2 Wakorintho 4 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

2 Wakorintho 4:1-18

Hazina Ya Mbinguni Katika Vyombo Vya Udongo

14:1 1Kor 7:25; 1Tim 1:13-16; Za 18:45; Isa 40:31Kwa hiyo, kwa kuwa tuna huduma hii kwa rehema za Mungu, hatukati tamaa. 24:2 Rum 6:21; 1Kor 4:5; 2Kor 2:17; Ebr 4:12; 2Kor 5:11Tumekataa mambo ya siri na ya aibu, wala hatufuati njia za udanganyifu, tukichanganya Neno la Mungu na uongo. Kinyume cha hayo, tunadhihirisha kweli waziwazi na kujitambulisha wenyewe kwenye dhamiri ya kila mtu mbele za Mungu. 34:3 2Kor 2:12; 3:14; 1Kor 1:18Hata nayo Injili yetu kama imetiwa utaji, ni kwa wale tu wanaopotea. 44:4 Yn 12:31; 1Kor 1:20; 2Kor 3:14; Yn 14:9Kwa habari yao, mungu wa dunia hii amepofusha akili za wasioamini, ili wasione nuru ya Injili ya utukufu wa Kristo, aliye sura ya Mungu. 54:5 1Kor 1:13; 1:23; 9:19Kwa maana hatujihubiri sisi wenyewe ila tunamhubiri Yesu Kristo kuwa ni Bwana na sisi ni watumishi wenu kwa ajili ya Yesu. 64:6 Mwa 1:3; Za 18:28; 2Pet 1:19Kwa kuwa Mungu, yeye aliyesema, “Nuru na ingʼae gizani,” ameifanya nuru yake ingʼae mioyoni mwetu ili kutupatia nuru ya maarifa ya utukufu wa Mungu katika uso wa Kristo.

74:7 Ay 4:19; Isa 64:8; 2Tim 2:20; Amu 7:2; 1Kor 2:5; 2Kor 6:7Lakini tunayo hazina hii katika vyombo vya udongo, ili ijulikane wazi kwamba uwezo huu wa ajabu unatoka kwa Mungu wala si kwetu. 84:8 2Kor 7:5; Gal 4:20Twataabika kila upande lakini hatuangamizwi; twaona wasiwasi lakini hatukati tamaa; 94:9 Yn 15:20; Rum 8:35; Ebr 13:5; Za 37:24; Mit 24:16twateswa lakini hatuachwi; twatupwa chini lakini hatupondwi. 104:10 Rum 6:6; 2Kor 1:5; Rum 6:5Siku zote twachukua katika mwili kufa kwake Yesu ili kwamba uzima wa Yesu uweze kudhihirika katika miili yetu. 114:11 Rum 8:36Kwa maana sisi tulio hai siku zote tumetolewa tufe kwa ajili ya Yesu, ili kwamba uzima wake upate kudhihirishwa katika mwili wetu upatikanao na mauti. 124:12 2Kor 13:9Hivyo basi, mauti inatenda kazi ndani yetu, bali uzima unatenda kazi ndani yenu.

134:13 Za 116:10; 1Kor 12:29Imeandikwa, “Niliamini, kwa hiyo nimesema.” Kwa roho yule yule wa imani pia tuliamini na hivyo tunasema, 144:14 Mdo 2:24; 1The 4:14; Efe 5:27; Kol 1:22; Yud 24kwa sababu tunajua kwamba yeye aliyemfufua Bwana Yesu kutoka kwa wafu, atatufufua sisi pia pamoja na Yesu na kutuleta sisi pamoja nanyi mbele zake. 154:15 1Kor 1:11; 9:11Haya yote ni kwa faida yenu, ili kwamba neema ile inavyowafikia watu wengi zaidi na zaidi, ipate kusababisha shukrani nyingi kwa utukufu wa Mungu.

164:16 Za 18:45; Rum 7:22; Za 103:5Kwa hiyo, hatukati tamaa. Ingawa utu wetu wa nje unachakaa, utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. 174:17 Za 30:5; Rum 8:18; 1Pet 1:6-7Kwa maana dhiki yetu nyepesi iliyo ya kitambo inatutayarisha kwa ajili ya utukufu wa milele unaozidi kuwa mwingi kupita kiasi, 184:18 2Kor 5:7; Rum 8:24; Ebr 11kwa sababu hatuangalii yale yanayoweza kuonekana bali yale yasiyoweza kuonekana. Kwa maana yale yanayoweza kuonekana ni ya kitambo tu, bali yale yasiyoweza kuonekana ni ya milele.