Ayubu 32 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Ayubu 32:1-22

Sehemu Ya Tatu: Mazungumzo Ya Elihu

(Ayubu 32–37)

Elihu Awakemea Rafiki Za Ayubu

132:1 Ay 2:3; 10:7Basi watu hawa watatu wakaacha kumjibu Ayubu, kwa kuwa alikuwa mwadilifu machoni pake mwenyewe. 232:2 Mwa 22:21; Ay 13:19; 35:2Lakini Elihu mwana wa Barakeli, wa kabila la Buzi wa jamaa ya Ramu, akamkasirikia sana Ayubu, kwa sababu ya kujihesabia haki mwenyewe badala ya Mungu. 332:3 Ay 42:7; 32:12-13; 15:13Pia aliwakasirikia hao rafiki watatu wa Ayubu, kwa sababu hawakuweza kupata njia ya kuthibitisha ya kuwa hayo maneno ya Ayubu hayakuwa ya kweli, nao bado walikuwa wamemlaumu. 432:4 Law 19:32Basi Elihu alikuwa amesubiri kwanza waongee na Ayubu kwa sababu walikuwa na umri mkubwa kumliko yeye. 5Lakini alipoona watu hao watatu hawakuwa na kitu zaidi cha kusema, hasira yake ikaamka.

632:6 Ay 15:10Basi Elihu mwana wa Barakeli wa kabila la Buzi akasema:

“Mimi ni mdogo kwa umri,

nanyi ni wazee;

ndiyo sababu niliogopa,

sikuthubutu kuwaambia kile ninachojua.

732:7 1Nya 29:15; 2Nya 10:6Nilifikiri, ‘Yafaa umri useme,

nao wingi wa miaka ungefundisha hekima.’

832:8 Ay 27:3; 33:4; Mit 2:6; 1Fal 3:9Lakini ni Roho iliyoko ndani ya mwanadamu,

pumzi ya Mwenyezi, ndiyo impayo yeye ufahamu.

932:9 1Kor 1:21-26Sio wazee peke yao walio na hekima,

sio wenye umri mkubwa peke yao wanaofahamu lililo sawa.

1032:10 Ay 33:1; 31:33; Za 34:11; Ay 5:27“Kwa hiyo nasema: Nisikilizeni mimi;

mimi nami nitawaambia lile ninalojua.

11Nilingojea mlipokuwa mnaongea,

nilizisikiliza hoja zenu;

mlipokuwa mkitafuta maneno ya kusema,

1232:12 Ay 32:3niliwasikiliza kwa makini.

Lakini hakuna hata mmoja wenu

aliyethibitisha kwamba Ayubu amekosa;

hakuna hata mmoja wenu

aliyeweza kujibu hoja zake.

1332:13 Mhu 9:11; Yer 9:23Msiseme, ‘Tumepata hekima;

Mungu na amthibitishe kuwa mwongo,

wala si mwanadamu.’

1432:14 Ay 23:4Lakini Ayubu hajayapanga maneno yake dhidi yangu,

nami sitamjibu kwa kutumia hoja zenu.

1532:15 Ay 32:1“Wametiwa hofu na hawana la zaidi la kusema;

maneno yamewaishia.

16Je, ningoje sasa kwa sababu wamekuwa kimya,

kwa vile sasa wanasimama bila kuwa na la kujibu?

1732:17 Ay 5:27; 33:3; 36:4Mimi nami nitakuwa na la kusema;

mimi nami nitasema lile nilijualo.

1832:18 Mdo 4:20; 1Kor 9:16; 2Kor 5:14Kwa kuwa nimejawa na maneno,

nayo Roho iliyomo ndani yangu yanisukuma;

1932:19 Yer 20:9; Amo 3:8; Mt 9:17ndani yangu niko kama chupa iliyojazwa divai,

kama kiriba kipya cha divai kilicho tayari kupasuka.

2032:20 Ay 4:2; Yer 6:11Ni lazima niseme ili niweze kutulia;

ni lazima nifumbue midomo yangu nipate kujibu.

2132:21 Law 19:15; 2Nya 19:7; Mt 22:16Sitampendelea mtu yeyote,

wala sitajipendekeza kwa mtu yeyote;

2232:22 Ay 4:17; 9:9; Za 12:2-4kwa kuwa kama ningekuwa stadi wa kujipendekeza,

Muumba wangu angeniondolea mbali kwa upesi.