Ayubu Anamaliza Utetezi Wake
129:1 Za 18:28; Ay 13:12Ayubu akaendelea na hoja yake, akasema:
229:2 Yer 1:12; 44:27“Tazama jinsi ninavyoitamani miezi iliyopita,
zile siku ambazo Mungu alikuwa akinilinda,
329:3 Ay 11:17; 12:25wakati taa yake iliniangazia kichwani changu,
na kwa mwanga wake Mungu nikapita katikati ya giza!
429:4 Za 25:14; Mit 3:32Natamani siku zile nilizokuwa katika ustawi wangu,
wakati urafiki wa Mungu wa ndani ulipoibariki nyumba yangu,
529:5 Za 127:3-5; 128:3; Rum 4:1wakati Mwenyezi alikuwa pamoja nami,
nao watoto wangu walikuwa wamenizunguka,
629:6 Ay 20:17; Za 81:16; Mwa 49:20; Kum 32:13wakati njia yangu ilikuwa imenyweshewa siagi,
nao mwamba ukanimiminia vijito vya mafuta ya zeituni.
729:7 Ay 5:4; 31:21; Yer 20:2; 38:7“Wakati nilipokwenda kwenye lango la mji
na kuketi katika kiwanja,
829:8 1Tim 5:1; Law 19:32vijana waliniona wakakaa kando,
nao wazee walioketi wakasimama;
929:9 Amu 16:19; Mit 30:32wakuu wakaacha kuzungumza
na kuziba vinywa vyao kwa mikono yao;
1029:10 Za 137:6wenye vyeo wakanyamazishwa,
nazo ndimi zao zikagandamana na makaakaa ya vinywa vyao.
1129:11 Ay 4:4; Ebr 11:4Yeyote aliyenisikia alinena mema juu yangu,
nao walioniona walinisifu,
1229:12 Kum 24:17; Ay 31:17-21; Za 72:12; Mit 21:13kwa sababu nilimwokoa maskini aliyeomba msaada,
naye yatima aliyekuwa hana wa kumsaidia.
1329:13 Ay 31:20; 22:9; Kum 10:18Mtu aliyekuwa karibu kufa alinibariki,
nami niliufanya moyo wa mjane kuimba.
1429:14 2Sam 8:15; Rum 13:14; Efe 6:14Niliivaa haki kama vazi langu;
uadilifu ulikuwa joho langu na kilemba changu.
1529:15 Hes 10:31Nilikuwa macho ya kipofu
na miguu kwa kiwete.
1629:16 Ay 24:4; Mit 29:7Nilikuwa baba kwa mhitaji;
nilimtetea mgeni.
1729:17 Ay 24:9; 4:10, 11; Za 3:7Niliyavunja meno makali ya waovu,
na kuwapokonya wahanga kwenye meno yao.
1829:18 Za 62:2; Mit 3:1-2“Nikafikiri, ‘Nitafia katika nyumba yangu mwenyewe,
nazo siku zangu zitakuwa nyingi kama chembechembe za mchanga.
1929:19 Hes 24:6; Yer 17:8Mizizi yangu itafika mpaka kwenye maji,
nao umande utakaa juu ya matawi yangu usiku kucha.
2029:20 Za 18:34; Isa 38:12; Mwa 49:24Utukufu wangu utabakia kuwa mpya ndani yangu,
upinde wangu daima utaendelea kuwa mpya mkononi mwangu.’
2129:21 Ay 29:21“Watu walinisikiliza kwa tumaini,
wakingojea ushauri wangu kwa utulivu.
2229:22 Kum 32:2Baada ya mimi kuzungumza, hawakusema zaidi;
maneno yangu yaliingia masikioni mwao kwa makini.
23Waliningojea kama manyunyu ya mvua
na kuyapokea maneno yangu
kama ardhi inyonyavyo mvua ya vuli.
24Walipokata tamaa niliwaonyesha uso wa furaha;
nuru ya uso wangu ilikuwa ya thamani kwao.
2529:25 Ay 31:31; 4:4Niliwachagulia njia na kukaa kama mkuu wao;
niliishi kama mfalme katikati ya majeshi yake;
nikawa kama yeye anayewafariji waombolezaji.