2 Wakorintho 2 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

2 Wakorintho 2:1-17

12:1 2Kor 1:23; 12:20, 21; 13:10Hivyo nilikusudia moyoni mwangu nisifanye ziara nyingine yenye kuwaumiza ninyi. 22:2 2Kor 7:8Kwa kuwa kama nikiwahuzunisha ninyi, ni nani aliyebaki wa kunifurahisha isipokuwa ninyi ambao nimewahuzunisha? 32:3 2Kor 7:8-12; 12:21; 7:16; 8:22; Gal 5:10; 2The 3:4Niliandika hivyo kama nilivyofanya, ili nikija nisihuzunishwe na wale watu ambao wangenifanya nifurahi. Nina uhakika na ninyi nyote, kwamba wote mngeshiriki furaha yangu. 42:4 2Kor 7:8-12; 12:20, 21; 13:10Kwa maana niliwaandikia kutokana na dhiki kubwa na kutaabika sana kwa moyo wangu tena kwa machozi mengi, shabaha yangu si ili niwasababishe mhuzunike bali kuwaonyesha kina cha upendo wangu kwenu.

Msamaha Kwa Mwenye Dhambi

52:5 1Kor 5:1-2; Gal 4:12; 1Kor 5:1Lakini ikiwa mtu yeyote amesababisha huzuni, kwa kiasi fulani hakunihuzunisha mimi kama vile alivyowahuzunisha ninyi nyote, ili nisiwe mkali kupita kiasi. 62:6 1Kor 5:4-5; 2Kor 7:11Adhabu hii aliyopewa na wengi inamtosha. 72:7 Gal 6:1; Efe 4:32; Kol 3:13Basi sasa badala yake, inawapasa kumsamehe na kumfariji, ili asigubikwe na huzuni kupita kiasi. 8Kwa hiyo, nawasihi, mpate kuuthibitisha tena upendo wenu kwa ajili yake. 92:9 2Kor 7:8-12; 7:15; 10:6Sababu ya kuwaandikia ni kuona kama mngeweza kushinda hilo jaribio na kutii katika kila jambo. 102:10 Lk 10:16Kama ninyi mkimsamehe mtu yeyote, mimi pia nimemsamehe. Kile nilichosamehe, kama kulikuwa na kitu chochote cha kusamehe, nimekwisha kusamehe mbele ya Kristo kwa ajili yenu, 112:11 Mt 4:10; Lk 22:31; 2Kor 4:4; 1Pet 5:8ili Shetani asitushinde. Kwa maana hatuachi kuzijua hila zake.

Wasiwasi Wa Paulo Huko Troa

122:12 Rum 1:1; 2Kor 4:3-4; 8:18; 9:13; 1The 3:2; Mdo 14:21Basi nilipofika Troa kuhubiri Injili ya Kristo na kukuta kwamba Bwana alikuwa amenifungulia mlango, 132:13 2Kor 7:5; 7:6-13; 8:6-23; 12:18; Gal 2:1-3; Tit 1:4; Mdo 16:9bado nilikuwa sina utulivu akilini mwangu kwa sababu sikumkuta ndugu yangu Tito huko. Hivyo niliagana nao nikaenda Makedonia.

142:14 Rum 6:17; 7:25; 1Kor 15:57; 2Kor 9:15; Eze 20:41; Efe 5:2; Flp 4:18; 2Kor 8:7Lakini Mungu ashukuriwe, yeye ambaye siku zote hutufanya tuandamane kwa ushindi tukiwa ndani ya Kristo. Naye kupitia kwetu hueneza kila mahali harufu nzuri ya kumjua yeye. 152:15 Mwa 8:21; Kut 29:18Kwa maana sisi kwa Mungu ni harufu nzuri ya manukato ya Kristo miongoni mwa wale wanaookolewa na kwa wale wanaopotea. 162:16 Lk 2:34; Yn 3:36; 2Kor 3:5-6Kwa wale wanaopotea, sisi ni harufu ya mauti iletayo mauti; lakini kwa wale wanaookolewa, sisi ni harufu nzuri iletayo uzima. Ni nani awezaye mambo hayo? 172:17 Mdo 20:33; 2Kor 4:2; 1The 2:5; 1Kor 5:8; 2Kor 1:12; 12:19Tofauti na watu wengine wengi, sisi hatufanyi biashara na Neno la Mungu kwa ajili ya kupata faida. Kinyume chake, katika Kristo tunalisema Neno la Mungu kwa unyoofu, kama watu tuliotumwa kutoka kwa Mungu.