2 Timotheo 3 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

2 Timotheo 3:1-17

Hatari Za Siku Za Mwisho

13:1 1Tim 4:1; 2Pet 3:3; 2Tim 4:3; 1Yn 2:18; Yud 18Lakini yakupasa ufahamu jambo hili, kwamba siku za mwisho kutakuwa na nyakati za hatari. 23:2 1Tim 3:3; Rum 1:30Kwa maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kumkufuru Mungu, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio watakatifu, 33:3 Rum 1:31; 2Pet 3:3wasio na upendo, wasiopenda kupatanishwa, wasingiziaji, wasiozuia tamaa zao, wakatili, wasiopenda mema, 43:4 1Tim 3:6; 2Pet 2:10; Flp 3:19; 2Pet 2:13; Yud 4, 9wasaliti, wakaidi, waliojaa majivuno, wapendao anasa zaidi kuliko kumpenda Mungu: 53:5 1Tim 5:8; Tit 1:16; 2The 3:6; 1Tim 6:5wakiwa na mfano wa utauwa kwa nje, lakini wakizikana nguvu za Mungu. Jiepushe na watu wa namna hiyo.

63:6 Yud 4; Mt 23:14; Tit 1:11Miongoni mwao wamo wale wajiingizao katika nyumba za watu na kuwachukua mateka wanawake wajinga, waliolemewa na dhambi zao na kuyumbishwa na aina zote za tamaa mbaya. 73:7 1Tim 2:4; 2Tim 1:11Wakijifunza siku zote lakini kamwe wasiweze kufikia ujuzi wa kweli. 83:8 Kut 7:11; Mdo 13:8; 1Tim 6:5Kama vile Yane na Yambre walivyopingana na Mose, vivyo hivyo watu hawa hupingana na ile kweli. Hawa ni watu wenye akili zilizopotoka, ambao wamekataliwa kwa mambo ya imani. 93:9 Kut 8:18; 9:11; 7:12Lakini hawataendelea sana, kwa sababu upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote, kama ulivyokuwa dhahiri upumbavu wa hao watu wawili.

Paulo Amwagiza Timotheo

103:10 1Tim 4:6; Flp 2:22Lakini wewe umeyajua mafundisho yangu, mwenendo, makusudi, imani, uvumilivu, upendo, ustahimilivu, 113:11 Mdo 13:14, 50; 2Kor 11:23-27; Za 34:19mateso na taabu, yaani mambo yote yaliyonipata huko Antiokia, Ikonio na Listra, mateso yote niliyostahimili, lakini Bwana aliniokoa katika hayo yote. 123:12 Mdo 14:22; Za 34:19; Mdo 14:22; Mt 16:24; Yos 17:14; 1Kor 15:19Naam, yeyote anayetaka kuishi maisha ya utauwa ndani ya Kristo Yesu atateswa. 133:13 2Tim 2:16; 2The 2:11; 1Tim 4:1Lakini watu waovu na wadanganyaji watazidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika. 143:14 2Tim 1:13; 2:2Bali wewe, udumu katika yale uliyojifunza na kuyaamini kwa uthabiti, ukitambua ya kuwa ulijifunza hayo kutoka kwa nani, 153:15 Yn 5:39; Za 119:98-99na jinsi ambavyo tangu utoto umeyajua Maandiko matakatifu, ambayo yanaweza kukuhekimisha upate wokovu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu. 163:16 2Pet 1:20-21; Rum 4:23-24Kila Andiko limevuviwa na Mungu na lafaa kwa mafundisho, kwa kuwaonya watu makosa yao, kwa kuwaongoza na kwa kuwafundisha katika haki, 173:17 1Tim 6:11; 2Tim 2:21ili mtu wa Mungu awe amekamilishwa, apate kutenda kila kazi njema.