2 Wafalme 6 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version

2 Wafalme 6:1-33

Shoka Laelea

16:1 1Sam 10:5Wana wa manabii wakamwambia Elisha, “Tazama, mahali hapa tunapokutana nawe ni padogo sana kwetu. 2Twendeni Yordani, mahali ambapo kila mmoja wetu anaweza kupata nguzo moja, nasi tujenge huko mahali petu pa kuishi.”

Naye akawaambia, “Nendeni.”

3Kisha mmoja wao akasema, “Je, tafadhali, huwezi kufuatana na watumishi wako?”

Elisha akajibu, “Nitakuja.” 4Naye akaenda pamoja nao.

Basi wakaenda Yordani, nao wakaanza kukata miti. 5Mmoja wao alipokuwa anakata mti, shoka lilitumbukia kwenye maji. Akalia, “Ee bwana wangu, shoka lilikuwa la kuazima!”

66:6 Kut 15:25; 2Fal 2:21Mtu wa Mungu akauliza, “Je, liliangukia wapi?” Alipomwonyesha mahali penyewe, Elisha akakata kijiti na kukitupa mahali pale, nalo shoka likaelea. 7Akasema, “Lichukue.” Kisha yule mtu akanyoosha mkono wake, akalichukua.

Elisha Awanasa Waaramu Waliopofushwa

8Wakati huo mfalme wa Aramu alikuwa akipigana vita na Israeli. Baada ya kukubaliana na maafisa wake, akasema, “Nitapiga kambi yangu mahali fulani na fulani.”

96:9 2Fal 6:12Mtu wa Mungu akatuma ujumbe kwa mfalme wa Israeli: “Jihadhari usije ukapita mahali pale, kwa sababu Waaramu wanashuka huko.” 106:10 Yer 11:18Kwa hiyo mfalme wa Israeli akatuma neno la tahadhari mahali pale alikokuwa ameelekezwa na mtu wa Mungu. Mara kwa mara Elisha alimwonya mfalme kwamba watu wawe macho kwenye maeneo kama hayo.

11Hili lilimfadhaisha sana mfalme wa Aramu. Akawaita maafisa wake, akawauliza, “Je, hamtaniambia ni nani miongoni mwenu aliye upande wa mfalme wa Israeli?”

126:12 2Fal 6:9Mmoja wa maafisa wake akasema, “Mfalme bwana wangu, hakuna hata mmoja wetu. Lakini Elisha, yule nabii aliye Israeli, humwambia mfalme wa Israeli hata yale maneno unayozungumza katika chumba chako cha kulala.”

136:13 Mwa 37:17Mfalme akaagiza akisema, “Nendeni, mkatafute aliko, ili niweze kutuma watu kumkamata.” Taarifa ikarudi kwamba, “Yuko Dothani.” 146:14 2Fal 1:9Ndipo akatuma farasi na magari ya vita na jeshi lenye nguvu huko. Walikwenda usiku na kuuzunguka mji.

15Kesho yake asubuhi na mapema, mtumishi wa mtu wa Mungu alipoamka na kutoka nje, jeshi, pamoja na farasi na magari ya vita, likawa limeuzunguka mji. Mtumishi wake akasema, “Ole wetu, bwana wangu! Tutafanya nini?”

166:16 2Nya 32:7; Za 55:18Nabii akajibu, “Usiogope. Wale walio pamoja nasi ni wengi zaidi kuliko wale walio pamoja nao.”

17Kisha Elisha akaomba, “Ee Bwana, mfumbue macho huyu mtumishi ili apate kuona.” Ndipo Bwana akayafumbua macho ya yule mtumishi, naye akatazama na kuona vilima vimejaa farasi na magari ya moto, yamemzunguka Elisha pande zote.

186:18 Mwa 19:11; Mdo 13:11Wakati adui waliposhuka kumwelekea, Elisha akamwomba Bwana: “Wapige watu hawa kwa upofu.” Basi Mungu akawapiga kwa upofu, kama Elisha alivyoomba.

19Elisha akawaambia, “Hii sio njia yenyewe, na huu sio huo mji. Nifuateni mimi, nami nitawapeleka kwa huyo mtu mnayemtafuta.” Naye akawapeleka Samaria.

