2 Samweli 7 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version

2 Samweli 7:1-29

Ahadi Ya Mungu Kwa Daudi

(1 Nyakati 17:1-15)

17:1 1Nya 22:18; 17:1; 2Sam 6:3; Dan 4:29-30Baada ya mfalme kuingia rasmi katika jumba lake la kifalme, naye Bwana akiwa amemstarehesha pande zote mbali na adui zake, 27:2 2Sam 12:1; 1Fal 1:8, 22; 1Nya 29:29; 2Nya 9:29; 2Sam 5:11; 1Fal 3:1; 7:1-7; 9:1; 2Nya 8:1; Yer 22:14; Hag 1:4; Kut 26:1; Za 132:3; Mdo 7:45-46; Kut 40:21akamwambia nabii Nathani, “Mimi hapa, ninaishi katika jumba la kifalme la mierezi, wakati Sanduku la Mungu limebaki katika hema.”

37:3 1Sam 10:7; Za 132:1-5; 1Fal 8:17; 1Nya 22:7; 28:2Nathani akamjibu mfalme, “Lolote ulilo nalo moyoni, endelea ukalifanye, kwa maana Bwana yu pamoja nawe.”

4Usiku ule neno la Bwana likamjia Nathani, kusema:

57:5 1Fal 8:19; 1Nya 22:8; 1Fal 5:3-5; 1Nya 28:3“Nenda ukamwambie mtumishi wangu Daudi, ‘Hili ndilo asemalo Bwana: Je, ewe ndiwe wa kunijengea mimi nyumba ili nikae ndani yake? 67:6 Mdo 7:45; Kut 40:18, 34; Yos 18:1; 1Fal 8:16Sijakaa ndani ya nyumba tangu siku niliyowaleta Waisraeli kutoka Misri hadi leo. Nimekuwa nikitembea kutoka mahali pamoja hadi mahali pengine ndani ya hema kama makao yangu. 77:7 Kum 23:14; 2Sam 5:2; 1Fal 8:27; Isa 66:1; Law 26:11; Za 78:72; Eze 34:2, 15, 23; Mt 2:6; Mdo 20:28; 1Pet 5:2Popote nilipotembea pamoja na Waisraeli wote, je, nimewahi kumwambia kiongozi wao yeyote niliyemwamuru kuwachunga watu wangu Israeli, “Kwa nini hujanijengea nyumba ya mierezi?” ’

87:8 1Sam 16:11; 1Nya 21:17; Za 74:1; Amo 7:15; Isa 9:16; 16:1; 2Sam 6:21; Za 78:70-72; 2Kor 6:18“Sasa basi, mwambie mtumishi wangu Daudi, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: Nilikutoa wewe kutoka machungani na kutoka kuandama kundi la kondoo na mbuzi ili kuwaongoza watu wangu Israeli. 97:9 1Sam 18:14; 2Sam 5:10; Za 18:37-42; Kut 11:3; Mwa 12:2; 1Nya 17:8; Lk 1:52Nimekuwa pamoja nawe popote ulipokwenda, nami nimekuondolea mbali adui zako wote mbele yako. Basi nitalifanya jina lako kuwa kuu kama majina ya watu walio wakuu sana duniani. 107:10 Kut 15:17; Isa 5:1-7; 2Fal 21:8; 2Nya 33:8; Za 89:22-23; 147:14; Isa 54:14; 60:18; Za 44:2; 80:8; Yer 24:6; Amo 9:15Nami nitawapatia watu wangu Israeli mahali niwapande humo ili kwamba wawe na nyumbani kwao wenyewe wasisumbuliwe tena. Watu waovu hawatawaonea tena, kama walivyofanya mwanzoni, 117:11 Amu 2:16; 1Sam 12:9-11; 1Fal 2:24; 1Sam 25:28; Za 89:35-37; Lk 1:32-33; Mdo 13:22-23; 2Tim 2:8; Kut 1:21; Isa 7:2na kama walivyofanya tangu mwanzo wakati nilipowaweka viongozi juu ya watu wangu Israeli. Pia nitawapa raha mbele ya adui zenu wote.

