Ayubu 25 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Ayubu 25:1-6

Bildadi Anasema: Mwanadamu Awezaje Kuwa Mwadilifu Mbele Za Mungu?

125:1 Ay 8:1Ndipo Bildadi Mshuhi akajibu:

225:2 Zek 9:2; Ufu 1:6“Mamlaka na kuheshimiwa ni vyake Mungu;

yeye huthibitisha amani katika mbingu juu.

325:3 Mt 5:45; Yak 1:17; Mwa 1:14-16Je, majeshi yake yaweza kuhesabika?

Ni nani asiyeangaziwa na nuru yake?

425:4 Ay 4:17; 14:4; Rum 3:19-20Mtu awezaje kuwa mwadilifu mbele za Mungu?

Awezaje mtu aliyezaliwa na mwanamke kuwa safi?

525:5 Ay 31:26; 4:18Ikiwa hata mwezi sio mwangavu

nazo nyota si safi machoni pake,

625:6 Za 22:6; 80:17; Eze 2:1; Ay 7:5sembuse mtu ambaye ni funza:

mwanadamu ambaye ni buu tu!”