20Baada ya kuingia mjini, Elisha akasema, “Bwana, yafungue macho ya watu hawa ili wapate kuona.” Ndipo Bwana akayafungua macho yao, na walipotazama, kumbe hapo ndipo walipojikuta, ndani ya Samaria.

216:21 2Fal 5:13Wakati mfalme wa Israeli alipowaona, akamuuliza Elisha, “Je, baba yangu, niwaue?”

226:22 Kum 20:11; 2Nya 28:8-15Naye akajibu, “Usiwaue. Je, utawaua watu uliowateka kwa upanga wako mwenyewe na upinde wako? Wape chakula na maji ili wapate kula na kunywa, na kisha wamrudie bwana wao.” 236:23 2Fal 5:2Basi akawaandalia karamu kubwa, na baada ya kula na kunywa, akawaaga nao wakarudi kwa bwana wao. Hivyo, vikosi kutoka Aramu vikakoma kuvamia nchi ya Israeli.

Njaa Katika Samaria Iliyozingirwa

246:24 1Fal 15:18; Kum 28:52Baada ya kitambo kidogo, Ben-Hadadi mfalme wa Aramu akaandaa jeshi lake lote akapanda kwenda kuihusuru Samaria. 256:25 Law 26:26; Isa 36:12Kukawa na njaa kuu katika mji. Samaria ilizingirwa kwa muda mrefu, kiasi kwamba kichwa cha punda kiliuzwa kwa shekeli themanini6:25 Shekeli 80 za fedha ni sawa na kilo moja. za fedha, na robo ya kibaba6:25 Robo ya kibaba ni sawa na lita 0.3. cha mavi ya njiwa kiliuzwa kwa shekeli tano6:25 Shekeli tano za fedha ni sawa na gramu 55. za fedha.

26Wakati mfalme wa Israeli alipokuwa anapita juu ya ukuta, mwanamke mmoja akamlilia, “Bwana wangu mfalme, nisaidie!”

27Mfalme akajibu, “Ikiwa Bwana hakusaidii, nitakutolea wapi msaada? Je, ni kutoka kwenye sakafu ya kupuria? Au kwenye shinikizo la divai?” 28Kisha akamuuliza, “Kwani kuna nini?”

Yule mwanamke akamjibu, “Huyu mwanamke aliniambia, ‘Mtoe mwanao ili tupate kumla leo, na kesho tutamla mwanangu.’ 296:29 Law 26:29; Kum 28:53-55Basi tukampika mwanangu na kumla. Siku iliyofuata nikamwambia, ‘Mtoe mwanao ili tupate kumla.’ Lakini akawa amemficha.”

306:30 Isa 22:15; Mwa 37:34Wakati mfalme aliposikia maneno ya yule mwanamke, alirarua mavazi yake. Naye alipoendelea kutembea ukutani, watu wakamtazama, na ndani ya mavazi yake alikuwa amevaa nguo ya gunia mwilini mwake. 31Akasema, “Mungu na anitendee hivyo na kuzidi, ikiwa kichwa cha Elisha mwana wa Shafati kitabaki juu ya mabega yake leo!”

326:32 Eze 8:1; 1Fal 18:4Wakati huu, Elisha alikuwa ameketi ndani ya nyumba yake, akiwa pamoja na wazee. Mfalme akatuma mjumbe kumtangulia, lakini kabla hajafika, Elisha akawaambia wale wazee, “Hammwoni huyu muuaji jinsi anavyotuma mtu kukata kichwa changu? Tazama, wakati mjumbe huyo atakapofika, fungeni mlango na mzuieni asiingie. Je, vishindo vya nyayo za bwana wake haviko nyuma yake?”

336:33 Ay 2:9Alipokuwa angali bado anazungumza nao, mjumbe akamfikia. Naye mfalme akasema, “Maafa haya yanatoka kwa Bwana. Kwa nini niendelee kumngoja Bwana zaidi?”

