Sofari Anasema: Uovu Hupokea Malipo Ya Haki
120:1 Ay 2:11Ndipo Sofari Mnaamathi akajibu:
220:2 Za 42:5; Mao 1:20“Mawazo yanayonisumbua yananisukuma kujibu,
kwa sababu nimehangaika sana.
320:3 Ay 19:3Ninasikia makaripio ambayo yananivunjia heshima,
nao ufahamu wangu unanisukuma kujibu.
420:4 Kum 4:32; Ay 32:7“Hakika unajua jinsi ilivyokuwa tangu zamani,
tangu zamani mwanadamu alipowekwa duniani,
520:5 Ay 8:12; Za 73:19; 37:35macheko ya mtu mwovu ni ya muda mfupi,
nayo furaha ya wasiomcha Mungu hudumu kwa kitambo tu.
620:6 Ay 33:17; Isa 16:6; Mwa 11:4; Isa 14:13-14; Oba 1:3-4Ingawa kujikweza kwake hufikia mbinguni
na kichwa chake hugusa mawingu,
720:7 Ay 4:20; 7:8; 14:20ataangamia milele kama mavi yake mwenyewe.
Wale waliomwona watauliza, ‘Yuko wapi?’
820:8 Za 90:5; 73:20; Mhu 6:12; 12:7; Ay 18:11-18; Isa 17:14; 29:7Kama ndoto hutoweka, wala hapatikani tena,
amefukuziwa mbali kama maono ya usiku.
920:9 Ay 7:8Jicho lililomwona halitamwona tena;
mahali pake hapatamwona tena.
1020:10 Ay 5:4; 20:15, 18, 20; 3:15Watoto wake watalipa yote baba yao aliyowadhulumu maskini,
nayo mikono yake itarudisha mali yote aliyonyangʼanya watu.
1120:11 Ay 13:26; 21:24; 17:16Nguvu za ujana zilizoijaza mifupa yake,
zitalala naye mavumbini.
1220:12 Ay 15:16; Za 10:7; 140:3“Ingawa uovu ni mtamu kinywani mwake
naye huuficha chini ya ulimi wake,
1320:13 Hes 11:18-20ingawa hawezi kukubali kuuachia uende,
lakini huuweka kinywani mwake.
1420:14 Za 104:26; Ay 10:18; Mwa 1:21; Ay 41:1, 8, 10, 2520:14 Mit 20:17; Yer 2:19; 4:18; Ufu 10:9; Hes 21:6Hata hivyo chakula chake kitakuwa kichungu tumboni mwake,
nacho kitakuwa sumu kali ya nyoka ndani yake.
1520:15 Ay 20:10; Law 18:25Atatema mali alizozimeza;
Mungu atalifanya tumbo lake kuzitapika.
1620:16 Kum 32:24, 34Atanyonya sumu za majoka;
meno ya nyoka mwenye sumu kali yatamuua.
1720:17 Kum 32:13-14; Ay 29:6; Yer 17:6Hatafurahia vijito,
mito inayotiririsha asali na siagi.
1820:18 Ay 20:10; 5:5; Za 109:11Vile alivyovitaabikia atavirudisha bila kuvila;
hatafurahia faida itokanayo na biashara yake.
1920:19 Kum 15:11; Amo 8:4Kwa kuwa aliwaonea maskini na kuwaacha pasipo kitu;
amenyangʼanya kwa nguvu nyumba asizozijenga.
2020:20 Mhu 5:12-14“Hakika hatakuwa na raha katika kutamani kwake sana;
hawezi kujiokoa mwenyewe kwa hazina zake.
2120:21 Ay 7:8Hakuna chochote kitakachosalia kwa ajili yake ili ale;
kufanikiwa kwake hakutadumu.
2220:22 Amu 2:15; Lk 2:16-20; Ay 20:29; 21:17, 30; 31:2-3Katikati ya wingi wa ustawi wake, dhiki itampata;
taabu itamjia kwa nguvu zote.
2320:23 Za 78:30-31Atakapokuwa amelijaza tumbo lake,
Mungu ataionyesha ghadhabu kali dhidi yake,
na kumnyeshea mapigo juu yake.
2420:24 Yer 46:21; Amo 5:19; Isa 24:18Ijapokuwa aikimbia silaha ya chuma,
mshale wa shaba utamchoma.
2520:25 Ay 18:11; 16:13; Za 88:15-16Atauchomoa katika mgongo wake,
ncha ingʼaayo kutoka ini lake.
Vitisho vitakuja juu yake;
2620:26 Ay 5:14; 1:16; 15:34; 26:6; 28:22; 31:12; Za 21:9giza nene linavizia hazina zake.
Moto usiopepewa na mtu utamteketeza,
na kuangamiza yaliyosalia nyumbani mwake.
2720:27 Kum 31:28; Isa 26:21Mbingu zitaweka wazi hatia yake,
nayo nchi itainuka kinyume chake.
2820:28 Kum 28:31; Mt 7:26-27; Hes 14:28-32; Efe 5:6Mafuriko yataichukua nyumba yake,
maji yaendayo kasi katika siku ya ghadhabu ya Mungu.
2920:29 Yer 13:25; Kum 29:20, 28; Ufu 21:8; Mt 24:51Hili ndilo fungu Mungu alilowagawia waovu,
urithi uliowekwa kwa ajili yao na Mungu.”