Salamu
11:1 Mdo 11:30; 2Yn 1Mzee:
Kwa Gayo rafiki yangu, nimpendaye katika kweli.
Gayo Anasifiwa Kwa Ajili Ya Ukarimu Wake
21:2 2Yn 4Mpendwa, naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya njema kama vile roho yako ifanikiwavyo. 31:3 Mdo 1:16; 2Yn 4Ilinifurahisha sana baadhi ya ndugu walipokuja na kutueleza juu ya uaminifu wako katika kweli na jinsi unavyoendelea kuenenda katika hiyo kweli. 41:4 1Kor 4:14; 1Yn 1:2Sina furaha kubwa kuliko hii, kusikia kwamba watoto wangu wanaenenda katika kweli.
51:5 Rum 12:13Rafiki mpendwa, wewe ni mwaminifu kwa yale unayowatendea ndugu, ingawa wao ni wageni kwako. 61:6 1Kor 16:11; 2Kor 1:16; Efe 4:1Wameshuhudia kuhusu upendo wako mbele ya kanisa. Utafanya vyema ukiwasafirisha kama inavyostahili kwa Mungu. 71:7 Yn 15:21; Mdo 20:33, 35Ilikuwa ni kwa ajili ya hilo Jina waliondoka, bila kukubali kupokea msaada wowote kutoka kwa watu wasioamini. 81:8 Ebr 13:2; 2Yn 10Kwa hiyo imetupasa sisi kuonyesha ukarimu kwa watu kama hao ili tuweze kutenda kazi pamoja kwa ajili ya kweli.
Deotrefe
9Nililiandikia kanisa, lakini Deotrefe, yeye apendaye kujifanya wa kwanza, hakubali mamlaka yetu. 101:10 3Yn 14; 2Yn 5; Yn 9:22, 34Hivyo kama nikija, nitakumbuka matendo yake atendayo, akitusingizia kwa maneno ya hila. Wala hatosheki na hayo anayotusingizia, bali pia hukataa kuwakaribisha ndugu, na hata huwazuia wale walio tayari kufanya hivyo na kuwafukuza watoke kanisani.
Demetrio
111:11 Za 34:14; 37:27; 1Yn 2:29; 3:6, 9, 10Rafiki mpendwa, usiige lile lililo baya bali lile lililo jema. Yeyote atendaye mema atoka kwa Mungu, bali atendaye mabaya hajamwona Mungu.
121:12 Yn 19:39; 21:24Kila mtu ameshuhudia mema kuhusu Demetrio, vivyo hivyo hata na hiyo kweli yenyewe. Sisi pia twashuhudia mema juu yake, nanyi mwajua kwamba ushuhuda wetu ni kweli.
Salamu Za Mwisho
131:13 2Yn 12Ninayo mambo mengi ya kukuandikia, lakini sipendi kuandika kwa kalamu na wino. 141:14 2Yn 12; Rum 1:7; Efe 6:23; Yn 10:3Badala yake, nataraji kukuona upesi, nasi tutaongea pamoja ana kwa ana.
15Amani iwe kwako. Rafiki zetu walioko hapa wanakusalimu. Wasalimu hao rafiki zetu walioko huko, kila mmoja kwa jina lake.