Ayubu 15 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version

Ayubu 15:1-35

Elifazi Anaongea: Ayubu Anadhoofisha Imani

115:1 Ay 4:1Kisha Elifazi Mtemani akajibu:

215:2 Mwa 41:6; Ay 6:26“Je, mtu mwenye hekima hujibu kwa mawazo matupu,

au kujaza tumbo lake kwa upepo wenye joto wa mashariki?

315:3 Neh 4:2-3; Ay 6:26Je, aweza kubishana juu ya maneno yasiyofaa,

kwa hotuba zisizo na maana?

415:4 Ay 25:6Lakini unadhoofisha hata uchaji wa Mungu

na kuzuia ibada mbele za Mungu.

515:5 Ay 11:6; 22:5; 5:13; Mt 16:23Dhambi yako inasukuma kinywa chako,

nawe umechagua ulimi wa hila.

615:6 Za 10:2; Mt 12:37; Lk 19:22; Ay 7:15; 18:7Kinywa chako mwenyewe kinakuhukumu, wala si changu;

midomo yako mwenyewe inashuhudia dhidi yako.

715:7 Ay 38:21; 1Sam 2:8; Mit 8:25; Za 90:2“Je, wewe ni mtu wa kwanza kuzaliwa?

Ulizaliwa kabla ya vilima?

815:8 Yer 23:18; 1Kor 2:11Je, wewe husikiliza mashauri ya siri ya Mungu?

Je, wewe unaizuia hekima iwe yako mwenyewe?

915:9 Ay 12:3Wewe unajua kitu gani tusichokijua sisi?

Unafahamu kitu gani tusichokifahamu sisi?

1015:10 Ay 12:12; 32:6-7; 8:8-10Wale wenye mvi na wazee wako upande wetu,

watu ambao ni wazee hata kuliko baba yako.

1115:11 Mwa 37:35; 2Kor 1:3-4; Kum 8:3; Yer 15:16Je, faraja za Mungu hazikutoshi,

au maneno yaliyosemwa kwako kwa upole si kitu?

1215:12 Ay 11:13; 36:13Kwa nini moyo wako unakudanganya,

na kwa nini macho yako yanangʼaa,

1315:13 Mit 29:11; Dan 11:30; Za 94:4; Ay 11:8; 22:5; 30:2ili kwamba upate kutoa hasira yako dhidi ya Mungu,

na kumwaga maneno kama hayo kutoka kinywani mwako?

1415:14 Ay 14:1; 4:17; 2Nya 6:36; Mhu 7:18, 20“Mwanadamu ni kitu gani, hata aweze kuwa safi,

au yeye aliyezaliwa na mwanamke, hata aweze kuwa mwadilifu?

1515:15 Ay 5:1; 4:18Kama Mungu hawaamini watakatifu wake,

kama hata mbingu zenyewe si safi machoni pake,

1615:16 Law 5:2; Ay 12:4; 20:12; Mit 19:28; Za 14:1sembuse mwanadamu ambaye ni mwovu na mpotovu,

ambaye hunywa uovu kama anywavyo maji!

1715:17 Ay 4:8“Nisikilize mimi nami nitakueleza,

acha nikuambie yale niliyoyaona,

1815:18 Kum 32:7; Ay 8:8; Mwa 18:19ambayo watu wenye hekima wameyanena,

bila kuficha lolote walilopokea toka kwa baba zao

1915:19 Mwa 12:1; Ay 22:8(wakati ambao wao peke yao ndio walipewa nchi,

hakuna mgeni aliyepita miongoni mwao):

2015:20 Oba 1:15; Sef 1:17Mtu mwovu siku zake zote hupata mateso,

miaka yote aliwekewa mkorofi.

2115:21 1Sam 3:11; Yer 6:25; Isa 13:3; 1The 5:3Sauti za kutisha hujaa masikioni mwake;

katika kufanikiwa kwake, wanyangʼanyi humshambulia.

2215:22 Hos 9:13; Amo 5:19Hukata tamaa kuokoka gizani;

amewekwa kwa ajili ya upanga.

2315:23 Za 59:15; 109:10; Ay 18:12Hutangatanga, akitafuta chakula;

anajua kwamba siku ya giza iko karibu.

2415:24 Isa 8:22; 9:1; Ay 15:20; 18:14Taabu na maumivu makuu vinamtia hofu;

humshinda kama mfalme aliye tayari kwa vita,

2515:25 Za 2:2-3; Mit 21:30kwa sababu amemkunjia Mungu ngumi yake

na kujigamba dhidi ya Mwenyezi,

2615:26 Yer 44:16kwa kiburi akishambulia dhidi ya Mungu

akiwa na ngao nene, iliyo imara.

