Ayubu 17 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Ayubu 17:1-16

117:1 Za 88:3-4; Mhu 12:1-7Moyo wangu umevunjika,

siku zangu zimefupishwa,

kaburi linaningojea.

217:2 1Sam 1:6-7; Ay 11:3Hakika wenye mizaha wamenizunguka;

macho yangu yamebaki kutazama uadui wao.

Ayubu Anaomba Msaada

317:3 Za 35:27; 40:17; Mit 6:1; Isa 38:14“Ee Mungu, nipe dhamana unayodai.

Ni nani mwingine atakayeweka dhamana kwa ajili yangu?

417:4 Ay 12:12Umezifunga akili zao zisipate ufahamu,

kwa hiyo hutawaacha wapate ushindi.

517:5 Kut 22:15; Ay 11:20Kama mtu akiwashutumu rafiki zake ili apate ujira,

macho ya watoto wake yatashindwa kuona.

617:6 1Fal 9:7; Yer 15:4“Mungu amenifanya kitu cha dhihaka kwa kila mtu,

mtu ambaye watu humtemea mate usoni.

717:7 Ay 16:8; 2:12; 16:16Macho yangu yamefifia kwa ajili ya majonzi;

umbile langu lote ni kama kivuli.

817:8 Kut 4:14; Ay 22:19Watu wanyofu wanatishwa na hili;

watu wasio na hatia wanasimama dhidi ya wasiomcha Mungu.

917:9 Mit 4:18; 2Sam 22:21; Ay 22:30Hata hivyo, waadilifu watazishika njia zao,

nao wale wenye mikono safi wataendelea kupata nguvu.

1017:10 Ay 12:3“Lakini ninyi njooni, ninyi nyote, jaribuni tena!

Sitampata mtu mwenye hekima miongoni mwenu.

1117:11 Ay 17:15; Isa 38:10; Ay 7:6Siku zangu zimepita, mipango yangu imevunjika,

vivyo hivyo shauku za moyo wangu.

1217:12 Isa 50:11; Ay 5:17-26; 11:17Watu hawa hufanya usiku kuwa mchana,

kwenye giza wao husema, ‘Mwanga u karibu.’

1317:13 2Sam 14:14; Ay 3:13; Za 139:8; 88:18Kama nyumba pekee ninayoitarajia ni kaburi,17:13 Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol.

kama nikikitandika kitanda changu gizani,

1417:14 Ay 13:28; 30:28, 30; 4:19; 7:5; Za 16:10; 49:9; 17:15; Ay 7:6; Za 31:23; Mao 3:18; Eze 37:11kama nikiuambia uharibifu, ‘Wewe u baba yangu,’

na kuliambia buu, ‘Wewe u mama yangu’ au ‘Dada yangu,’

15liko wapi basi tarajio langu?

Ni nani awezaye kuona tarajio lolote kwa ajili yangu?

1617:16 Mwa 2:7; Yon 2:6; Ay 3:17Je, litashuka chini hadi kwenye malango ya mauti?17:16 Malango ya mauti hapa ina maana ya Kuzimu.

Je, tutashuka pamoja mavumbini?”