Ayubu 33 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Ayubu 33:1-33

Elihu Anamkemea Ayubu

133:1 Ay 32:10; 6:28; 13:6“Lakini Ayubu, sasa, sikiliza maneno yangu;

zingatia kila kitu nitakachosema.

2Karibu nitafungua kinywa changu;

maneno yangu yapo katika ncha ya ulimi wangu.

333:3 Ay 27:4; 36:4Maneno yangu yanatoka katika moyo mnyofu;

midomo yangu hunena kwa uaminifu yale niyajuayo.

433:4 Mwa 2:7; Ay 10:3; 27:3Roho wa Mungu ameniumba;

pumzi ya Mwenyezi hunipa uhai.

533:5 Ay 13:18Unijibu basi, kama unaweza;

jiandae kunikabili mimi.

633:6 Ay 9:32; 4:19Mimi ni kama wewe mbele za Mungu;

mimi pia nimetolewa kwenye udongo.

733:7 Ay 13:21; 2Kor 2:4Huna sababu ya kuniogopa,

wala mkono wangu haupaswi kukulemea.

8“Lakini umesema nikiwa ninakusikia,

nami nilisikia maneno yenyewe:

933:9 Ay 10:7; 9:30; 16:17‘Mimi ni safi na sina dhambi;

mimi ni safi na sina hatia.

1033:10 Ay 13:24Lakini bado Mungu amepata dosari kwangu,

naye ananiona kama adui yake.

1133:11 Ay 13:27; Mit 3:6; Isa 30:21Ananifunga miguu kwa pingu,

tena anaziangalia njia zangu zote kwa karibu.’

1233:12 Mhu 7:20; Za 8:4; Isa 55:8-9“Lakini mimi ninakuambia, katika jambo hili wewe una makosa,

kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mwanadamu.

1333:13 Ay 40:2; Isa 45:9Kwa nini unamlalamikia

kwamba yeye hamjibu mwanadamu?

1433:14 Za 62:11; Mwa 30:2; Mt 27:19Kwa kuwa Mungu husema, wakati huu kwa njia moja,

au wakati mwingine kwa njia nyingine,

ingawa mwanadamu anaweza asielewe.

1533:15 Mwa 30:2; Mt 27:19Mungu husema na mwanadamu katika ndoto,

katika maono ya usiku,

wakati usingizi mzito uwaangukiapo

wanadamu wasinziapo vitandani mwao,

1633:16 Ay 36:10anaweza akasemea masikioni mwao,

na kuwatia hofu kwa maonyo,

1733:17 Ay 36:10, 15; 6:4; Za 88:15-16ili kumgeuza mtu kutoka kwenye kutenda mabaya

na kumwepusha na kiburi,

1833:18 Yn 2:6; Zek 9:11; Ay 15:22; Mt 26:52kuiokoa nafsi yake na shimo,

uhai wake usiangamizwe kwa upanga.

1933:19 Kum 8:5; Za 6:2; Isa 38:13Mtu anaweza kutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake,

kwa dhiki za mfululizo katika mifupa yake,

2033:20 Za 102; 4; 107:18; Ay 3:24kiasi kwamba maisha yake yenyewe yanakataa chakula

nayo nafsi yake ikakichukia kabisa hata chakula kizuri.

2133:21 Ay 2:5; 16:8Nyama ya mwili wake huisha kwa kukonda,

nayo mifupa yake ambayo mwanzoni ilikuwa imefichika,

sasa inatokeza nje.

2233:22 Ay 38:17; Za 9:13; 88:3; 107:18; 116:3Nafsi yake inakaribia kaburi,

nao uhai wake karibu na wajumbe wa kifo.

2333:23 Ay 36:9-10; Mik 6:8; Gal 3:19; Ebr 8:6; 9:15; Ay 36:9-10; Mik 6:8“Kama bado kuna malaika upande wake

kama mtetezi, mmoja miongoni mwa elfu,

wa kumwambia mwanadamu lililo jema kwake,

2433:24 Isa 38:17kumwonea huruma na kusema,

‘Mwokoe asije akatumbukia shimoni;

nimepata ukombozi kwa ajili yake’:

2533:25 2Fal 5:14ndipo nyama ya mwili wake hufanywa mpya kama ya mtoto;

hurudishwa upya kama siku za ujana wake.

2633:26 Mit 8:35; 2Fal 20:2-5; Lk 2:52; Ezr 3:13; Za 13:5Humwomba Mungu, akapata kibali kwake,

huuona uso wa Mungu na kushangilia kwa furaha;

Mungu humrudisha katika hali yake ya uadilifu.

2733:27 Hes 22:34; 2Sam 12:13; Ezr 9:13; Yak 2:13; Lk 15:21Ndipo huja mbele za watu na kusema,

‘Nilitenda dhambi na kupotosha kilichokuwa haki,

lakini sikuadhibiwa kama nilivyostahili.

2833:28 Kut 15:13; Za 34:22; 107:20; Ay 17:16; 22:20Alinikomboa nafsi yangu nisitumbukie shimoni,

nami nitaishi ili kuufurahia mwanga.’

2933:29 Yer 10:23; Flp 2:13“Mungu hufanya haya yote kwa mwanadamu;

mara mbili hata mara tatu,

3033:30 Za 49:19; Isa 53:11; Zek 9:11ili aigeuze nafsi yake toka shimoni,

ili nuru ya uzima imwangazie.

3133:31 Yer 23:18; Ay 32:10“Ayubu, zingatia, nisikilize mimi;

nyamaza, nami nitanena.

3233:32 Ay 6:29; 35:2Kama unalo lolote la kusema, unijibu;

sema, kwa maana ninataka uonekane huna hatia.

3333:33 Mit 10:8, 10, 19; Za 34:11Lakini kama huna la kusema, basi nisikilize mimi;

nyamaza, nami nitakufundisha hekima.”