Amosi 3 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Amosi 3:1-15

Mashahidi Waitwa Dhidi Ya Israeli

13:1 Amo 2:10; Sef 2:5Sikilizeni neno hili alilosema Bwana dhidi yenu, enyi watu wa Israeli, dhidi ya jamaa nzima niliowapandisha toka Misri:

23:2 Kut 19:6; 1Pet 4:17; Lk 12:47; Mik 2:3; Eze 9:6; Dan 9:12; Mt 11:22; Rum 2:9; Kum 7:6; Yer 14:10“Ni ninyi tu niliowachagua

kati ya jamaa zote za dunia;

kwa hiyo nitawaadhibu

kwa ajili ya dhambi zenu zote.”

3Je, watu wawili hutembea pamoja

wasipokubaliana kufanya hivyo?

43:4 Za 104:21; Hos 5:14; Isa 42:13Je, simba hunguruma katika kichaka

wakati hana mawindo?

Aweza kuvuma katika pango

wakati ambao hajakamata chochote?

5Je, ndege aweza kuanguka kwenye mtego ulio ardhini

ambapo hajategewa chambo?

Je, mtego unaweza kufyatuka toka ardhini

wakati ambapo hakuna chochote cha kunasa?

63:6 Isa 14:24-27; 31:2; 45:7; Hes 10:2; Eze 33:3; Ay 39:24; Yer 4:21Je, tarumbeta inapopigwa mjini kujulisha hatari,

watu hawatetemeki?

Mji upatwapo na maafa,

je, si Bwana amesababisha?

73:7 1Sam 3:7; Mwa 6:13; 18:17; Mit 3:32; Yn 15:15; Yer 23:22; Mit 3:32; Dan 9:22-27; Ufu 1:1, 19Hakika Bwana Mwenyezi hatafanya neno lolote

bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.

83:8 1Kor 9:16; Yn 3:1-3; Mdo 4:20; Isa 31:4; 42:13; Yer 20:9Simba amenguruma:

je, ni nani ambaye hataogopa?

Bwana Mwenyezi ametamka:

je, ni nani awezaye kukosa kutoa unabii?

93:9 Yos 13:3; 2Nya 26:6Tangazeni katika ngome za Ashdodi

na katika ngome za Misri:

“Kusanyikeni juu ya milima ya Samaria;

angalieni wingi wa wasiwasi ulio ndani yake,

na uonevu ulio miongoni mwa watu wake.”

103:10 Yer 4:22; Amo 6:12; 5:7; Mik 6:10; Hab 2:8Bwana asema: “Hawajui kutenda lililo jema,

wale ambao hujilundikia nyara

na vitu vilivyotekwa katika ngome zao.”

113:11 Amo 2:5; 6:14; 2Fal 17:6Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi:

“Adui ataizingira nchi;

ataangusha chini ngome zenu

na kuteka nyara maboma yenu.”

123:12 1Sam 17:34; Es 1:6; Amo 6:4Hili ndilo asemalo Bwana:

“Kama vile mchungaji aokoavyo kinywani mwa simba

vipande viwili tu vya mfupa wa mguu

au kipande cha sikio,

hivyo ndivyo Waisraeli watakavyookolewa,

wale wakaao Samaria

kwenye kingo za vitanda vyao,

na katika Dameski

kwenye viti vyao vya fahari.”

13“Sikia hili na ushuhudie dhidi ya nyumba ya Yakobo,” asema Bwana, Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote.

143:14 Mwa 12:8; Amo 5:5-6; Kut 27:2; Law 26:18“Siku nitakapomwadhibu Israeli kwa sababu ya dhambi zake,

nitaharibu madhabahu za Betheli;

pembe za madhabahu zitakatiliwa mbali

na kuanguka chini.

153:15 Yer 36:22; Amu 3:20; 1Fal 22:39; Hos 10:5-8; Isa 34:5; Amo 5:11; 6:11Nitabomoa nyumba ya wakati wa masika,

pamoja na nyumba ya wakati wa kiangazi;

nyumba zilizonakshiwa kwa pembe za ndovu

na majumba makubwa ya fahari yatabomolewa,”

asema Bwana.