Ayubu 12 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Ayubu 12:1-25

Hotuba Ya Nne Ya Ayubu

Ayubu Anajibu: Mimi Ni Mtu Wa Kuchekwa

1Ndipo Ayubu akajibu:

212:2 Ay 15:8; 17:10“Bila shaka ninyi ndio watu,

nayo hekima itakoma mtakapokufa!

312:3 Ay 13:2; 15:9Lakini mimi ninao ufahamu kama ninyi;

mimi si duni kwenu.

Ni nani asiyejua mambo haya yote?

412:4 Mwa 6:9; 38:23; Ay 21:3; 15:16; Za 91:15“Nimekuwa mtu wa kuchekwa na rafiki zangu,

ingawa nilimwita Mungu naye akanijibu:

mimi ni mtu wa kuchekwa tu,

ingawa ni mwadilifu na nisiye na hatia!

512:5 Za 123:4; 17:5; 37:31; 38:16; 66:9; 73:2; 94:18; Mit 14:2Wanadamu wakiwa katika utulivu huwa na dharau kwa wale wenye msiba

kana kwamba ndiyo haki ya wale ambao miguu yao inateleza.

612:6 Ay 5:24; 22:18; 9:24Hema za wanyangʼanyi hazisumbuliwi,

wale wanaomghadhibisha Mungu wako salama:

wale wamchukuao mungu wao mikononi mwao.

712:7 Ay 35:11; 18:3; Mt 6:26; Rum 1:20“Lakini ulizeni wanyama, nao watawafundisha,

au ndege wa angani, nao watawaambia;

8au zungumzeni na dunia, nayo itawafundisha,

au acheni samaki wa baharini wawape taarifa.

912:9 Isa 41:20; 1:3; Ay 9:24Ni nani miongoni mwa hawa wote asiyejua

kwamba mkono wa Bwana ndio uliofanya hili?

1012:10 Hes 16:22; Mdo 17:28; Dan 5:23Mkononi mwake kuna uhai wa kila kiumbe,

na pumzi ya wanadamu wote.

1112:11 Ay 34:3Je, sikio haliyajaribu maneno

kama vile ulimi uonjavyo chakula?

1212:12 1Fal 4:2; Ay 15:10; 17:4; 32:7, 9; 34:4, 10Je, hekima haipatikani katikati ya wazee?

Je, maisha marefu hayaleti ufahamu?

1312:13 Mit 21:30; Isa 45:9; Yer 32:19; 1Kor 1:24; Dan 1:17“Hekima na nguvu ni vya Mungu;

shauri na ufahamu ni vyake yeye.

1412:14 Ay 16:9; 9:3; Kum 13:16; Eze 26:14; Ufu 3:7; Za 127:1; Isa 24:20; 25:2Kile anachokibomoa hakiwezi kujengeka tena;

mtu aliyefungiwa naye hawezi kufunguliwa.

1512:15 1Fal 8:35; Isa 40:12; Kum 28:22; Mwa 7:11, 14Akizuia maji, huwa pana ukame;

akiyaachia maji, huharibu nchi.

1612:16 2Nya 18:22; Rum 2:11; Ay 9:4; 13:7, 9; 27:4Kwake kuna nguvu na ushindi;

adanganywaye na adanganyaye, wote wawili ni wake.

1712:17 Ay 12:19; 19:9; Isa 20:4; Ay 3:14; 1Kor 1:20Yeye huwaondoa washauri wakiwa wametekwa nyara,

naye huwapumbaza wanaotoa maamuzi.

1812:18 Za 107:14; 116:16; Nah 1:13; Ay 12:21; 34:18Huondoa pingu zilizofungwa na wafalme,

na kuwafunga mishipi ya kiunoni.

1912:19 Dan 2:21, 34; Kum 24:15; Ay 9:24; 14:20; 22:8; 24:12, 22; 12:17; Isa 2:22Huwaondoa makuhani wakiwa wametekwa nyara,

na kuwaangusha waliojiimarisha muda mrefu.

2012:20 Yer 32:9; Kum 4:33-34; Ay 12:12, 24; Dan 4:33-34Hunyamazisha midomo ya washauri wanaoaminika,

na kuondoa busara ya wazee.

2112:21 Ay 12:18; 3:15; Isa 34:12Huwamwagia dharau wanaoheshimika,

na kuwavua silaha wenye nguvu.

2212:22 1Kor 4:5; Ay 3:5; Za 139:12; Dan 2:22Hufunua mambo ya ndani ya gizani,

na kuyaleta nuruni yale yaliyositirika sana.

2312:23 Isa 13:4; 54:3; Kut 34:24; Mt 10:26Huyafanya mataifa yatukuke na kuyaangamiza;

hufanya mataifa kuwa makubwa, naye huyatawanya.

24Huwaondolea viongozi wa nchi akili zao;

huwapeleka watangetange nyikani pasipo na njia.

2512:25 Kum 28:29; Ay 5:14; Za 107:27; Isa 24:20Hupapasa gizani pasipokuwa na mwanga;

huwafanya wapepesuke kama walevi.