Ayubu 28 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Ayubu 28:1-28

Mapumziko: Imani Inakopatikana

128:1 Za 12:6; 66:10; Yer 9:7; Mal 3:3; Dan 11:35“Kuna machimbo ya fedha,

na mahali dhahabu isafishwapo.

228:2 Kum 8:9Chuma hupatikana ardhini,

nayo shaba huyeyushwa kutoka mawe ya madini.

328:3 Mhu 7:25; 8:17; Mit 2:4Mwanadamu hukomesha giza;

huyatafuta hadi sehemu iliyo mbali,

kwa ajili ya kuchimbua mawe yenye madini

katika giza jeusi sana.

428:4 2Sam 5:8Huchimba shimo jembamba mbali na makao ya watu,

mahali paliposahaulika na nyayo za wanadamu;

mbali na wanadamu huningʼinia na kupembea kwa kamba.

528:5 Mwa 1:29; Za 145:15Ardhi, ambako chakula hutoka,

chini hugeuzwa kwa moto;

628:6 Isa 54:11; Wim 5:14; Ay 22:24yakuti samawi hutoka katika miamba yake,

nalo vumbi lake lina vipande vya dhahabu.

728:7 Ay 28:21Hakuna ndege awindaye aijuaye njia ile iliyofichika,

wala hakuna jicho la mwewe lililoiona.

828:8 Ay 41:34; Isa 35:9Wanyama wa porini wanaotamba hawajawahi kupakanyaga,

wala simba azungukaye huko.

928:9 Kum 8:15; Yn 2:6Mikono ya mwanadamu hushambulia miamba migumu sana,

na kuiacha wazi mizizi ya milima.

1028:10 Mit 2:4; Ay 28:4Hutoboa shimo refu la kupenya chini kwa chini kwenye miamba;

macho yake huona hazina zake zote.

1128:11 Mwa 7:11; Isa 48:6; Yer 33:3Hutafuta vyanzo vya mito

na kuvileta vitu vilivyofichika katika nuru.

1228:12 Mit 1:20; Mhu 7:24“Lakini hekima inaweza kupatikana wapi?

Ufahamu unakaa wapi?

1328:13 Mit 3:15; Mt 13:44-46Mwanadamu hatambui thamani yake;

haiwezi kupatikana katika nchi ya walio hai.

14Kilindi husema, ‘Haiko ndani yangu’;

bahari nayo husema, ‘Haiko pamoja nami.’

1528:15 Mit 16:16; Mdo 8:20Haiwezi kununuliwa kwa dhahabu safi kuliko zote,

wala thamani yake haiwezi kupimwa kwa fedha.

16Haiwezi kununuliwa kwa dhahabu ya Ofiri,

kwa shohamu ya thamani kubwa au yakuti samawi ya thamani kubwa.

1728:17 Za 119:72; Mit 8:10; Ay 28:15Dhahabu wala mawe maangavu haviwezi kulinganishwa nayo,

wala haiwezi hubadilishwa na vito vya dhahabu.

18Marijani na yaspi hazistahili kutajwa;

thamani ya hekima ni zaidi ya akiki nyekundu.

1928:19 Mit 3:14-15; 8:10-19Yakuti manjano ipatikanayo Kushi haiwezi kulinganishwa nayo,

wala haiwezi kununuliwa kwa dhahabu safi.

20“Ni wapi basi hekima itokako?

Ufahamu hukaa wapi?

2128:21 Ay 28:7Imefichika machoni pa kila kitu kilicho hai,

imesitiriwa hata kwa ndege wa angani.

2228:22 Ay 26:6Uharibifu na Mauti husema,

‘Ni uvumi wake tu uliotufikia masikioni mwetu.’

2328:23 Mdo 15:18; Ay 22:22; Mit 8:22-31Mungu anaifahamu njia ya kuiendea hekima

na ndiye peke yake anayefahamu inakokaa,

2428:24 Isa 11:12; Yos 3:11; Ebr 4:13; Za 66:7kwa maana yeye huitazama miisho ya dunia

na huona kila kitu chini ya mbingu.

2528:25 Ay 38:8-11; Za 135:7Alipofanyiza nguvu za upepo

na kuyapima maji,

2628:26 Ay 38:25-27; Isa 35:7; Yer 14:22alipofanya maagizo kwa ajili ya mvua

na njia kwa ajili ya umeme wa radi,

27ndipo alipoitazama hekima na kuikadiria thamani yake,

akaithibitisha na kuihakikisha.

2828:28 Kut 20:20; Kum 4:6Naye Mungu akamwambia mwanadamu,

‘Kumcha Bwana: hiyo ndiyo hekima,

nako kujitenga na uovu ndio ufahamu.’ ”