Ayubu 10 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Ayubu 10:1-22

Ayubu: Nayachukia Maisha Yangu

110:1 Hes 11:15; 1Sam 1:10; Ay 7:11; 9:18, 21; 1Fal 19:4“Nayachukia sana haya maisha yangu;

kwa hiyo nitatoa malalamiko yangu kwa wazi bila kujizuia,

nami nitanena kutokana na uchungu wa moyo wangu.

210:2 Ay 13:3; 40:1; Isa 3:13; Hos 4:1; 5:1; Mik 6:2; Rum 8:33Nitamwambia Mungu: Usinihukumu,

bali niambie una mashtaka gani dhidi yangu.

310:3 Ay 9:24; 22:18; 31:23; Mwa 1:26; Za 138:8; Isa 60:21; 64:8; Za 8:6; 95:6; 100:3Je, inakupendeza wewe kunionea,

kuikataa kwa dharau kazi ya mikono yako,

huku wewe ukitabasamu juu ya mipango ya waovu?

410:4 Mit 5:21; Yer 16:17; 1Sam 16:7; Ay 11:11; 14:16; Za 11:4; 33:15; Mit 15:3; Yer 11:20-23Je, wewe una macho ya kimwili?

Je, wewe huona kama mwanadamu aonavyo?

510:5 Za 102:24; 2Pet 3:8; Ay 36:26; Za 39:5; 90:2, 4Je, siku zako ni kama zile za mwanadamu,

au miaka yako ni kama ile ya mtu,

610:6 Ay 14:16ili kwamba utafute makosa yangu

na kuichunguza dhambi yangu;

710:7 Ay 10:15; 6:29; 11:4; 16:17; Kum 32:39ingawa wajua kuwa mimi sina hatia,

na hakuna awezaye kunitoa mkononi mwako?

810:8 Za 119:73; Isa 43:7; Mwa 2:7; 2Sam 14:14; Ay 30:15“Mikono yako ndiyo iliyoniumba na kunifanya.

Je, sasa utageuka na kuniangamiza?

910:9 Isa 29:16; 64:8; Mwa 2:7; Ay 7:21; 4:19Kumbuka kuwa ulinifinyanga kama udongo wa mfinyanzi.

Je, sasa utanifanya kuwa mavumbi tena?

10Je, wewe hukunimimina mimi kama maziwa,

na kunigandisha kama jibini,

1110:11 Za 139:13, 15ukanivika ngozi na nyama,

na kuniunga pamoja kwa mifupa na mishipa?

1210:12 Mwa 2:7; 24:12; 45:5; 1Pet 2:25Umenipa uhai na kunitendea wema,

katika uangalizi wako umeilinda roho yangu.

1310:13 Ay 23:13; Za 115:3“Lakini hili ndilo ulilolificha moyoni mwako,

nami ninajua kuwa hili lilikuwa katika nia yako:

1410:14 Kut 34:7; Ay 7:21; 13:27Kama nilifanya dhambi, ungekuwa umeniona,

wala usingeacha kosa langu lipite bila kuadhibiwa.

1510:15 Ay 9:13; 10:7; Isa 3:11; Za 25:18; 25:16Kama nina hatia, ole wangu!

Hata kama ningekuwa sina hatia,

siwezi kukiinua kichwa changu,

kwa kuwa nimejawa na aibu,

na kuzama katika mateso yangu.

1610:16 Yer 5:6; Hos 5:14; 1Sam 28:21; Isa 38:16; Za 7:2; 1Sam 17:38; Mao 3:10Kama nikiinua kichwa changu juu, unaninyatia kama simba,

na kuonyesha tena uwezo wa kutisha dhidi yangu.

1710:17 1Fal 21:10; Ay 16:8; Rut 1:21Wewe waleta mashahidi wapya dhidi yangu

na kuzidisha hasira yako juu yangu;

nazo nguvu zako zinanijia wimbi moja baada ya jingine.

1810:18 Ay 3:8; 3:26; Za 22:9; Mhu 4:2; 7:1“Kwa nini basi ulinitoa tumboni?

Ninatamani ningekufa kabla jicho lolote halijaniona.

1910:19 Ay 3:3; Yer 15:10Laiti nisingekuwako kamwe,

au ningekuwa nimechukuliwa moja kwa moja

kutoka tumboni kwenda kaburini!

2010:20 Mhu 6:12; Ay 7:16-19; 5:7; Za 39:13; Ay 9:25Je, siku zangu chache si zimekaribia kuisha?

Niachie ili niweze kupata muda mfupi wa kufurahi

2110:21 2Sam 12:23; Za 88:12; 23:4; Ay 3:13; Mhu 2:9kabla sijaenda mahali ambapo hakuna kurudi tena,

katika nchi ya giza na uvuli wa mauti,

2210:22 Ay 3:5; 1Sam 2:9nchi ya giza kuu sana,

yenye uvuli wa giza na machafuko,

mahali ambapo hata nuru ni giza.”