“ ‘Bwana akuambia kwamba Bwana mwenyewe atakujengea nyumba. 127:12 Mwa 15:15; 1Fal 2:1; Mdo 13:36; 1Fal 8:20; Za 132:11-12; Yer 30:21; 33:15; 2Nya 23:3Siku zako zitakapokwisha nawe ulale pamoja na baba zako, nitainua mzao wako aingie mahali pako, ambaye atatoka viunoni mwako, nami nitauimarisha ufalme wake. 137:13 Kum 12:5; 1Fal 5:5; 6:12; 8:19, 29; Kum 16:11; 2Fal 21:4, 7; Mit 25:5; Dan 7:27; Mwa 9; 16; 2Sam 22:51; 1Fal 2:4, 45; 1Nya 22; 10; 28:6; 2Nya 6:16; 7:18; 13:5; 21:7; Za 89:3-4; Isa 9:7; 16:5; Yer 17:25; 33:17-21Yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa ajili ya Jina langu, nami nitaimarisha kiti cha enzi cha ufalme wake milele. 147:14 Za 2:7; 89:26; Yer 3:19; Mt 3:17; Yn 1:49; 2Kor 6:18; Ebr 1:5; Ufu 21:7; Kum 8:5; 1Fal 11:34; 1Nya 22:10; Ebr 12:7; Za 89:30-33; Mit 13:24Nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu. Atakapokosea nitamwadhibu kwa fimbo ya wanadamu, kwa adhabu ya kupigwa na wanadamu. 157:15 1Fal 2:4; 6:12; 8:25; 9:5; 11:13; 2Fal 19:34; 2Nya 6:16; 7:18; 21:7; Za 89:34; Yer 33; 17; 1Sam 13:13; 15:28; 16:14; 7:16; Za 89:36-37; Lk 1:33; Za 9:7; 93:2; 103:19Lakini upendo wangu kamwe hautaondolewa kwake, kama nilivyouondoa kwa Sauli, niliyemwondoa atoke mbele yako. 16Nyumba yako na ufalme wako utadumu milele mbele zangu, kiti chako cha enzi kitafanywa imara milele.’ ”

17Nathani akamwarifu Daudi maneno yote ya maono haya.

Maombi Ya Daudi

(1 Nyakati 17:16-27)

187:18 Kut 3:11; 1Sam 18:18Ndipo Mfalme Daudi akaingia ndani, akaketi mbele za Bwana, akasema:

“Ee Bwana Mwenyezi, mimi ni nani, na jamaa yangu ni nini, hata umenileta mpaka hapa nilipo? 197:19 Isa 55:8-9Naam, kana kwamba hili halitoshi machoni pako, Ee Bwana Mwenyezi, wewe umenena pia kuhusu siku zijazo za nyumba ya mtumishi wako. Je, hii ndiyo njia yako ya kawaida ya kushughulika na mwanadamu, Ee Bwana Mwenyezi?

207:20 Isa 38:15; Yn 21:17; 1Sam 16:7; Mwa 18:19; Za 139:1“Je, Daudi aweza kukuambia nini zaidi? Kwa maana unamjua mtumishi wako, Ee Bwana Mwenyezi. 217:21 Efe 4:32Kwa ajili ya neno lako na kwa mapenzi yako, umefanya jambo hili kubwa na kulifanya lijulikane na lifahamike kwa mtumishi wako.

227:22 Za 48:1; 77; 13; 86:10; Yer 10:6; Kum 3:24; Kut 9:14; 8:10; 20:4; 10:2; Amu 6:13; 1Nya 16:25; 2Nya 2:5; Kum 4:35; Isa 45:5“Tazama jinsi ulivyo mkuu, Ee Bwana Mwenyezi! Hakuna mwingine kama wewe, wala hakuna Mungu ila wewe, kama vile tulivyosikia kwa masikio yetu wenyewe, 237:23 Kum 4:32-38; 33:29; 1Sam 12:22; Hes 6:27; Kum 10:21; 7:7-8; 9:29; 15:15; Za 147:20; Neh 1:10Naye ni nani aliye kama watu wako Israeli, taifa pekee duniani ambalo Mungu alitoka kwenda kulikomboa kwa ajili yake mwenyewe, na kujifanyia jina mwenyewe, kwa kufanya maajabu makubwa na ya kutisha kwa kuwafukuza mataifa na miungu yao mbele ya watu wako, ambao uliwakomboa kutoka Misri? 247:24 Kum 26:18; Kut 6:6-7; Za 48:14Umeimarisha watu wako Israeli hasa kama watu wako mwenyewe milele, nawe, Ee Bwana, umekuwa Mungu wao.

