Ayubu 11 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Ayubu 11:1-20

Sofari Anasema: Hatia Ya Ayubu Inastahili Adhabu

111:1 Ay 2:11Ndipo Sofari Mnaamathi akajibu:

211:2 Ay 8:2; 16:3; Mwa 41:6“Je, maneno haya yote yapite bila kujibiwa?

Je, huyu mnenaji athibitishwe kuwa na haki?

311:3 Efe 4:29; 5:4; Ay 12:4; 16:10; 17:2; 21:3Je, maneno yako ya upuzi yawafanye watu wanyamaze kimya?

Je, mtu asikukemee unapofanya dhihaka?

411:4 Ay 6:10; 9:21; 10:7; 1Pet 3:15Unamwambia Mungu, ‘Imani yangu ni kamili

nami ni safi mbele zako.’

5Aha! Laiti kwamba Mungu angesema,

kwamba angefungua midomo yake dhidi yako,

611:6 Ay 9:4; 1Kor 2:10; Mao 3:22; Ezr 9:13naye akufunulie siri za hekima,

kwa kuwa hekima ya kweli ina pande mbili.

Ujue hili: Mungu amesahau hata baadhi ya dhambi zako.

711:7 Mhu 3:11; Rum 11:33; Isa 40:28; Ay 5:9; Mt 11:27; Efe 3:8“Je, waweza kujua siri za Mungu?

Je, waweza kuyachunguza mambo yote kumhusu Mwenyezi?

811:8 Za 57:10; Isa 55:9; Efe 3:18; Mwa 15:5; Ay 22:12; 25:2; Za 57:10; 139:8; Isa 55:9; Ay 7:9; 15:13, 25; 33:13; 40:2Ni juu mno kuliko mbingu: waweza kufanya nini?

Kina chake ni kirefu kuliko kuzimu:

wewe waweza kujua nini?

911:9 Efe 3:19-20; Ay 22:12; 35:5; 36:26; 37:5, 23; Isa 40:26Kipimo chake ni kirefu kuliko dunia,

nacho ni kipana kuliko bahari.

1011:10 Ay 9:12; Ufu 3:7“Kama akija na kukufunga gerezani,

na kuitisha mahakama, ni nani awezaye kumpinga?

1111:11 Ay 10:4; 31:37; 34:11, 25; 36:7; Za 10:14Hakika anawatambua watu wadanganyifu;

naye aonapo uovu, je, haangalii?

1211:12 Mwa 12:16; 2Nya 6:36Mpumbavu aweza kuwa mwenye hekima,

endapo mtoto wa punda-mwitu atazaliwa mwanadamu.

1311:13 1Sam 7:3; Za 78:8; 88:9; Kut 9:29; Ay 5:8, 27“Hata sasa ukiutoa moyo wako kwake

na kumwinulia mikono yako,

1411:14 Yos 24:14; Za 101:4; 22:23ukiiondolea mbali ile dhambi iliyo mkononi mwako

wala usiuruhusu uovu ukae hemani mwako,

1511:15 Ay 22:26; 1Yn 3:21; 1Tim 2:8; 1Sam 2:9; Za 20:8; 37:23; 40:2; Efe 6:14; Mwa 4:7ndipo utainua uso wako bila aibu;

utasimama imara bila hofu.

1611:16 Isa 26:16; 37:3; 65:16; Eze 21:7; Yos 7:5; Za 58:7; 112:10; Ay 22:11Hakika utaisahau taabu yako,

utaikumbuka tu kama maji yaliyokwisha kupita.

1711:17 Ay 22:28; Za 37:6; Isa 58:8, 10; 62:1; Ay 17:12; Za 18:28Maisha yako yatangʼaa kuliko adhuhuri,

nalo giza litakuwa kama alfajiri.

1811:18 Mhu 5:12; Isa 11:10; Zek 3:10; Za 127:2Utakuwa salama, kwa kuwa lipo tumaini;

utatazama pande zote na kupumzika kwa salama.

1911:19 Law 26:6; Isa 45:14Utalala, wala hakuna atakayekuogofya,

naam, wengi watajipendekeza kwako.

2011:20 Kum 28:65; Yer 11:11; Amo 2:14; Ay 8:13; 17:5Bali macho ya waovu hayataona,

wokovu utawaepuka;

tarajio lao litakuwa ni hangaiko

la mtu anayekata roho.”