhidi ya Mungu.”