Amosi 7 – NEN & NVI

Kiswahili Contemporary Version

Amosi 7:1-17

Maono Ya Kwanza: Nzige

17:1 Amo 8:1; Za 78:46; Yer 51:14; Yoe 1:4Hili ndilo alilonionyesha Bwana Mwenyezi katika maono: Alikuwa anaandaa makundi ya nzige baada ya kuvunwa fungu la mfalme na wakati ule tu mimea ya pili ilipokuwa ikichipua. 27:2 Kut 10:15; Eze 11:13; Isa 37:4; Amo 4:9Wakati nzige walikuwa wamekula mimea yote ya nchi, nililia kwa sauti kuu, “Bwana Mwenyezi, samehe! Je, Yakobo atawezaje kuendelea kuishi? Yeye ni mdogo sana!”

37:3 Kut 32:14; Yon 3:10; Kum 32:36; Za 106:45; 1Nya 21:15; Hos 11:8; Yoe 2:14; Yak 5:16; Yer 18:8; 26:19Kwa hiyo Bwana akaghairi.

Kisha Bwana akasema, “Hili halitatokea.”

Maono Ya Pili: Moto

47:4 Isa 66:16; Yoe 1:19; Kum 32:22Hili ndilo Bwana Mwenyezi alilonionyesha katika maono: Bwana Mwenyezi alikuwa akiita hukumu ya moto; nao ulikausha vilindi vikuu, ukateketeza nchi. 57:5 Yoe 2:17Ndipo nikalia, “Bwana Mwenyezi, nakusihi, zuia! Je, Yakobo atawezaje kuendelea kuishi? Yeye ni mdogo sana!”

67:6 Kut 32:14; Yer 18:8; 42:10; Za 102:17; Yon 3:10; Eze 9:8Kwa hiyo Bwana akaghairi.

Bwana Mwenyezi akasema, “Hili nalo halitatokea.”

Maono Ya Tatu: Timazi

7Hili ndilo alilonionyesha katika maono: Bwana alikuwa amesimama karibu na ukuta ambao ulikuwa umejengwa kwa timazi, akiwa na uzi wa timazi mkononi mwake. 87:8 Isa 28:17; Mao 2:8; 2Fal 21:13; Eze 7:2-9; Yer 1:11-13; 15:6; Mik 7:18Naye Bwana akaniuliza, “Je, Amosi unaona nini?”

Nikamjibu, “Uzi wa timazi.”

Kisha Bwana akasema, “Tazama, ninaweka uzi wa timazi miongoni mwa watu wangu Israeli; sitawahurumia tena.

97:9 Law 26:31; Mwa 26:23; 2Fal 14:23; 1Fal 13:34; 2Fal 15:9-10; Isa 63:18; Hos 10:8“Mahali pa Isaki pa juu pa kuabudia miungu pataangamizwa,

na mahali patakatifu pa Israeli pa kuabudia pataharibiwa;

kwa upanga wangu nitainuka

dhidi ya nyumba ya Yeroboamu.”

Amosi Na Amazia

107:10 1Fal 12:32; Yos 7:2; 2Fal 14:23-24; Yer 38:4; 26:8-11Kisha Amazia kuhani wa Betheli akatuma ujumbe kwa Yeroboamu mfalme wa Israeli, akisema: “Amosi analeta fitina juu yako katikati ya Israeli. Nchi haiwezi kuvumilia maneno yake yote. 117:11 Amo 5:27; Yer 36:16Kwa kuwa hili ndilo Amosi analosema:

“ ‘Yeroboamu atakufa kwa upanga,

na kwa hakika Israeli watakwenda uhamishoni,

mbali na nchi yao.’ ”

127:12 Mt 8:34; 1Sam 9:9Kisha Amazia akamwambia Amosi, “Nenda zako, ewe mwonaji! Urudi katika nchi ya Yuda. Ujipatie riziki yako huko na kutoa unabii wako. 137:13 Yer 20:2; 36:5; Amo 2:12; Mdo 4:18; Yos 7:2; 1Fal 12:29Usiendelee kutoa unabii katika Betheli, kwa sababu hapa ni mahali pa mfalme pa kuabudia na Hekalu la ufalme huu.”

