Ayubu 22 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Ayubu 22:1-30

Elifazi Anasema: Uovu Wa Ayubu Ni Mkubwa

122:1 Ay 4:1Ndipo Elifazi Mtemani akajibu:

222:2 Lk 17:10; Za 16:2“Je, mwanadamu aweza kuwa wa faida kwa Mungu?

Je, hata mtu mwenye hekima aweza kumfaidi?

322:3 Isa 1:11; Hag 1:8; Za 143:2; Ay 35:7; Za 9:12Je, Mwenyezi angefurahia nini

kama ungekuwa mwadilifu?

Au je, yeye angepata faida gani

kama njia zako zingekuwa kamilifu?

422:4 Isa 3:14; Eze 20:35“Je, ni kwa ajili ya utaua wako ndiyo maana anakukemea

na kuleta mashtaka dhidi yako?

522:5 Ezr 9:13; Ay 11:6; Ezr 9:13; Ay 15:5; 15:13; 20:29; 29:17Je, uovu wako si mkuu?

Dhambi zako si hazina mwisho?

622:6 Kum 24:6, 17; Eze 18:12-16Umedai dhamana kwa ndugu zako bila sababu;

umewavua watu nguo zao, ukawaacha uchi.

722:7 Ay 31:16-17; Eze 18:7; Mt 25:42Hukumpa maji aliyechoka,

nawe ulimnyima chakula mwenye njaa,

822:8 Ay 15:19; Isa 3:3; 5:13; 9:15; Ay 12:19ingawa ulikuwa mtu mwenye uwezo ukimiliki nchi:

mtu uliyeheshimiwa, ukiishi ndani yake.

922:9 Isa 10:2; Lk 1:53Umewafukuza wajane mikono mitupu

na kuzivunja nguvu za yatima.

1022:10 Ay 18:9; 10:3; 15:21Ndiyo sababu mitego imekuzunguka pande zote,

hatari ya ghafula inakutia hofu,

1122:11 Ay 5:14; Isa 58:10-11; Mao 3:54ndiyo sababu ni giza sana huwezi kuona,

tena ndiyo sababu mafuriko ya maji yamekufunika.

1222:12 Ay 11:8; 16:19“Je, Mungu hayuko katika mbingu za juu?

Juu kuliko nyota zilizo juu sana!

1322:13 Eze 9:9; Efe 6:2; Sef 1:12; Za 139:11Hivyo wewe wasema, ‘Mungu anajua nini?’

Je, yeye huhukumu katika giza kama hilo?

1422:14 Ay 26:9; Za 97:2; 105:39; 105:13; 2Fal 21:16; Ay 37:18; Za 18:11; Mit 8:27; Yer 23:23-24Mawingu mazito ni pazia lake, hivyo hatuoni sisi

atembeapo juu ya anga la dunia.

1522:15 Mwa 6:11-13Je, utaifuata njia ya zamani,

ambayo watu waovu waliikanyaga?

1622:16 Ay 15:32; Mwa 7:23; Mt 7:26-27Waliondolewa kabla ya wakati wao,

misingi yao ikachukuliwa na mafuriko.

1722:17 Ay 21:15Walimwambia Mungu, ‘Tuache sisi!

Huyo Mwenyezi aweza kutufanyia nini?’

1822:18 Ay 12:6; 21:16Lakini ndiye alizijaza nyumba zao na vitu vizuri,

hivyo ninajitenga mbali na mashauri ya waovu.

1922:19 Za 64:10; 97:12; Ay 21:3“Wenye haki wanaona maangamizi yao na kufurahi,

nao wasio na hatia huwadhihaki, wakisema,

2022:20 Ay 15:30‘Hakika adui zetu wameangamizwa,

nao moto umeteketeza mali zao.’

2122:21 Mit 3:10; 1Pet 5:6; Isa 27:5“Mjue sana Mungu ili uwe na amani,

ndipo mema yatakapokujia.

2222:22 Kum 8:3; Ay 6:10; Eze 3:10; Mit 2:6; Za 37:31Uyapokee mafundisho toka kinywani mwake,

na maneno yake uyaweke moyoni mwako.

2322:23 Isa 19:22; 44:22; Eze 18:32; Mdo 20:32; Ay 11:14Kama ukimrudia Mwenyezi, utarudishwa upya:

Kama ukiuondoa uovu uwe mbali na hema lako,

2422:24 Isa 2:20; 30:22kama dhahabu yako ukiihesabu kama mavumbi,

dhahabu yako ya Ofiri kama miamba ya mabondeni,

2522:25 2Fal 18:7; Mt 6:20-21ndipo Mwenyezi atakuwa dhahabu yako,

naye atakuwa fedha yako iliyo bora.

2622:26 Za 2:8; Isa 61:10Hakika ndipo utakapojifurahisha kwa Mwenyezi,

nawe utamwinulia Mungu uso wako.

2722:27 Ay 5:27; Isa 58:9Utamwomba yeye, naye atakusikia,

nawe utazitimiza nadhiri zako.

2822:28 Za 103:11; 145:19; Ay 33:28; Mit 4:18; Za 97:11Utakusudia jambo nalo litatendeka,

nao mwanga utaangazia njia zako.

2922:29 Za 18:27; 1Pet 5:5Watu watakaposhushwa, nawe ukasema, ‘Wainue!’

ndipo atamwokoa aliyevunjika moyo.

3022:30 2Sam 22:21; Ay 42:7-8Atamwokoa hata yule ambaye ana hatia,

ataokolewa kwa sababu ya usafi wa mikono yako.”