Ayubu 18 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Ayubu 18:1-21

Bildadi Anasema: Mungu Huwaadhibu Waovu

118:1 Ay 8:1Bildadi Mshuhi akajibu:

218:2 Ay 8:2; 16:3“Je, ni lini utafika mwisho wa maneno haya?

Uwe mwenye busara, nasi ndipo tutakapoweza kuongea.

318:3 Za 73:22; Ay 12:7Kwa nini sisi tunafikiriwa kama wanyama,

na kuonekana wajinga machoni pako?

418:4 Ay 13:14; 16:9; 14:18Wewe unayejirarua mwenyewe vipande vipande

katika hasira yako,

je, dunia iachwe kwa ajili yako wewe?

Au ni lazima miamba iondolewe mahali pake?

518:5 Yer 25:10; Yn 8:12; Mit 13:9“Taa ya mwovu imezimwa,

nao mwali wa moto wake umezimika.

618:6 Ay 8:22; 5:14; 11:17; 12:25Mwanga hemani mwake umekuwa giza;

taa iliyo karibu naye imezimika.

718:7 Za 18:36; Mit 4:12; Ay 5:13; 15:6Nguvu za hatua zake zimedhoofishwa;

shauri lake baya litamwangusha.

818:8 Mik 7:2; Hab 1:15Miguu yake imemsukumia kwenye wavu,

naye anatangatanga kwenye matundu ya wavu.

918:9 Ay 22:10; 30:12; Isa 24:18; Yer 48:44; Amo 5:14; Mit 7:22Tanzi litamkamata kwenye kisigino;

mtego utamshikilia kwa nguvu.

1018:10 Mit 7:22; Isa 51:20; 1Sam 28:9; Za 140:5Kitanzi kimefichwa ardhini kwa ajili yake;

mtego uko kwenye njia yake.

1118:11 Ay 15:21; 20:8; Za 31:13; Isa 22:18; Yer 6:25Vitisho vimemtia hofu kila upande,

na adui zake humwandama kila hatua.

1218:12 Isa 9:20; 65:13; 8:21; Ay 21:17; 31:3; 15:25Janga linamwonea shauku;

maafa yako tayari kwa ajili yake aangukapo.

1318:13 Zek 14:12; Hes 12:12Nayo yatakula sehemu ya ngozi yake;

mzaliwa wa kwanza wa mauti atakula maungo yake.

1418:14 Ay 8:22; 15:24; 18:11Atangʼolewa kutoka usalama wa hema lake,

na kupelekwa kwa mfalme wa vitisho.

1518:15 Mwa 19:24; Za 11:6; Ay 18:18; 20:26Moto utakaa katika hema lake;

moto wa kiberiti utamwagwa juu ya makao yake.

1618:16 Hos 5:12; Amo 2:9; Mwa 27:28Mizizi yake chini itakauka

na matawi yake juu yatanyauka.

1718:17 Mit 2:22; 10:7; Isa 49:15; Kum 32:26; 9:14; Za 9:5; 69:28Kumbukumbu lake litatoweka katika dunia,

wala hatakuwa na jina katika nchi.

1818:18 Ay 5:14; 18:11; 11:20; 30:8Ameondolewa nuruni na kusukumiwa gizani,

naye amefukuzwa mbali atoke duniani.

1918:19 Za 37:28; 21:10; Isa 14:22; Ay 27:14-15Hana mtoto wala mzao miongoni mwa watu wake,

wala aliyenusurika mahali alipoishi.

2018:20 Yer 46:21; Eze 7:7Watu wa magharibi watashangaa yaliyompata;

watu wa mashariki watapatwa na hofu.

2118:21 Ay 21:28; Yer 9:3; 1The 4:5Hakika ndivyo yalivyo makao ya mtu mwovu;

ndivyo palivyo mahali pake mtu asiyemjua Mungu.”