Ayubu 24 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Ayubu 24:1-25

Ayubu Analalamikia Jeuri Duniani

124:1 Yer 46:10; 2Pet 3:7; Ay 15:20; Mdo 1:7“Kwa nini Mwenyezi asiweke nyakati kwa ajili ya hukumu?

Kwa nini wale wamjuao wazitafute siku kama hizo bila mafanikio?

224:2 Kum 19:14; 27:17; Mit 23:10Watu husogeza mawe ya mpaka;

huchunga makundi ya wanyama waliyonyangʼanya kwa nguvu.

324:3 Kum 24:6-10; 12:17; Ay 6:27Huwanyangʼanya yatima punda wao,

na kumchukua rehani fahali wa mjane.

424:4 Mit 28:28; Ay 20:19; Isa 11:4; Za 12:5Humsukuma mhitaji kutoka njia,

na kuwafanya maskini wote wa nchi kulazimika kujificha.

524:5 Mwa 16:12; Za 104:23; Ay 30:3Kama punda-mwitu jangwani,

maskini huzunguka katika kazi zao za kutafuta chakula;

mahali palipo jangwa

huwapa chakula cha watoto wao.

624:6 Ay 6:5; Rut 2:22; 1Fal 21:19Hukusanya chakula mashambani na kuokota masazo

katika mashamba ya mizabibu ya waovu.

724:7 Kut 22:26-27; Kum 24:12; Ay 22:6Kwa kukosa nguo, usiku kucha hukaa uchi;

hawana chochote cha kujifunika baridi.

824:8 Dan 4:25, 33; Mao 4:5Hutota kwa mvua za mlimani,

nao huikumbatia miamba kwa ajili ya kukosa pa kujisitiri.

924:9 Kum 24:17Mtoto yatima hupokonywa matitini;

mtoto wachanga wa maskini hunyakuliwa kwa ajili ya deni.

1024:10 Kum 24:12-13; Law 19:9Kwa kukosa nguo, hutembea uchi;

hubeba miganda ya ngano, lakini huwa na njaa.

1124:11 Isa 5:2; 16:10; Hag 2:16; Mik 6:15Hukamua zeituni katika mawe ya kusagia;

hukanyaga mashinikizo, lakini wanaona kiu.

1224:12 Isa 30:19; Ay 9:23; Ufu 6:10; Mhu 8:11Kilio cha huzuni cha wanaokufa kinapaa kutoka mjini,

nazo nafsi za waliojeruhiwa zinalilia msaada.

Lakini Mungu hamlaumu mtu yeyote

kwa kutenda mabaya.

1324:13 Ay 38:15; 1The 5:4-5; Za 18:28; Efe 5:8-14“Wako wale wanaoiasi nuru,

wasiofahamu njia zake

wala hawakai katika mapito yake.

1424:14 Isa 3:15; Mik 3:3; Ay 20:19; Za 37:32; 10:9Wakati mwanga wa mchana unapotoweka, muuaji huinuka

naye huwaua maskini na mhitaji;

wakati wa usiku hunyemelea kama mwizi.

1524:15 Mit 7:8-9; Za 10:11Jicho la mzinzi hungojea wakati wa giza,

naye hufikiri, ‘Hakuna jicho litakaloniona,’

naye huuficha uso wake.

1624:16 Kut 22:2; Mt 6:19; Yn 3:20Katika giza, huvunja majumba,

lakini wakati wa mchana hujifungia ndani;

hawataki kufanya lolote nuruni.

1724:17 Ay 18:11; 15:22; 18:5Kwa wote hawa, giza nene ndiyo asubuhi yao;

hujifanya rafiki na vitisho vya gizani.

1824:18 Ay 9:26; 22:16; Yud 23; Isa 57:20“Lakini wao ni povu juu ya maji;

sehemu yao juu ya nchi imelaaniwa,

hivyo hakuna hata mmoja

aendaye kwenye shamba la mizabibu.

1924:19 Ay 6:17; 21:13Kama vile joto na hari vinyakuavyo theluji iliyoyeyuka,

ndivyo kuzimu kuwanyakuavyo waliotenda dhambi.

2024:20 Ay 18:17; Mit 10:7; Dan 4:14; Za 31:12Tumbo lililowazaa huwasahau,

nao huwa karamu ya mabuu;

watu waovu hawakumbukwi tena,

lakini huvunjika kama mti.

2124:21 Ay 22:9Huwafanya mawindo wanawake tasa na wasio na watoto,

nao hawaonyeshi huruma kwa wajane.

2224:22 Kum 28:66; Mt 6:27Lakini Mungu huwakokota wenye nguvu kwa uwezo wake;

ingawa wamestawi, hawana hakika ya maisha.

2324:23 Ay 9:24; Amo 6:1; 2Nya 16:9; Ay 10:4Aweza akawaacha wakapumzika wakijihisi salama,

lakini macho yake yanaona njia zao.

2424:24 2Fal 19:35; Za 37:35-36; 83:13; Isa 17:5Kwa kitambo kidogo hutukuka, hatimaye hutoweka;

hushushwa na kukusanywa kama wengine wote,

hukatwa kama masuke ya nafaka.

2524:25 Ay 16:17; 27:4“Kama hili sivyo, ni nani awezaye kunithibitisha kuwa mwongo,

na kuyafanya maneno yangu kuwa si kitu?”