2 Wakorintho 5 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

2 Wakorintho 5:1-21

Makao Yetu Ya Mbinguni

15:1 1Kor 15:47; Isa 38:12; 1Pet 1:13-14Kwa maana twajua kama hema yetu ya dunia tunayoishi ikiharibiwa, tunalo jengo kutoka kwa Mungu, nyumba iliyo ya milele kule mbinguni, isiyojengwa kwa mikono ya wanadamu. 2Katika hema hii twalia kwa uchungu, tukitamani kuvikwa makao yetu ya mbinguni, 3kwa kuwa tukiisha kuvikwa hatutaonekana tena kuwa uchi. 45:4 1Kor 15:33, 54; Rum 8:23; 2Kor 5:2; 1Kor 15:51Kwa kuwa tukiwa bado katika hema hii twalia kwa uchungu na kulemewa, kwa sababu hatutaki kuvuliwa bali kuvikwa makao yetu ya mbinguni ili kwamba kile kipatikanacho na mauti kimezwe na uzima. 55:5 Rum 8:23; 2Kor 1:22; Efe 1:13-14Basi Mungu ndiye alitufanya kwa ajili ya jambo lilo hilo naye ametupa Roho Mtakatifu kuwa amana, akituhakikishia ahadi ya kile kijacho.

65:6 Ebr 11:13Kwa hiyo siku zote tunalo tumaini, hata ingawa tunajua kwamba wakati tukiwa katika mwili huu, tuko mbali na Bwana, 75:7 1Kor 13:12; 2Kor 4:18kwa maana twaenenda kwa imani wala si kwa kuona. 85:8 Yn 12:26; Flp 1:23Naam, tunalo tumaini na ingekuwa bora zaidi kuuacha mwili huu na kwenda kukaa na Bwana. 95:9 Rum 14:18; Efe 5:10; Kol 1:10; 1The 4:1Kwa hiyo, kama tuko katika mwili huu au tuko mbali nao, lengo letu ni kumpendeza Bwana. 105:10 Mt 16:27; Mdo 10:42; Rum 2:16; 14:10; Efe 6:8Kwa kuwa sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mmoja apate kulipwa kwa ajili ya yale ambayo yametendwa katika mwili wake, yakiwa mema au mabaya.

Huduma Ya Upatanisho

115:11 Ay 23:15; Ebr 10:31; 12:29; Yud 23; 2Kor 4:2Basi, kwa kuwa tunajua kumcha Bwana, tunajitahidi kuwavuta wengine. Lakini Mungu anatufahamu dhahiri, nami natumaini kwamba tu dhahiri katika dhamiri zenu pia. 125:12 2Kor 3:1; 1:14Sio kwamba tunajaribu kujistahilisha kwenu tena, lakini tunataka kuwapa nafasi ili mwone fahari juu yetu mweze kuwajibu hao wanaoona fahari juu ya mambo yanayoonekana badala ya mambo yaliyo moyoni. 135:13 2Kor 11:1, 16-17; 12:11Kama tumerukwa na akili, ni kwa ajili ya Mungu; kama tuna akili timamu, ni kwa ajili yenu. 145:14 Rum 6:6-7; Gal 2:20; Kol 3:3Kwa kuwa upendo wa Kristo unatutia nguvu, kwa sababu tunasadiki kuwa mmoja alikufa kwa ajili ya wote, kwa hiyo wote walikufa. 155:15 Rum 14:7-9; 4:25Naye alikufa kwa ajili ya watu wote, ili kwamba wote wanaoishi wasiishi tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa na kufufuliwa tena kwa ajili yao.

165:16 2Kor 10:4; 11:18Hivyo tangu sasa hatumwangalii mtu yeyote kwa mtazamo wa kibinadamu. Ingawa wakati fulani tulimwangalia Kristo kwa namna ya kibinadamu, hatumwangalii tena hivyo. 175:17 Rum 16:3; Yn 1:13; Rum 6:4; Gal 6:15; Isa 65:17; Ufu 21:4-5Kwa hiyo kama mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama, yamekuwa mapya. 185:18 Rum 11:36; 5:10Haya yote yanatokana na Mungu, ambaye ametupatanisha sisi na nafsi yake kwa njia ya Yesu Kristo na kutupata sisi huduma ya upatanisho: 19Kwamba Mungu alikuwa ndani ya Kristo akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake mwenyewe, akiwa hawahesabii watu dhambi zao. Naye ametukabidhi sisi ujumbe huu wa upatanisho. 205:20 2Kor 6:1; Efe 6:20; Isa 27:5Kwa hiyo sisi ni mabalozi wa Kristo, kana kwamba Mungu anawasihi kupitia kwa vinywa vyetu. Nasi twawaomba sana ninyi kwa niaba ya Kristo, mpatanishwe na Mungu. 215:21 Ebr 4:15; 7:26; 1Pet 2:22-24; 1Yn 3:5; Rum 1:17; 1Kor 1:30Kwa maana Mungu alimfanya yeye asiyekuwa na dhambi kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kufanywa haki ya Mungu kwake yeye.