Ayubu 13 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Ayubu 13:1-28

113:1 Ay 9:24“Macho yangu yameona hili lote,

masikio yangu yamesikia na kulielewa.

213:2 Ay 12:3Hayo mnayoyajua mimi pia ninayajua;

mimi si mtu duni kuliko ninyi.

313:3 Ay 5:8; 23:3-4; 5:17; 40:2Lakini ninayo shauku ya kuzungumza na Mwenyezi

na kuhojiana shauri langu na Mungu.

413:4 Isa 9:15; Yer 23:32; Za 119:69; Yer 8:22; Ay 6:15Ninyi, hata hivyo, hunipakaza uongo;

ninyi ni matabibu wasiofaa kitu, ninyi nyote!

513:5 Mit 17:28; Amo 5:13; Ay 13:13; Amu 18:19; Mhu 5:3; Yak 1:19Laiti wote mngenyamaza kimya!

Kwa kuwa kwenu hilo lingekuwa hekima.

613:6 Ay 33:1; 36:4Sikieni sasa hoja yangu;

sikilizeni kusihi kwangu.

713:7 Ay 16:17; 36:4; 17:5; Rum 3:5-8Je, mtazungumza kwa uovu kwa niaba ya Mungu?

Je, mtazungumza kwa udanganyifu kwa niaba yake?

813:8 Law 19:15; Mit 24:23Mtamwonyesha upendeleo?

Mtamtetea Mungu kwenye mashtaka yake?

913:9 Ay 12:16; 9:3; Gal 6:7Je, ingekuwa vyema Mungu akiwahoji ninyi?

Je, mngeweza kumdanganya kama ambavyo mngeweza kuwadanganya wanadamu?

1013:10 Law 19:15; 2Nya 19:7Hakika angewakemea

kama mkiwapendelea watu kwa siri.

1113:11 Ay 31:23; Kut 3:6Je, huo ukuu wake haungewatisha ninyi?

Je, hofu yake isingewaangukia ninyi?

1213:12 Neh 4:2-3Maneno yenu ni mithali za majivu;

utetezi wenu ni ngome za udongo wa mfinyanzi.

1313:13 Ay 13:5; 7:11; 9:21“Nyamazeni kimya nipate kusema;

kisha na yanipate yatakayonipata.

1413:14 Amu 9:17; Za 119:109Kwa nini nijiweke mwenyewe kwenye hatari

na kuyaweka maisha yangu mikononi mwangu?

1513:15 Za 27:1; Dan 3:28; Ay 5:8; 27:5; Mit 14:32; Rum 8:38-39Ingawa ataniua, bado nitamtumaini;

hakika nitazitetea njia zangu mbele zake.

1613:16 Hos 14:4; Flp 1:19; Isa 12:1-2Naam, hili litanigeukia kuwa wokovu wangu,

kwa maana hakuna mtu asiyemcha Mungu

atakayethubutu kuja mbele yake!

1713:17 Ay 21:2Sikilizeni maneno yangu kwa makini;

nayo masikio yenu yaingize kile nisemacho.

1813:18 Ay 13:3; 23:4; 37:19; 2:3; 9:21Sasa kwamba nimekwisha kutayarisha mambo yangu,

ninajua mimi nitahesabiwa kuwa na haki.

1913:19 Isa 50:8; Rum 8:33; Ay 3:13; 40:4; 9:15Je, kuna yeyote anayeweza kuleta mashtaka dhidi yangu?

Kama ndivyo, nitanyamaza kimya na nife.

20“Ee Mungu, unijalie tu mimi haya mambo mawili,

nami sitajificha uso wako:

2113:21 Za 39:10; Ebr 10:31; Kut 9:3; Ay 6:4Ondoa mkono wako uwe mbali nami,

nawe uache kuniogofya kwa hofu zako kuu.

2213:22 Ay 9:35; 14:15Niite kwenye shauri nami nitajibu,

au niache niseme, nawe upate kujibu.

2313:23 1Sam 26:18; Ay 7:21; 9:21; 14:17; 33:9Ni makosa na dhambi ngapi nilizotenda?

Nionyeshe kosa langu na dhambi yangu.

2413:24 Isa 8:17; Za 88:14-15; Yer 30:14Kwa nini kuuficha uso wako

na kunihesabu mimi kuwa adui yako?

2513:25 Law 26:36; Isa 43:17; Hos 13:3Je, utaliadhibu jani lipeperushwalo na upepo?

Je, utayasaka makapi makavu?

2613:26 Ay 21:23; Za 25:7Kwa kuwa unaandika mambo machungu dhidi yangu

na kunifanya nizirithi dhambi za ujana wangu.

2713:27 Mwa 40:15; Mdo 16:24Umeifunga miguu yangu kwenye pingu.

Unazichunga kwa makini njia zangu zote

kwa kutia alama kwenye nyayo za miguu yangu.

2813:28 Hos 5:12; Yak 5:2“Hivyo mwanadamu huangamia kama kitu kilichooza,

kama vazi lililoliwa na nondo.