147:14 1Sam 10:5; Zek 13:5; 2Fal 2:5; 4:38; Isa 9:10; 1Fal 10:27Amosi akamjibu Amazia, “Mimi sikuwa nabii wala mwana wa nabii, lakini nilikuwa mchungaji wa kondoo na mtunza mikuyu. 157:15 Mwa 37:5; 2Sam 7:8; Yer 7:1-2; 26:12; Eze 2:3-4; Isa 6:9Lakini Bwana akanitoa kutoka kuchunga kondoo na kuniambia, ‘Nenda, ukawatabirie watu wangu Israeli.’ 167:16 Isa 30:10; Eze 20:46; Mik 2:6; Yer 22:2Sasa basi, sikieni neno la Bwana. Ninyi mnasema,

“ ‘Usitabiri dhidi ya Israeli,

na uache kuhubiri dhidi ya nyumba ya Isaki.’

177:17 Hos 4:13; 9:3; Eze 4:13; Yer 28:12; 29:21; Mao 5:11; Amo 5:27; 2:12-13; 2Fal 17:6“Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana:

“ ‘Mke wako atakuwa kahaba mjini,

nao wana wako na binti zako watauawa kwa upanga.

Shamba lako litapimwa na kugawanywa,

na wewe mwenyewe utafia katika nchi ya kipagani.

Nayo Israeli kwa hakika itakwenda uhamishoni,

mbali na nchi yao.’ ”

Nueva Versión Internacional

Amós 7:1-17

Tres visiones

1Esto es lo que el Señor y Dios me mostró: empezaba a crecer la hierba después de la siega que corresponde al rey y vi al Señor preparando enjambres de langostas. 2Cuando las langostas acababan con la hierba de la tierra, exclamé:

—¡Señor mi Dios, te ruego que perdones a Jacob! ¿Cómo va a sobrevivir, si es tan pequeño?

3Entonces el Señor se compadeció y dijo:

—Esto no va a suceder.

4Esto es lo que el Señor y Dios me mostró: Vi al Señor y Dios llamar a juicio con un fuego que devoraba el gran abismo y consumía los campos. 5Y exclamé:

—¡Detente, Señor mi Dios, te lo ruego! ¿Cómo sobrevivirá Jacob, si es tan pequeño?

6Entonces el Señor se compadeció y dijo:

—Esto tampoco va a suceder.

7Esto es lo que me mostró: El Señor estaba de pie junto a un muro construido a plomo y tenía una cuerda de plomada en la mano. 8Y el Señor me preguntó:

—¿Qué ves, Amós?

—Una cuerda de plomada —respondí.

Entonces el Señor dijo:

—Mira, voy a tirar la plomada en medio de mi pueblo Israel; no volveré a perdonarlo.

9»Los altares paganos de Isaac serán destruidos

y quedarán en ruinas los santuarios de Israel;

me levantaré con espada contra la casa de Jeroboán».

Amasías contra Amós

10Entonces Amasías, sacerdote de Betel, envió un mensaje a Jeroboán rey de Israel: «Amós está conspirando contra ti en medio de Israel. La tierra no puede soportar sus palabras, 11porque anda diciendo:

»“Jeroboán morirá a espada

e Israel será llevado cautivo

lejos de su tierra”».

12Entonces Amasías dijo a Amós:

—¡Vete de aquí, vidente! ¡Si quieres ganarte el pan profetizando, vete a la tierra de Judá! 13No vuelvas a profetizar en Betel, porque este es el santuario del rey; es el templo del reino.

14Amós respondió a Amasías:

—Yo no soy profeta ni hijo de profeta, sino que soy pastor y cultivo higos silvestres. 15Pero el Señor me sacó de detrás del rebaño y me dijo: “Ve y profetiza a mi pueblo Israel”. 16Así que oye la palabra del Señor. Tú dices:

»“No profetices contra Israel;

deja de predicar contra los descendientes de Isaac”.

17»Por eso, así dice el Señor:

»“Tu esposa se prostituirá en la ciudad

y tus hijos y tus hijas caerán a espada.

Tu tierra será medida y repartida,

tú mismo morirás en un país pagano

e Israel será llevado cautivo

lejos de su tierra”».