Chinese Contemporary Bible 2023 (Traditional)

列王紀下 6:1-33

以利沙找回斧頭

1一群先知對以利沙說:「你看,我們住的地方實在太小了。 2請讓我們去約旦河吧,我們每人都可以從那裡砍一根木頭蓋房子居住。」以利沙說:「你們去吧。」 3其中一人請以利沙一起去,以利沙答應了, 4便和他們一起去約旦河砍伐樹木。 5有個人砍樹的時候,斧頭掉進了水裡。他大喊:「唉!師傅,這把斧頭是借來的。」 6上帝的僕人問:「斧頭掉在哪裡了?」他就指給以利沙看。以利沙砍了一根樹枝拋進水裡,斧頭便浮了上來。 7以利沙說:「你去拿上來吧!」他便伸手拿起了斧頭。

以利沙使亞蘭軍敗退

8亞蘭王與以色列人交戰,他和臣僕商議要在某處安營。 9上帝的僕人傳信給以色列王,說:「你要小心,不要經過那個地方,因為亞蘭人埋伏在那裡。」 10以色列王派人到上帝的僕人所說的地方,警告那裡的人要小心防備。這樣的事情發生了好幾次。

11亞蘭王因此十分惱怒,召來臣僕質問他們:「你們當中誰向以色列王洩露了我們的計劃?」 12一位臣僕說:「我主我王啊,沒有人洩露。是以色列的先知以利沙將王在寢宮所談的事告訴了以色列王。」 13王說:「去找出他在哪裡,我派人去捉拿他。」王得知以利沙多坍後, 14便派出大隊人馬和戰車前往那裡,他們在夜間抵達多坍,把城圍住。 15上帝僕人的侍者清早起來,走到外面,看見城被軍隊、車馬包圍,就對上帝的僕人說:「唉!我主啊,我們該怎麼辦呢?」 16上帝的僕人說:「不要害怕!我們的兵馬比他們的還要多。」 17他隨後禱告:「耶和華啊,求你開他的眼睛,讓他看見。」於是,耶和華開那個侍者的眼睛,他就看見山上到處都是火車火馬圍繞著以利沙18亞蘭人向以利沙衝來,以利沙祈求耶和華說:「求你使他們瞎眼。」耶和華聽了以利沙的禱告,使他們瞎了眼。 19以利沙對他們說:「不是這條路,也不是這座城。跟我來,我帶你們到你們要找的人那裡。」以利沙把他們領到撒瑪利亞

20他們進城後,以利沙禱告:「耶和華啊,求你開他們的眼睛,讓他們看見。」耶和華開了他們的眼睛,他們就看見了,發現自己在撒瑪利亞城中。 21以色列王看見他們,問以利沙說:「我父啊,我可以殺他們嗎?」 22以利沙答道:「不可殺他們。豈可殺用刀和弓抓來的俘虜呢?給他們吃的喝的,讓他們吃喝完了回自己主人那裡吧。」 23於是,以色列王為他們大擺宴席,等他們吃喝完畢,便放他們回自己主人那裡。之後,亞蘭人不再侵犯以色列

撒瑪利亞城被圍困

24後來,亞蘭便·哈達召集全軍圍困撒瑪利亞25撒瑪利亞被困後,城裡陷入嚴重饑荒,以致一個驢頭可賣二十兩銀子,二百克鴿子糞可賣一兩銀子。 26一天,以色列王從城牆上走過,一個婦人向他呼喊:「我主我王啊,求你幫幫我!」 27王說:「如果耶和華不幫助你,我怎能幫助你呢?我豈有麥子和酒? 28你有什麼難處呢?」婦人說:「這個女人對我說,『我們今天吃你兒子,明天再吃我兒子。』 29於是我們把我兒子煮了吃。第二天我叫她把她兒子交出來,她卻把兒子藏了起來。」 30王聽了婦人的話,就撕裂衣服。王走在城牆上,人們都看見他貼身穿著麻衣。 31王說:「如果今天沙法的兒子以利沙的頭顱還留在他頸項上,願上帝重重地懲罰我!」

32王派使者去以利沙那裡。那時,以利沙正與長老們坐在他家中。使者到達之前,以利沙對長老說:「你們看,這兇手派人來斬我的頭。使者到達時,你們要把他關在門外。他後面不就是他主人的腳步聲嗎?」 33話音未落,使者已經到了,說:「既然這禍是從耶和華來的,我何必再仰望祂呢?」