2 Wafalme 13 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

2 Wafalme 13:1-25

Yehoahazi Mfalme Wa Israeli

1Katika mwaka wa ishirini na tatu wa utawala wa Yoashi mwana wa Ahazia mfalme wa Yuda, Yehoahazi mwana wa Yehu alianza kutawala Israeli katika Samaria, naye akatawala miaka kumi na saba. 213:2 1Fal 12:26-33Akafanya maovu machoni pa Bwana kwa kufuata dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambazo alikuwa amesababisha Israeli kuzitenda, na wala hakuziacha. 3Kwa hiyo hasira ya Bwana ikawaka dhidi ya Israeli na kwa muda mrefu akawaweka chini ya utawala wa Hazaeli mfalme wa Aramu, na Ben-Hadadi mwanawe.

413:4 Kum 4:29; Hes 10:9Ndipo Yehoahazi akamsihi Bwana rehema, naye Bwana akamsikiliza, kwa maana aliona jinsi mfalme wa Aramu alivyokuwa akiwatesa Israeli vikali. 513:5 Mwa 45:7; Amu 2:18Bwana akamtoa mwokozi kwa ajili ya Israeli, nao wakaokoka kutoka kwenye mamlaka ya Aramu. Hivyo Waisraeli wakaishi katika nyumba zao wenyewe kama ilivyokuwa hapo awali. 613:6 1Fal 16:33Lakini hawakuziacha dhambi za nyumba ya Yeroboamu, ambazo alisababisha Israeli kuzitenda, bali wakaendelea kuzitenda. Nguzo ya Ashera pia iliendelea kusimama katika Samaria.

713:7 2Sam 22:43Hapakubaki kitu chochote katika jeshi la Yehoahazi isipokuwa wapanda farasi hamsini, magari kumi ya vita na askari wa miguu elfu kumi, kwa kuwa mfalme wa Aramu alikuwa amewaangamiza hao wengine na kuwafanya kama mavumbi wakati wa kupura nafaka.

8Matukio mengine ya utawala wa Yehoahazi yote aliyoyafanya na mafanikio yake, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli? 9Yehoahazi akalala pamoja na baba zake, akazikwa huko Samaria. Naye Yehoashi13:9 Yehoashi ni namna nyingine ya kutaja jina la Yoashi. mwanawe akawa mfalme baada yake.

Yehoashi Mfalme Wa Israeli

10Katika mwaka wa thelathini na saba wa utawala wa Yoashi mfalme wa Yuda, Yehoashi mwana wa Yehoahazi alianza kutawala Israeli huko Samaria, naye akatawala miaka kumi na sita. 11Alifanya maovu machoni pa Bwana, na hakuacha dhambi yoyote kati ya zile za Yeroboamu mwana wa Nebati ambazo alikuwa amesababisha Israeli kuzitenda, bali aliendelea kuzitenda.

1213:12 2Fal 14:15Na kwa matukio mengine ya utawala wa Yehoashi, yote aliyoyafanya na mafanikio yake, pamoja na vita yake dhidi ya Amazia mfalme wa Yuda, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli? 1313:13 2Fal 14:23; Hos 1:1Yehoashi akalala pamoja na baba zake, akazikwa Samaria pamoja na wafalme wa Israeli. Yeroboamu akawa mfalme baada yake.

1413:14 2Fal 2:12Wakati huu, Elisha alikuwa anaumwa na ugonjwa ambao baadaye ulimuua. Yehoashi mfalme wa Israeli akashuka kwenda kumwona na kumlilia. Akalia, “Baba yangu! Baba yangu! Magari ya vita ya Israeli na wapanda farasi wake!”

15Elisha akasema, “Leta upinde na baadhi ya mishale,” naye mfalme akafanya hivyo. 16Elisha akamwambia mfalme wa Israeli, “Shika upinde mikononi mwako.” Alipokwisha kuichukua, Elisha akaweka mikono yake juu ya mikono ya mfalme.

1713:17 Yos 8:18; 1Fal 20:26Elisha akasema, “Fungua dirisha la mashariki,” naye akalifungua. Elisha akasema, “Piga mshale!” Naye akapiga mshale. Elisha akasema, “Mshale wa ushindi wa Bwana, mshale wa ushindi juu ya Aramu! Utawaangamiza Waaramu kabisa huko Afeki.” 18Kisha akasema, “Chukua mishale,” naye mfalme akaichukua. Elisha akamwambia, “Piga ardhi kwa hiyo mishale.” Akaipiga mara tatu, halafu akaacha.

1913:19 2Fal 13:25Mtu wa Mungu akamkasirikia na akasema, “Ungepiga chini mara tano au sita, ndipo ungeishinda Aramu na kuiangamiza kabisa. Lakini sasa utaishinda mara tatu tu.”

2013:20 2Fal 5:2Elisha akafa, nao wakamzika.

