Ayubu 26 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version

Ayubu 26:1-14

Hotuba Ya Tisa Ya Ayubu

Ayubu Anajibu: Utukufu Wa Mungu Hauchunguziki

1Kisha Ayubu akajibu:

226:2 Ay 6:12; 4:3; Za 71:9; Mit 25:11“Tazama jinsi ulivyomsaidia mtu asiye na uwezo!

Jinsi ulivyouokoa mkono ulio dhaifu!

326:3 Ay 34:35Ni shauri gani ulilompa yeye asiye na hekima?

Nayo ni busara gani kubwa uliyoonyesha!

426:4 1Fal 22:24Ni nani aliyekusaidia kutamka maneno hayo?

Nayo ni roho ya nani iliyosema kutoka kinywani mwako?

526:5 Za 88:10; Isa 14:9“Wafu wako katika maumivu makuu,

wale walio chini ya maji na wale waishio ndani yake.

626:6 Za 139:8; Mit 15:11; Ebr 4:13; Amo 9:2Mauti26:6 Yaani Kuzimu; Kiebrania ni Sheol. iko wazi mbele za Mungu;

Uharibifu26:6 Kwa Kiebrania ni Abadon. haukufunikwa.

726:7 Ay 9:826:7 Ay 8:22; 31:35Hutandaza anga la kaskazini mahali patupu;

naye huiningʼiniza dunia mahali pasipo na kitu.

826:8 Mit 30:4; Za 147:8Huyafungia maji kwenye mawingu yake,

hata hivyo mawingu hayapasuki kwa uzito wake.

926:9 2Sam 22:10; Za 97:2Huufunika uso wa mwezi mpevu,

akitandaza mawingu juu yake.

1026:10 Mit 8:27; Isa 40:22; Ay 28:3Amechora mstari wa upeo juu ya uso wa maji,

ameweka mpaka wa nuru na giza.

1126:11 2Sam 22:8Nguzo za mbingu nazo zatetemeka,

zinatishika anapozikemea.

1226:12 Isa 51:15; Kut 14:21; Yer 31:35; Ay 12:13; Kut 14:21; Ay 12:13; 9:13Kwa nguvu zake aliisukasuka bahari;

kwa hekima yake alimkata Rahabu26:12 Rahabu hapa ni fumbo la kumaanisha Lewiathani, mnyama mkubwa wa baharini mwenye magamba anayefanana na joka kubwa, mwenye umbo la kutisha, asiyeweza kuvuliwa. vipande vipande.

1326:13 Za 33:6; Isa 27:1Aliisafisha anga kwa pumzi yake;

kwa mkono wake alimchoma joka aendaye mbio.

1426:14 Ay 9:6; 36:29Haya ni mambo madogo tu katika matendo yake;

tazama jinsi ulivyo mdogo mnongʼono tunaousikia kumhusu!

Ni nani basi awezaye kuelewa

ngurumo za nguvu zake?”

Chinese Contemporary Bible 2023 (Traditional)

約伯記 26:1-14

約伯的回答

1約伯回答說:

2「你真是幫了軟弱者的大忙!

救了臂膀無力的人!

3無智慧的人真多虧你的指教!

承蒙你的真知灼見!

4誰幫你說出這些話?

誰的靈在藉著你發言?

5「陰魂和水族在水底顫抖,

6陰間裸露在祂面前,

滅亡之地毫無遮掩。

7祂將北極鋪在空中,

將地懸在虛無中;

8祂將水捲在密雲中,

雲負重卻不裂開。

9祂遮蓋自己的寶座26·9 「寶座」或譯「滿月」。

把雲彩鋪在上面。

10祂在海面上畫出地平線,

作為光明與黑暗的交界。

11祂的斥責使天柱震動驚駭,

12祂的能力使大海平靜,

祂運用智慧擊碎海怪。

13祂吹的氣使天空晴朗,

祂揮手刺穿逃跑的蛇。

14看啊,這不過是祂作為的一斑,

是我們聽到的點滴微音!

誰能領悟祂的雷霆萬鈞?」