257:25 Hes 23:19; 2Nya 1:9“Basi sasa, Bwana, ukaitimize ahadi uliyosema kuhusu mtumishi wako na nyumba yake milele. Fanya kama ulivyoahidi, 267:26 Kut 6:3; Neh 9:5; Za 72:19; 96:8; Mt 6:9; 1Sam 25:28ili kwamba jina lako litukuke milele. Ndipo watu watasema, ‘Bwana Mwenye Nguvu Zote ni Mungu juu ya Israeli!’ Nayo nyumba ya mtumishi wako Daudi itakuwa imara mbele zako.

27“Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, umelifunua hili kwa mtumishi wako, ukisema, ‘Nitakujengea nyumba.’ Hivyo mtumishi wako amepata ujasiri kukuletea dua hii. 287:28 Kut 34:6; Yn 17:17Ee Bwana Mwenyezi, wewe ndiwe Mungu! Maneno yako ndiyo kweli, nawe umemwahidi mtumishi wako mambo haya mazuri. 297:29 Hes 6:23-27Sasa naomba uwe radhi kuibariki nyumba ya mtumishi wako, ili idumu mbele zako milele, kwa maana wewe, Ee Bwana Mwenyezi, umesema, na kwa baraka zako nyumba ya mtumishi wako itaendelea kubarikiwa milele.”

Chinese Contemporary Bible 2023 (Traditional)

撒母耳記下 7:1-29

上帝對大衛的應許

1大衛住在王宮裡,耶和華使他安享太平,不受四圍的仇敵侵擾。 2一天,王對拿單先知說:「你看,我住在香柏木建的王宮中,上帝的約櫃卻還在帳幕裡。」 3拿單答道:「你有什麼想法,就去做吧,因為耶和華與你同在。」 4當晚耶和華對拿單說: 5「你去告訴我的僕人大衛,『耶和華說,你要建造殿宇給我居住嗎? 6從我把以色列人帶出埃及那天起,直到今天,我從未住過殿宇,一路上都住在帳幕裡。 7在我與以色列人同行的日子,我從未責問任何我委派牧養我子民的士師,你為何不為我建香柏木的殿宇呢?』

8「現在你要告訴我的僕人大衛,萬軍之耶和華說,『你原本在草場牧羊,我召你來做我以色列子民的首領。 9無論你去哪裡,我都與你同在,為你剷除所有仇敵。現在我要使你聲名遠揚,與世上的偉人齊名。 10-11我必為我的以色列子民預備一個地方,栽培他們,使他們住在自己的家園,不再受驚擾,不會像從前我設立士師治理他們的時候那樣受惡人壓迫。我必使你安定,免受仇敵的侵擾。我耶和華向你宣告,我必為你建立王朝。 12你離世與祖先同眠時,我必興起你親生的後裔接替你,使他的國穩固。 13他必為我的名建造殿宇,我必使他的國度王位永固。 14我要作他的父親,他要作我的兒子。如果他犯了罪,我必用人的杖、世人的鞭子來懲治他, 15我的慈愛曾離開從你面前被廢的掃羅,但我的慈愛必不離開他。 16你的家和你的國必在我面前永遠堅立,你的王位必永遠穩固。』」

17拿單就把所聽到的啟示全部告訴大衛

大衛的禱告

18於是,大衛王進去,在耶和華面前坐下,說:「主耶和華啊,我是誰?我的家算什麼?你竟這樣厚待我。 19主耶和華啊,在你眼中這還不夠,你還說到僕人家的將來。主耶和華啊,你竟這樣恩待世人! 20主耶和華啊,大衛還能對你說什麼呢?因為你深知你的僕人。 21你讓僕人知道你憑自己的應許、按自己的心意成就這大事。 22主耶和華啊,你真偉大!我們從未聽過有誰能與你相比,你是獨一無二的上帝。 23世上哪個民族比得上你的以色列子民呢?你從埃及救贖他們,讓他們做你的子民,又彰顯你的大名,行偉大而可畏的事,把列國及其神明從你的以色列子民面前趕走。 24你讓以色列人永遠做你的子民,你耶和華做他們的上帝。

25「耶和華上帝啊,求你永遠信守你對僕人和僕人家的應許,求你成就你的應許。 26這樣,你的名必永遠被尊崇,人們必說,『萬軍之耶和華是以色列的上帝。』你僕人大衛的家必在你面前堅立。 27以色列的上帝——萬軍之耶和華啊,因為你曾啟示僕人,說要為僕人建立王朝,僕人才敢這樣向你祈禱。 28主耶和華啊,唯有你是上帝,你的話真實可靠,你給了僕人美好的應許。 29現在求你賜福給僕人家,使僕人家在你面前永續不斷。主耶和華啊,這些都是你的應許,願你永遠賜福給僕人家。」