Amosi 1 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Amosi 1:1-15

11:1 2Sam 14:2; Zek 14:5; 2Fal 14:21-23; Hos 1:1; 2Nya 11:6; Za 78:70; 2Nya 26:23Maneno ya Amosi, mmoja wa wachunga wanyama wa Tekoa: yale aliyoyaona kuhusu Israeli miaka miwili kabla ya tetemeko la ardhi, wakati Uzia alikuwa mfalme wa Yuda, na Yeroboamu mwana wa Yehoashi alikuwa mfalme wa Israeli.

21:2 Isa 42:13; Yoe 3:16; Amo 9:3; Yer 12:4; Za 29:3Alisema:

Bwana ananguruma toka Sayuni,

pia ananguruma kutoka Yerusalemu;

malisho ya wachunga wanyama yanakauka,

kilele cha Karmeli kinanyauka.”

Hukumu Juu Ya Majirani Wa Israeli

31:3 Isa 8:4; 7:9; 17:1-3; 8:4; 2Fal 10:33; Amo 2:6Hili ndilo asemalo Bwana:

“Kwa dhambi tatu za Dameski,

hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.

Kwa sababu aliipura Gileadi

kwa vyombo vya chuma vyenye meno.

41:4 Eze 30:8; Yer 17:27; 49:23-27; 1Fal 20:1; 19:17; 2Fal 6:24Nitatuma moto juu ya nyumba ya Hazaeli

ambao utateketeza ngome za Ben-Hadadi.

51:5 Yer 51:30; 49:27; Isa 7:1, 16; 22:6; Zek 9:1; 2Fal 16:9Nitalivunja lango la Dameski;

nitamwangamiza mfalme aliyeko katika Bonde la Aveni,1:5 Bonde la Aveni maana yake Bonde la Uovu.

na yeye ambaye anaishika fimbo ya utawala katika Beth-Edeni.

Watu wote wa Aramu watakwenda uhamishoni huko Kiri,”

asema Bwana.

61:6 2Nya 28:18; 1Sam 6:17; Mwa 10:19; 14:6; Oba 1:11; Sef 2:4Hili ndilo asemalo Bwana:

“Kwa dhambi tatu za Gaza,

hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.

Kwa sababu walichukua mateka jumuiya nzima

na kuwauza kwa Edomu,

71:7 2Fal 18:8nitatuma moto juu ya kuta za Gaza

ambao utateketeza ngome zake.

81:8 2Nya 26:6; Za 81:14; Eze 25:16; Isa 14:28-32; 34:8; Sef 2:4-7Nitamwangamiza mfalme wa Ashdodi

na yeye aishikaye fimbo ya utawala katika Ashkeloni.

Nitaugeuza mkono wangu dhidi ya Ekroni,

hadi Mfilisti wa mwisho atakapokufa,”

asema Bwana Mwenyezi.

91:9 Isa 23:1-18; 1Fal 5:12; 9:11-14; Yer 25:22; Yoe 3:4Hili ndilo asemalo Bwana:

“Kwa dhambi tatu za Tiro,

hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.

Kwa sababu ameuza jumuiya nzima ya mateka kwa Edomu,

na kutokujali mapatano ya undugu,

101:10 Yer 47:6; Eze 26:2-4; Isa 23:1-18; 34:8; Zek 9:1-4Nitatuma moto kwenye kuta za Tiro

ambao utateketeza ngome zake.”

111:11 Yer 49:7-22; Eze 25:12-14; Zek 1:15; Mal 1:4; Za 83:6; Hes 20:14-21; 2Nya 28:17Hili ndilo Bwana asemalo:

“Kwa dhambi tatu za Edomu,

hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.

Kwa sababu alimfuatia ndugu yake kwa upanga,

alikataa kuonyesha huruma yoyote,

kwa sababu hasira yake kali iliendelea kupanda wakati wote

na ghadhabu iliwaka bila kuzuiliwa.

121:12 Mwa 36:11-15; Mao 1:9-10; Isa 34:5; 63:1-6; Eze 25:12-14; Mal 1:2-5Nitatuma moto juu ya Temani

ambao utateketeza ngome za Bosra.”

131:13 Mwa 19:38; 34:29; Yer 49:1-6; 2Fal 8:12; Hos 13:16; Eze 21:28Hili ndilo asemalo Bwana:

“Kwa dhambi tatu za Amoni,

hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.

Kwa sababu aliwatumbua wanawake wajawazito wa Gileadi

ili kuongeza mipaka yake.

141:14 Kum 3:11; Ay 39:25; Eze 25:5; Amo 2:2; Isa 30:30; Yer 23:19Nitatuma moto kwenye kuta za Raba

ambao utateketeza ngome zake

katikati ya vilio vya vita katika siku ya mapigano,

katikati ya upepo mkali katika siku ya dhoruba.

151:15 Yer 25:21; 49:1-3; Eze 21:28-32; 25:2-7; 1Nya 20:1Mfalme wake atakwenda uhamishoni,

yeye pamoja na maafisa wake,”

asema Bwana.