Vikosi vya Wamoabu vilikuwa vinashambulia nchi kwa vita kila mwaka wakati wa vuli. 2113:21 Mt 27:52Ikawa Waisraeli fulani walipokuwa wanamzika mtu, ghafula wakaona kikosi cha washambuliaji, basi wakaitupa ile maiti ya yule mtu ndani ya kaburi la Elisha. Wakati ile maiti ilipogusa mifupa ya Elisha, yule mtu akafufuka na kusimama kwa miguu yake.

2213:22 1Fal 19:17Hazaeli mfalme wa Aramu aliwatesa Israeli wakati wote wa utawala wa Yehoahazi. 2313:23 Kut 2:24; Kum 29:20Lakini Bwana akawarehemu na akawahurumia, akaonyesha kujishughulisha nao kwa sababu ya Agano lake na Abrahamu, Isaki na Yakobo. Hadi leo, hajawaangamiza wala kuwafukuza mbele zake.

2413:24 2Fal 13:3Hazaeli mfalme wa Shamu akafa, naye Ben-Hadadi mwanawe akawa mfalme baada yake. 2513:25 2Fal 10:32Kisha Yehoashi mwana wa Yehoahazi akateka tena kutoka kwa Ben-Hadadi mwana wa Hazaeli ile miji aliyokuwa ameitwaa kwa vita kutoka kwa baba yake Yehoahazi. Yehoashi alimshinda mara tatu, hivyo akaweza kuiteka tena ile miji ya Waisraeli.

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

列王纪下 13:1-25

约哈斯做以色列王

1亚哈谢的儿子犹大约阿施执政第二十三年,耶户的儿子约哈斯撒玛利亚登基做以色列王,执政十七年。 2约哈斯做耶和华视为恶的事,重蹈尼八的儿子耶罗波安的覆辙,使以色列人陷入罪中。他始终没有离开那些罪。 3因此,耶和华向以色列人发怒,屡次使他们败在亚兰哈薛和他儿子便·哈达手中。 4约哈斯求耶和华开恩,耶和华看见亚兰王非常残暴地欺压以色列人,便垂听他的祷告, 5赐给以色列人一位拯救者,从亚兰人手中救了他们。他们便像从前一样安居乐业。 6但他们一如既往地犯罪,没有离开耶罗波安家使以色列人犯的那些罪,在撒玛利亚仍然保留着亚舍拉神像。 7亚兰王摧毁了约哈斯的军队,把他们像麦场的尘土一样践踏。约哈斯只剩下五十名骑兵、十辆战车和一万步兵。 8约哈斯其他的事及一切所为和功业都记在《以色列列王史》上。 9约哈斯与祖先同眠后,葬在撒玛利亚。他儿子约阿施继位。

约阿施做以色列王

10犹大约阿施执政第三十七年,约哈斯的儿子约阿施撒玛利亚登基做以色列王,执政十六年。 11他做耶和华视为恶的事,一如既往地犯罪,没有离开尼八的儿子耶罗波安使以色列人犯的那些罪。 12约阿施其他的事及一切所为和功业,包括他英勇对抗犹大亚玛谢的事迹都记在《以色列列王史》上。 13约阿施与祖先同眠后,葬在撒玛利亚以色列王陵。耶罗波安二世继位。

以利沙病逝

14以利沙患了不治之症,以色列约阿施前去探望,伏在他身上哭喊道:“我父啊!我父啊!以色列的战车和骑兵啊!” 15以利沙对王说:“取弓箭来。”王便取来弓箭。 16以利沙以色列王拉开弓,王照做了。以利沙双手按着王的手, 17说:“打开朝东的窗户。”王便打开窗户。以利沙说:“射箭!”王便射箭。以利沙说:“这是耶和华的得胜之箭,是战胜亚兰人的箭。你会在亚弗彻底消灭亚兰人。” 18以利沙说:“拿几枝箭来。”王便取来箭。以利沙说:“用箭击打地!”王击打了三下就停下来。 19上帝的仆人很生气,说:“你应该击打五六下,那样你就可以彻底消灭亚兰人。现在,你只能击败他们三次。” 20以利沙去世后,人们埋葬了他。

每年春天摩押人都来犯境。 21一天,一些以色列人正安葬死人,忽然看见一群摩押入侵者,便连忙把尸体抛进以利沙的坟墓里。那死人碰到以利沙的骸骨,就复活了,并站了起来。

以色列与亚兰交战

22约哈斯执政期间,亚兰哈薛一直压迫以色列人。 23耶和华因为与亚伯拉罕以撒雅各所立的约,就恩待以色列人,怜悯、眷顾他们,至今仍不愿灭绝他们,没有把他们从自己面前赶走。 24亚兰哈薛死后,他儿子便·哈达继位。 25约阿施三次击败便·哈达,收回了他父亲约哈斯哈薛交战时失去的以色列城邑。