Ayubu 19 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Ayubu 19:1-29

Hotuba Ya Sita Ya Ayubu

Ayubu Anajibu: Najua Mkombozi Wangu Yu Hai

1Ndipo Ayubu akajibu:

219:2 1Sam 1:6; Za 6:2, 3; Ay 6:9; 13:25“Je, mtaendelea kunitesa mpaka lini,

na kuniponda kwa maneno yenu?

319:3 Mwa 31:7; Ay 20:3Mara kumi hizi mmenishutumu;

bila aibu mnanishambulia.

419:4 Ay 6:24; Za 19:12; Eze 18:4Kama ni kweli nimepotoka,

kosa langu ninabaki kuhusika nalo mwenyewe.

519:5 Za 38:16; 55:12; Mik 7:8Kama kweli mngejitukuza wenyewe juu yangu,

na kutumia unyonge wangu dhidi yangu,

619:6 Ay 6:29; 18:8; 10:3basi jueni kuwa Mungu amenitendea yaliyo mabaya,

naye amekokota wavu wake kunizunguka.

719:7 Ay 9:24; 30:20; Za 22:2; Hab 1:2-4“Ingawa ninalia, ‘Nimetendewa mabaya!’ sipati jibu;

ingawa ninaomba msaada, hakuna haki.

819:8 Mao 3:7; Hos 2:6; Mhu 6:4; Yer 14:19Yeye ameizuia njia yangu hivyo siwezi kupita;

ameyafunika mapito yangu na giza.

919:9 Ay 12:17; Za 89:39-44; Mao 5:16Amenivua heshima yangu,

na kuniondolea taji kichwani pangu.

1019:10 Ay 12:14; 7:6; 14:7Amenibomoa kila upande hadi nimeisha;

amelingʼoa tegemeo langu kama mti.

1119:11 Ay 16:9; 13:14Hasira yake imewaka juu yangu;

amenihesabu kuwa miongoni mwa adui zake.

1219:12 Ay 16:13; 16:10; 3:23Majeshi yake yananisogelea kwa nguvu;

yamenizingira,

yamepiga kambi kulizunguka hema langu.

1319:13 Ay 16:10-13; 30:12; Mt 26:56; 2Tim 4:16“Amewatenga ndugu zangu mbali nami;

wale tunaojuana nao wamefarakana nami kabisa.

1419:14 Ay 19:19; 2Sam 15:12; Ay 12:4; 16:20; Za 88:18; Yer 20:10; 38:22Watu wa jamaa yangu wamekwenda mbali;

rafiki zangu wamenisahau.

1519:15 Mwa 14:14; Mhu 2:7Wageni wangu na watumishi wangu wa kike wananiona kama mgeni;

wananitazama kama mgeni.

16Namwita mtumishi wangu, wala haitiki,

ingawa namwomba kwa kinywa changu mwenyewe.

1719:17 Za 38:5Pumzi ya kinywa changu ni kinyaa kwa mke wangu;

nimekuwa chukizo mno kwa ndugu zangu mwenyewe.

1819:18 2Fal 2:23; Ay 13:25Hata watoto wadogo hunidhihaki;

ninapojitokeza, hunifanyia mzaha.

1919:19 Za 38:11; 55:12-13; Ay 3:10Rafiki zangu wa moyoni wote wananichukia kabisa;

wale niwapendao wamekuwa kinyume nami.

2019:20 Ay 2:5Mimi nimebaki mifupa na ngozi tu;

nimeponea nikiwa karibu kufa.

2119:21 Ay 6:14; Amu 2:15; Ay 4:5; 10:3; Mao 3:1“Nihurumieni, rafiki zangu, kuweni na huruma,

kwa kuwa mkono wa Mungu umenipiga.

2219:22 Ay 13:25; 16:11; Mit 30:14; Isa 53:4Kwa nini mnanifuatia kama Mungu afanyavyo?

Hamtosheki kamwe na mwili wangu?

2319:23 Kut 17:16; Isa 30:8“Laiti maneno yangu yangewekwa kwenye kumbukumbu,

laiti kwamba yangeandikwa kwenye kitabu,

2419:24 Yer 17:1; Ay 16:18kwamba yangechorwa kwenye risasi kwa kifaa cha chuma,

au kuyachonga juu ya mwamba milele!

2519:25 Law 25:25; Mit 23:11; 1Sam 14:39; Ay 16:19Ninajua kwamba Mkombozi19:25 Au: Mtetezi. wangu yu hai,

naye kwamba mwishoni atasimama juu ya nchi.

2619:26 Hes 12:8; 1Yn 3:2Nami baada ya ngozi yangu kuharibiwa,

bado nikiwa na mwili huu nitamwona Mungu;

2719:27 Lk 2:30; Za 42:1; 63:1; 54:2mimi nitamwona kwa macho yangu mwenyewe:

mimi, wala si mwingine.

Tazama jinsi moyo wangu unavyomtamani sana!

28“Kama mkisema, ‘Tazama tutakavyomwinda,

maadamu mzizi wa tatizo uko ndani yake,’

2919:29 Ay 15:22; Za 58:11; Mhu 12:14ninyi wenyewe uogopeni upanga,

kwa kuwa ghadhabu italeta adhabu kwa upanga,

nanyi ndipo mtakapojua kwamba kuna hukumu.”