Amosi 9 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Amosi 9:1-15

Israeli Kuangamizwa

19:1 Za 68:21; Yer 11:11Nilimwona Bwana akiwa amesimama kando ya madhabahu, naye akasema:

“Piga vichwa vya nguzo

ili vizingiti vitikisike.

Viangushe juu ya vichwa vya watu wote;

na wale watakaosalia nitawaua kwa upanga.

Hakuna awaye yote atakayekimbia,

hakuna atakayetoroka.

29:2 Za 139:8-10; Ay 20:6; 7:9; Yer 51:33; Oba 1:4; Eze 26:20Wajapojichimbia chini mpaka kwenye vina vya kuzimu,

kutoka huko mkono wangu utawatoa.

Wajapopanda juu hadi kwenye mbingu,

kutoka huko nitawashusha.

39:3 Yer 23:24; 6:16-17; Za 139:8-10; 68:22; Mwa 49:17; Ay 11:20Wajapojificha juu ya kilele cha Karmeli,

huko nitawawinda na kuwakamata.

Wajapojificha kutoka kwenye uso wangu

katika vilindi vya bahari,

huko nako nitaamuru joka kuwauma.

49:4 Law 26:33; 17:10; Eze 5:12; 15:7; Kum 28:65; Yer 39:16; 21:10; 44:11Wajapopelekwa uhamishoni na adui zao,

huko nako nitaamuru upanga uwaue.

Nitawakazia macho yangu kwa mabaya

wala si kwa mazuri.”

59:5 Za 46:2; Amo 8:8; Mik 1:4Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote,

yeye agusaye dunia nayo ikayeyuka,

na wote wakaao ndani mwake wakaomboleza:

nayo nchi yote huinuka kama Naili,

kisha hushuka kama mto wa Misri;

69:6 Za 104:1-3, 5-13; Amo 5:8; Yer 43:9yeye ambaye hujenga jumba lake la kifalme katika mbingu

na kuisimika misingi yake juu ya dunia,

yeye aitaye maji ya bahari

na kuyamwaga juu ya uso wa nchi:

Bwana ndilo jina lake.

79:7 2Nya 12:3; Kum 2:23; Isa 43:3; 22:6; 2Fal 16:9; Yer 47:4; Amo 1:5; Mwa 10:14“Je, Waisraeli,

ninyi si sawa kwangu kama Wakushi?”

asema Bwana.

“Je, sikuleta Israeli kutoka Misri,

Wafilisti kutoka Kaftori,9:7 Yaani Krete.

na Washamu kutoka Kiri?

89:8 Yer 30:11; 44:27; Za 11:4“Hakika macho ya Bwana Mwenyezi

yako juu ya ufalme wenye dhambi.

Nami nitauangamiza

kutoka kwenye uso wa dunia:

hata hivyo sitaiangamiza kabisa

nyumba ya Yakobo,”

asema Bwana.

99:9 Lk 22:31; Isa 30:28; Yer 31:36; Dan 9:7“Kwa kuwa nitatoa amri,

na nitaipepeta nyumba ya Israeli

miongoni mwa mataifa yote,

kama vile nafaka ipepetwavyo katika ungo,

na hakuna hata punje moja itakayoanguka chini.

109:10 Yer 5:12; 23:17; 49:37; Eze 20:38; Amo 6:3Watenda dhambi wote miongoni mwa watu wangu

watauawa kwa upanga,

wale wote wasemao,

‘Maafa hayatatupata wala kutukuta.’

Kurejezwa Kwa Israeli

119:11 Mdo 15:16; Mik 7:8-11; Zek 12:7; Isa 7:2; 49:8; Mwa 26:22; Eze 17:24“Katika siku ile nitaisimamisha

hema ya Daudi iliyoanguka.

Nitakarabati mahali palipobomoka

na kujenga upya magofu yake,

na kuijenga kama ilivyokuwa awali,

129:12 Hes 24:18; Isa 43:7; Oba 1:19; Yer 25:29; Mdo 15:16-17ili wapate kuyamiliki mabaki ya Edomu,

na mataifa yote yale yanayobeba Jina langu,”

asema Bwana ambaye atafanya mambo haya.

139:13 Law 26:5; Amu 9:27; Yoe 3:18; 2:24; Yer 31:38; 33:14; Rut 2:3“Siku zinakuja,” asema Bwana,

“wakati mvunaji atatanguliwa na mkulima,

naye mpanzi atatanguliwa na yeye akamuaye zabibu.

Divai mpya itadondoka kutoka milimani,

na kutiririka kutoka vilima vyote.

149:14 Isa 32:18; 49:8; 62:9; 61:4; Eze 34:13-14; Yer 29:14; 33:7; 30:18Nitawarejesha tena watu wangu Israeli waliohamishwa;

wataijenga tena miji iliyoachwa magofu,

nao wataishi ndani mwake.

Watapanda mizabibu na kunywa divai yake;

watalima bustani na kula matunda yake.

159:15 Kut 15:17; Isa 60:21; 65:9; Yer 18:9; 23:8; 3:18; 24:6; 32:15; Eze 28:26; 34:28; Yoe 3:20Nitaipanda Israeli katika nchi yao wenyewe,

hawatangʼolewa tena

kutoka nchi ambayo nimewapa,”

asema Bwana Mungu wenu.