2 Samweli 8 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

2 Samweli 8:1-18

Ushindi Wa Daudi

(1 Nyakati 18:1-17)

18:1 2Sam 7:9; 21:15-22; 1Nya 18:1Baada ya muda, Daudi akawashinda Wafilisti na kuwatiisha, naye akautwaa Metheg-Amma kutoka mikononi mwa Wafilisti.

28:2 Mwa 19:37; Hes 21:29; Amu 3:15; Isa 45:14; Hes 24:17; 1Sam 14:47; Za 50:8; 72:10Pia Daudi akawashinda Wamoabu. Akawafanya walale chini kwa mstari akawapima kwa urefu wa kamba. Kila alipopima urefu wa hiyo kamba mara mbili hilo kundi waliuawa na alipopima mara ya tatu aliwaacha hai. Kwa hiyo Wamoabu wakawa chini ya Daudi nao wakamletea kodi.

38:3 2Sam 10:16; 1Fal 11:23; 1Sam 14:47; Mwa 2:14; 15:18Zaidi ya hayo, Daudi akapigana na Hadadezeri mwana wa Rehobu, mfalme wa Soba, alipokwenda kurudisha tena utawala wake kwenye eneo la Mto Frati. 48:4 Mwa 49:6; Yos 11:9Daudi akateka magari yake ya vita 1,000, askari wapanda farasi 7,000 na askari 20,000 watembeao kwa miguu. Daudi akawakata wale farasi wote wakokotao magari mishipa ya miguu, isipokuwa farasi 100 hakuwakata.

58:5 Mwa 14:15; 2Sam 10:6; 1Fal 11:24; 2Fal 8:7; 14:28Waaramu wa Dameski walipokuja kumsaidia Hadadezeri mfalme wa Soba, Daudi akawashambulia na kuwaua 22,000 miongoni mwao. 68:6 1Fal 20:34; 2Fal 10:19; 2Sam 3:18Daudi akaweka askari walinzi katika ufalme wa Waaramu huko Dameski, nao Waaramu wakawa watumwa wake na kumlipa ushuru. Bwana akampa Daudi ushindi kote alipokwenda.

78:7 1Fal 10:16; 14:26; 2Fal 11:10Daudi akazitwaa ngao za dhahabu zilizokuwa za maafisa wa Hadadezeri na kuzileta Yerusalemu. 88:8 Eze 47:16Kutoka miji ya Beta8:8 Beta ulikuwa mji wa Aramu-Soba ambao uliitwa Teba kwa Kiaramu; pia uliitwa Tibhathi (1Nya 18:8). na Berothai, iliyokuwa miji ya Hadadezeri, Mfalme Daudi akatwaa shaba nyingi sana.

98:9 1Fal 8:65; 2Fal 14:28; 2Nya 8:4; Lk 14:31-32Tou, mfalme wa Hamathi, aliposikia kwamba Daudi amelishinda jeshi lote la Hadadezeri, 10akamtuma mwanawe Yoramu kwa Mfalme Daudi kumsalimu na kumpongeza kwa ushindi wake katika vita dhidi ya Hadadezeri, kwa kuwa Hadadezeri alikuwa amepigana vita na Tou. Yoramu akamletea Daudi vyombo vya fedha, dhahabu na shaba.

118:11 1Fal 7:51; 15:15; 1Nya 26:26; 2Nya 5:1; 1Nya 18:11; 22:14-16; Mik 4:13; Ufu 21:24Mfalme Daudi akaviweka vifaa hivi wakfu kwa Bwana, kama vile alivyokuwa amefanya kwa fedha na dhahabu kutoka kwa mataifa yote aliyokuwa ameyashinda: 128:12 2Sam 10:14; 5:25; Hes 24:20; 1Sam 27:8yaani Edomu, Moabu, Waamoni, Wafilisti na Waamaleki. Pia akaweka wakfu nyara alizoteka kutoka kwa Hadadezeri mwana wa Rehobu, mfalme wa Soba.

138:13 2Sam 7:9; 2Fal 14:7; 1Nya 18:12; Za 60Naye Daudi akapata sifa baada ya kurudi kutoka kuwaua Waedomu 18,000 katika Bonde la Chumvi.

148:14 Hes 24:17-18; Za 108:9; Isa 34:5; 63:1; Yer 49:7; Eze 25:12; Mwa 27:29, 37-40; Za 144:10; 2Sam 22:44; Za 18:43Akaweka kambi za askari walinzi katika Edomu yote, nao Waedomu wakawa chini ya Daudi. Bwana alimpatia Daudi ushindi kila alipokwenda.

Maafisa Wa Daudi

158:15 Mwa 18:19; 1Fal 11:18; 14:8; 15:11; 22:43; 2Fal 12:2; Ay 29:14; Za 5:12; 119:121; Ebr 11:33Daudi akatawala Israeli yote, akitenda lililo haki na sawa kwa watu wake wote. 168:16 2Sam 2:13; 20:24; 1Fal 4:3; Isa 36:3, 22; 2Sam 19:13Yoabu mwana wa Seruya alikuwa jemadari wa jeshi; Yehoshafati mwana wa Ahiludi alikuwa mweka kumbukumbu; 178:17 1Sam 2:35; 15:24, 29; 2Sam 20:25; 1Fal 1:8; 4:4; 1Nya 6:8, 53; 16:39; 24:3; 27:17; 2Nya 13:10; Eze 40:46; 43:19; 44:15; 48:11; Mk 2:26; 1Fal 4:3; 2Fal 12:10; 19:2; 22:3; Isa 36:3; Yer 36:12Sadoki mwana wa Ahitubu na Ahimeleki mwana wa Abiathari walikuwa makuhani; Seraya alikuwa mwandishi; 188:18 2Sam 20:23; 23:20; 1Fal 1:8; 2:25, 35, 46; 4:4; 1Sam 30:14; 1Nya 18:17Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa msimamizi wa Wakerethi na Wapelethi; nao wana wa Daudi walikuwa washauri wa mfalme.