2715:27 Amu 3:17; Za 17:10“Ingawa uso wake umefunikwa na mafuta kwa unene

na kiuno chake kimevimba kwa kunenepa,

2815:28 Isa 5:9; Ay 3:14ataishi katika miji ya magofu,

na katika nyumba ambazo haziishi mwanadamu yeyote,

nyumba zinazokuwa vifusi.

2915:29 Ay 3:15; 7:8; Isa 5:8Hatatajirika tena, nao utajiri wake hautadumu,

wala mali zake hazitakuwa nyingi juu ya nchi.

3015:30 Ay 4:9, 15; 16:7; 20:26; Kut 15:10Hatatoka gizani;

mwali wa moto utanyausha machipukizi yake,

nayo pumzi ya kinywa cha Mungu itamwondolea mbali.

3115:31 Yer 7:4-8; Mt 6:19; Za 62:1015:31 Ay 31:5; Mit 1:16; 6:18; Isa 44:20; 59:7; Mik 2:11; Mk 13:5Asijidanganye mwenyewe kutumainia ubatili,

kwa kuwa hatapata malipo yoyote.

3215:32 Mhu 7:17; Za 109:8; Mit 10:27; Ay 18:16Atakuwa amelipwa kikamilifu kabla ya wakati wake,

nayo matawi yake hayatastawi.

3315:33 Hab 3:17Atafanana na mzabibu uliopukutishwa matunda yake kabla hayajaiva,

kama mzeituni unaodondosha maua yake.

3415:34 Kut 23:8; Ay 8:22; Isa 33:14Kwa kuwa jamii ya wasiomcha Mungu watakuwa tasa,

nao moto utateketeza hema za wale wanaopenda rushwa.

3515:35 Hos 10:13; Gal 6:7; Za 7:14Hutunga mimba ya madhara na kuzaa uovu;

matumbo yao huumba udanganyifu.”

Chinese Contemporary Bible 2023 (Traditional)

約伯記 15:1-35

以利法再次發言

1提幔以利法回答說:

2「智者豈會用空談作答,

滿腹東風?

3申辯時豈會講無用的話,

說無益之言?

4你摒棄對上帝的敬畏,

拒絕向祂默禱。

5你的罪指示你開口,

使你說出詭詐之言。

6並非我定你的罪,

定你罪的是你的口,

指控你的是你的嘴唇。

7你豈是第一個出生的人?

你豈在群山之前被造?

8你豈聽過上帝的密旨?

你豈獨攬智慧?

9有何事你知而我們不知,

你懂而我們不懂?

10我們這裡有白髮老人,

比你父親還年長。

11上帝用溫柔的話安慰你,

難道你還嫌不夠嗎?

12你為何失去理智,

為何雙眼冒火,

13以致你向上帝發怒,

口出惡言?

14人算什麼,怎能純潔?

婦人所生的算什麼,怎能公義?

15連上帝的聖者都無法令祂信任,

連諸天在祂的眼中都不潔淨,

16更何況可憎敗壞、

嗜惡如喝水的世人?

17「讓我告訴你,你好好聽著。

我要把所見的陳明,

18那是智者的教導,

是他們未曾隱瞞的祖訓。

19這片土地只賜給了他們,

沒有外人在他們中間出入。

20惡人一生受折磨,

殘暴之徒終身受苦。

21他耳邊響著恐怖的聲音,

他安逸時遭強盜襲擊。

22他不指望能逃脫黑暗,

他註定要喪身刀下。

23他到處流浪,尋找食物,

他知道黑暗之日快要來臨。

24患難和痛苦使他害怕,

像預備上陣的君王一樣壓制他。

25因為他揮拳對抗上帝,

藐視全能者,

26手拿堅盾狂妄地衝撞祂。

27他滿臉肥肉,

腰間堆滿脂肪。

28他活在毀滅的城邑,

住在被人廢棄、

行將坍塌的房屋。

29他不再富足,

家財不能久留,

地產無法加增。

30他無法逃脫黑暗,

火焰要燒焦他的嫩枝,

上帝口中的氣要毀滅他。

31他不可自欺,信靠虛空,

因為虛空必成為他的回報。

32在他離世以前,虛空必臨到他,

他的枝子再不會青綠。

33他必像一棵葡萄樹,

葡萄未熟已掉落;

又像一棵橄欖樹,

花剛開便凋零。

34不信上帝之輩必不生育,

受賄者的帳篷必被火燒。

35他們心懷不軌,生出罪惡,

他們滿腹詭詐。」