2 Timotheo 1 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

2 Timotheo 1:1-18

11:1 1Tim 6:19; Tit 1:2; 1Kor 1:1; Efe 3:6; Ebr 9:15Paulo mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, kulingana na ile ahadi ya uzima uliomo ndani ya Kristo Yesu.

21:2 Mdo 16:1; 1Tim 1:2Kwa Timotheo, mwanangu mpendwa:

Neema, rehema na amani itokayo kwa Mungu Baba, na kwa Kristo Yesu Bwana wetu.

Shukrani Na Kutiwa Moyo

31:3 Rum 1:10; Efe 1:16; Mdo 22:3; 23:1; 24:14; 27:23; Gal 1:14Ninamshukuru Mungu, ninayemtumikia kwa dhamiri safi, kama walivyofanya baba zangu, ninapokukumbuka usiku na mchana katika maombi yangu. 41:4 Mdo 20:37; 2Tim 4:9; 4:21Nikiyakumbuka machozi yako, ninatamani sana kukuona ili nipate kujawa na furaha. 51:5 1Tim 1:5; 2Tim 3:15Nimekuwa nikiikumbuka imani yako ya kweli, waliokuwa nayo bibi yako Loisi na mama yako Eunike na ambayo mimi ninasadiki sasa wewe pia unayo. 61:6 Mdo 6:6; 1The 5:19; 1Tim 4:14Kwa sababu hii nakukumbusha uchochee ile karama ya Mungu, iliyowekwa ndani yako nilipokuwekea mikono yangu. 71:7 Yer 42:11; Rum 8:15; Lk 24:49; Mdo 1:8Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali roho ya nguvu, ya upendo na ya moyo wa kiasi.

81:8 Rum 1:16; Efe 3:1; 2Tim 2:3-9; 4:5Kwa hiyo usione haya kushuhudia kuhusu Bwana wetu, wala usinionee haya mimi niliye mfungwa kwa ajili yake. Bali uishiriki pamoja nami taabu ya Injili, kwa kadiri ya nguvu ya Mungu, 91:9 Rum 8:28; 1Tim 1:1; Tit 3:4; 1The 4:7; Ebr 3:1; Rum 3:20; 9:11; Tit 3:5ambaye alituokoa na kutuita katika mwito mtakatifu: si kwa kadiri ya matendo yetu mema bali kwa sababu ya kusudi lake mwenyewe na neema yake. Neema hii tulipewa katika Kristo Yesu tangu milele. 101:10 Efe 1:9; 1Kor 15:26, 54; Rum 16:26; Kol 1:26; Tit 1:3; 1Pet 1:20; Ebr 2:14Lakini sasa imefunuliwa kwa kudhihirishwa kwake Mwokozi wetu, Kristo Yesu, ambaye amebatilisha mauti na kuleta uzima na kutokufa kwa njia ya Injili. 111:11 1Tim 2:7; Mdo 9:15; Efe 3:7, 8; 2Tim 4:17Nami nimewekwa kuwa mhubiri, mtume na mwalimu wa Injili hii. 121:12 1Tim 6:20; 1Kor 1:8; Efe 3:1; 2Tim 2:9; 1Pet 4:19; 1Tim 6:20; 2Tim 4:8Hii ndiyo sababu ninateseka namna hii, lakini sioni haya kwa maana ninamjua yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kuwa anaweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hadi siku ile.

131:13 Tit 1:9; 1Tim 1:14Shika kwa uthabiti kielelezo cha mafundisho yenye uzima yale uliyoyasikia kwangu, pamoja na imani na upendo katika Kristo Yesu. 141:14 Rum 8:9; 1Tim 6:20; Rum 8:11Ilinde ile amana uliyokabidhiwa kwa Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu.

151:15 2Tim 4:10-16, 19; Mdo 19:10Unajua ya kuwa watu wote katika Asia wameniacha, miongoni mwao wamo Filego na Hermogene.

161:16 Mt 5:7; 2Tim 4:19; Flm 7; Mdo 28:20Bwana akawahurumie watu wa nyumbani mwa Onesiforo, kwa sababu aliniburudisha mara kwa mara wala hakuionea aibu minyororo yangu. 17Badala yake, alipokuwa Rumi, alinitafuta kwa bidii mpaka akanipata. 181:18 Ebr 6:10; Mt 25:34-40; 2The 1:10; 1Tim 1:18Bwana na amjalie kupata rehema zake siku ile! Nawe unajua vyema jinsi alivyonisaidia huko Efeso.