Hotuba Ya Nane Ya Ayubu
Ayubu Anajibu: Kulalamika Kwangu Ni Uchungu
1Ndipo Ayubu akajibu:
223:2 Ay 6:3; 7:11; 1Sam 1:10“Hata leo malalamiko yangu ni chungu;
mkono wake ni mzito juu yangu hata nikiugua.
323:3 Kum 4:29Laiti ningefahamu mahali pa kumwona;
laiti ningeweza kwenda mahali akaapo!
423:4 Ay 13:18; 9:15Ningeliweka shauri langu mbele zake,
na kukijaza kinywa changu na hoja.
5Ningejua kwamba angenijibu nini,
na kuelewa lile ambalo angelisema.
623:6 Ay 9:4, 19; Isa 27:4Je, angenipinga kwa nguvu nyingi?
La, asingenigandamiza.
723:7 Mwa 3:8; Ay 9:3Hapo mtu mwadilifu angeweka shauri lake mbele zake,
nami ningeokolewa milele na mhukumu wangu.
8“Lakini nikienda mashariki, hayupo;
nikienda magharibi, simpati.
923:9 Ay 9:11Anapokuwa kazini pande za kaskazini, simwoni;
akigeukia kusini, nako simwoni hata kidogo.
1023:10 Za 66:10; 139:1-3; 12:6; 1Pet 1:7; Yak 1:12Lakini anaijua njia niiendeayo;
akiisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu.
1123:11 Za 17:5; Ay 31:7; Yer 11:20; Za 44:18; 125:5Nyayo zangu zimefuata hatua zake kwa karibu;
nimeishika njia yake bila kukengeuka.
1223:12 Ay 6:10; 15:11; Yn 4:32, 34; Mt 4:4Sijaziacha amri zilizotoka midomoni mwake;
nimeyathamini maneno ya kinywa chake kuliko chakula changu cha kila siku.
1323:13 Za 115:3; Isa 55:11; Mhu 3:14; Rum 9:19“Lakini yeye husimama peke yake; ni nani awezaye kumpinga?
Yeye hufanya lolote atakalo.
1423:14 1The 3:3; 1Pet 4:12Hutimiliza maagizo yake dhidi yangu,
na bado anayo mipango mingi kama hiyo ambayo ameiweka akiba.
1523:15 Mwa 45:3; Yos 24:14; Mhu 3:14; 12:13; 2Kor 5:11Hiyo ndiyo sababu ninaingiwa na hofu mbele zake;
nifikiriapo haya yote ninamwogopa.
1623:16 Za 22:14; Yer 51:46; Ay 27:223:16 Kum 20:3; Ay 27:2; Kut 3:6; Ufu 6:16Mungu ameufanya moyo wangu kuzimia;
yeye Mwenyezi amenitia hofu.
1723:17 Ay 3:6; 6:9; 19:8Hata hivyo sijanyamazishwa na giza,
wala kwa giza nene linalofunika uso wangu.