2 Wafalme 1 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

2 Wafalme 1:1-18

Hukumu Ya Bwana Juu Ya Ahazia

11:1 Mwa 19:37; 2Sam 8:2; 2Fal 3:5Baada ya kifo cha Mfalme Ahabu, nchi ya Moabu iliasi dhidi ya Israeli. 21:2 Amu 18:5; 2Fal 1:16; 8:7-10; Mt 10:25; Isa 14:29; Mk 3:22; 1Sam 5:10Basi Ahazia alikuwa ameanguka huko Samaria kutoka baraza ya chumba chake cha juu, akaumia. Hivyo akatuma wajumbe, akiwaambia, “Nendeni mkaulize kwa Baal-Zebubu, mungu wa Ekroni, mkaone kama nitapona kutokana na kuumia huku.”

31:3 Mwa 16:7; 1Sam 28:8; Isa 8:19; Yer 2:10-13; Yon 2:8Lakini malaika wa Bwana akamwambia Eliya, Mtishbi, “Panda ukakutane na wajumbe wa mfalme wa Samaria, uwaulize, ‘Je, ni kwa sababu hakuna Mungu katika Israeli ndiyo maana mnakwenda kumuuliza Baal-Zebubu, mungu wa Ekroni?’ 41:4 2Fal 1:6, 16; Za 41:8; Rum 6:23; Mhu 8:13; Mit 11:19; Isa 3:11; Yak 1:15Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana, ‘Hutaondoka kwenye kitanda unachokilalia. Hakika utakufa!’ ” Hivyo Eliya akaenda.

5Wajumbe waliporudi kwa mfalme, akawauliza, “Kwa nini mmerudi?”

61:6 2Fal 1:2; Mit 14:32Wakamjibu, “Mtu fulani alikuja kukutana nasi, naye akatuambia, ‘Rudini kwa mfalme aliyewatuma na mkamwambie, “Hili ndilo asemalo Bwana: Je, ni kwa sababu hakuna Mungu katika Israeli ndiyo maana unawatuma watu kwenda kuuliza kwa Baal-Zebubu, mungu wa Ekroni? Kwa hiyo hutaondoka kwenye kitanda unachokilalia. Hakika utakufa!” ’ ”

7Mfalme akawauliza, “Alikuwa mtu wa namna gani ambaye mlikutana naye, akawaambia hili?”

81:8 Isa 3:3; Zek 13:4; Mt 3:4Wakamjibu, “Alikuwa mtu aliyekuwa na vazi la manyoya na mkanda wa ngozi kiunoni mwake.”

Mfalme akasema, “Huyo alikuwa ni Eliya, Mtishbi.”

91:9 Kut 18:25; 2Fal 6:14; Za 105:15; Amo 7:12; Mt 27:29Ndipo mfalme akamtuma mkuu mmoja wa kikosi pamoja na kikosi chake cha askari hamsini kwa nabii Eliya. Yule mkuu wa kikosi akamwendea Eliya, aliyekuwa ameketi juu ya kilima, na kumwambia, “Mtu wa Mungu, mfalme anasema, ‘Shuka chini!’ ”

101:10 Hes 11:1; 1Fal 18:38; Lk 9:54; Ufu 11:5Eliya akamjibu yule mkuu wa kikosi, “Ikiwa mimi ni mtu wa Mungu, moto na ushuke kutoka mbinguni ukuteketeze wewe na watu wako hamsini!” Ndipo moto ukashuka kutoka mbinguni na kuwateketeza yule mkuu wa kikosi pamoja na watu wake.

111:11 Isa 26:11Aliposikia hili, mfalme akatuma kwa Eliya mkuu wa kikosi mwingine na askari wake hamsini. Yule mkuu wa kikosi akamwambia Eliya, “Mtu wa Mungu, hili ndilo asemalo mfalme, ‘Shuka chini mara moja!’ ”

12Eliya akajibu, “Ikiwa mimi ni mtu wa Mungu, moto na ushuke kutoka mbinguni ukuteketeze wewe na watu wako hamsini!” Ndipo moto wa Mungu ukashuka kutoka mbinguni, ukamteketeza yeye na watu wake hamsini.

131:13 1Sam 26:21; Za 72:14; Mit 22:27; Mhu 9:3; Yer 5:3Hivyo mfalme akatuma mkuu wa kikosi wa tatu na watu wake hamsini. Huyu mkuu wa kikosi wa tatu akapanda na kupiga magoti mbele ya Eliya, akiomba, “Mtu wa Mungu, tafadhali niachie uhai wangu na uhai wa hawa watu hamsini, watumishi wako! 14Tazama, moto umeshuka kutoka mbinguni na kuwateketeza wale wakuu wa vikosi viwili vya kwanza pamoja na watu wao. Lakini sasa niachie uhai wangu!”

151:15 2Fal 1:3; Isa 57:11-12; Yer 1:17; Eze 2:6Malaika wa Bwana akamwambia Eliya, “Shuka pamoja naye, usimwogope.” Hivyo Eliya akainuka na kushuka pamoja naye kwa mfalme.

16Akamwambia mfalme, “Hili ndilo asemalo Bwana: Je, ni kwa sababu hakuna Mungu katika Israeli wa kumuuliza habari, ndiyo maana ukatuma wajumbe kuuliza Baal-Zebubu, mungu wa Ekroni? Kwa sababu umefanya hili, kamwe hutaondoka kwenye kitanda unachokilalia. Hakika utakufa!” 171:17 2Fal 8:15-16; Yer 20:6; 28:17Hivyo akafa, sawasawa na lile neno la Bwana ambalo Eliya alikuwa amesema.

Kwa kuwa Ahazia hakuwa na mwana, Yoramu1:17 Yoramu ni namna nyingine ya kutaja jina Yehoramu. akawa mfalme baada yake katika mwaka wa pili wa Yehoramu mwana wa Yehoshafati mfalme wa Yuda. 18Kwa matukio mengine ya utawala wa Ahazia na yale aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli?