Yule Mtu Wa Kuasi
12:1 Mk 13:27; 1The 4:15-17Ndugu, kuhusu kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo na kukusanyika kwetu pamoja mbele zake, tunawasihi, 22:2 2The 3:17; 1Kor 1:8msiyumbishwe kwa urahisi wala msitiwe wasiwasi na roho wala neno au barua inayosemekana kuwa imetoka kwetu, isemayo kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwako. 32:3 Mk 13:5; Dan 8:25; Ufu 13:5, 6Mtu yeyote na asiwadanganye kwa namna yoyote kwa maana siku ile haitakuja mpaka uasi utokee kwanza, na yule mtu wa kuasi adhihirishwe, yule ambaye amehukumiwa kuangamizwa kabisa. 42:4 1Kor 8:5; Isa 14:13, 14; Eze 28:2Yeye atapingana na kujitukuza juu ya kila kitu kiitwacho Mungu au kinachoabudiwa, ili kujiweka juu katika Hekalu la Mungu, akijitangaza mwenyewe kuwa ndiye Mungu.
52:5 1The 3:4Je, hamkumbuki ya kwamba nilipokuwa pamoja nanyi niliwaambia mambo haya? 62:6 2The 2:7Nanyi sasa mnajua kinachomzuia, ili apate kudhihirishwa wakati wake utakapowadia. 72:7 2The 2:6Maana ile nguvu ya siri ya uasi tayari inatenda kazi, lakini yule anayeizuia ataendelea kufanya hivyo mpaka atakapoondolewa. 82:8 Isa 11:4; Ufu 2:16Hapo ndipo yule mwasi atafunuliwa, ambaye Bwana Yesu atamteketeza kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kabisa kwa utukufu wa kuja kwake. 92:9 Mt 24:24; Ufu 13:13Kuja kwa yule mwasi kutaonekana kana kwamba ni kutenda kazi kwake Shetani ambaye hutumia nguvu zote, ishara, maajabu ya uongo, 102:10 1Kor 1:18na kila aina ya uovu kwa wale wanaoangamia kwa sababu walikataa kuipenda kweli wapate kuokolewa. 112:11 Rum 1:28Kwa sababu hii, Mungu ameruhusu watawaliwe na nguvu ya udanganyifu, ili waendelee kuamini uongo, 122:12 Rum 1:32na wahukumiwe wote ambao hawakuiamini ile kweli, bali wamefurahia uovu.
Simameni Imara
132:13 Efe 1:4; 1The 5:9; 1Pet 1:2Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu daima kwa ajili yenu, ndugu mpendwao na Bwana, kwa sababu Mungu aliwachagua ninyi tangu mwanzo ili mwokolewe kwa kutakaswa na Roho kwa kuiamini kweli. 142:14 Rum 8:28; 11:29; 1The 1:5Kwa kusudi hili Mungu aliwaita kwa njia ya kuhubiri kwetu Injili, ili mpate kushiriki katika utukufu wa Bwana Yesu Kristo. 152:15 1Kor 16:13; 11:2Hivyo basi, ndugu wapendwa, simameni imara na myashike sana yale mafundisho tuliyowapa ikiwa ni kwa maneno ya kinywa au kwa barua.
162:16 Yn 3:16Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe na Mungu Baba yetu, aliyetupenda na kwa neema yake akatupatia faraja ya milele na tumaini jema, 172:17 1The 3:2; 2The 3:3awafariji mioyo yenu na kuwaimarisha katika kila neno na tendo jema.