2 Samweli 23 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

2 Samweli 23:1-39

Maneno Ya Mwisho Ya Daudi

123:1 Kut 11:3; Za 78:70-71; 89:27; 1Sam 2:10, 35; Za 18:50; 20:6; 84:9; Isa 45:1; Hab 3:13; 1Sam 16:12-13Haya ni maneno ya mwisho ya Daudi:

“Neno la Daudi mwana wa Yese,

neno la mtu aliyeinuliwa na Aliye Juu Sana,

mtu aliyepakwa mafuta na Mungu wa Yakobo,

mwimbaji wa nyimbo wa Israeli:

223:2 Mt 22:43; Mk 12:36; 2Pet 1:21“Roho wa Bwana alinena kupitia kwangu,

neno lake lilikuwa ulimini mwangu.

323:3 Kum 32:4; 1Sam 2:2; Za 18:31; 72:3; Mwa 42:18; Isa 11:1-5; 2Nya 19:7-9; Kut 18:21Mungu wa Israeli alinena,

mwamba wa Israeli akaniambia:

‘Mtu anatawala watu kwa haki,

wakati anapotawala

akiwa na hofu ya Mungu,

423:4 Yon 1:5; Za 119:147; 130:6; Mit 4:18; Amu 5:31; Mt 13:43; Kum 32:2yeye ni kama mwanga wa asubuhi jua lichomozapo

asubuhi isiyo na mawingu,

kama mwanga baada ya mvua

uchipuzao majani kutoka ardhini.’

523:5 Mwa 9:16; Za 89:29; Isa 55:3“Je, si hivyo ilivyo nyumba yangu

mbele za Mungu?

Je, hajafanya Agano la milele nami,

lililopangwa na kuimarishwa

kila sehemu?

Je, hatanifanya niufurahie wokovu wangu

na kunijalia matakwa yangu yote?

623:6 Isa 5:6; 9:18; 10:17; 27:4; 33:12; Mik 7:4; Nah 1:10; Mt 13:40-41Lakini watu waovu wote

watatupwa kando kama miiba,

ambayo haikusanywi kwa mkono.

7Yeyote agusaye miiba

hutumia chombo cha chuma

au mpini wa mkuki,

nayo huchomwa pale ilipo.”

Mashujaa Wa Daudi

(1 Nyakati 11:10-41)

823:8 2Sam 17:10; 1Nya 27:2Haya ndiyo majina ya mashujaa wa Daudi:

Yosheb-Bashebethi,23:8 Yosheb-Bashebethi au Yashobeamu (1Nya 11:11). Mtahkemoni, alikuwa kiongozi wa wale Watatu; yeye aliinua mkuki wake dhidi ya watu 800, ambao aliwaua katika pambano moja.

923:9 1Nya 27:4; 8:4; 11:12Wa pili wake alikuwa Eleazari mwana wa Dodai,23:9 Dodai tafsiri nyingine zinamwita Dodo. Mwahohi. Akiwa mmojawapo wa wale mashujaa watatu, alikuwa pamoja na Daudi wakati waliwadhihaki Wafilisti waliokuwa wamekusanyika huko Pas-Damimu kwa ajili ya vita. Kisha watu wa Israeli wakarudi nyuma, 10lakini yeye alisimama imara akawaua Wafilisti hadi mkono wake ukachoka na ukagandamana na upanga. Bwana akawapa ushindi mkubwa siku ile. Vikosi vikarudi kwa Eleazari, kuteka tu nyara za waliokufa.

11Aliyefuata alikuwa Shama mwana wa Agee, Mharari. Wafilisti walipokusanyika pamoja mahali palipokuwa shamba lililojaa dengu, vikosi vya Israeli viliwakimbia. 12Lakini Shama akasimama imara katikati ya lile shamba. Akalitetea na kuwaua Wafilisti, naye Bwana akawapa ushindi mkubwa.

1323:13 Mwa 38:1; Yos 12:15; 17:18; 1Sam 22:1; 2Sam 5:18; 1Nya 11:15; 14:9; Kum 33:29; 1Nya 29:11; 2Nya 11:14; 25:8; Za 3:8; 46:1; Rum 8:31; Isa 17:5Wakati wa mavuno, viongozi watatu kati ya viongozi thelathini walishuka, wakamwendea Daudi katika pango la Adulamu, wakati kikundi cha Wafilisti kilikuwa kimepiga kambi katika Bonde la Warefai. 1423:14 1Sam 22:4-5; 2Sam 5:17; Rut 1:19; 1Nya 12:16Wakati huo Daudi alikuwa katika ngome, na kambi ya Wafilisti ilikuwa huko Bethlehemu. 15Daudi akatamani maji, akasema, “Laiti mtu angenipatia maji ya kunywa kutoka kisima kilicho karibu na lango la Bethlehemu!” 1623:16 Mwa 35:14Basi mashujaa hao watatu wakapenya katikati ya Wafilisti, wakaenda kuchota maji kutoka kwa kisima kilicho karibu na lango la Bethlehemu, wakamletea Daudi. Lakini Daudi akakataa kuyanywa. Badala yake, aliyamimina mbele za Bwana. 1723:17 Law 17:10-1223:17 Law 17:10Akasema, “Iwe mbali nami, Ee Bwana, kufanya kitu hiki. Je, hii si damu ya watu ambao walikwenda kwa kuhatarisha maisha yao?” Naye Daudi hakuyanywa.

Haya yalifanywa na hao mashujaa watatu.

1823:18 1Sam 26:6; 1Nya 11:20; 2Sam 2:18Abishai ndugu yake Yoabu mwana wa Seruya ndiye alikuwa kiongozi wa hao Watatu. Aliinua mkuki wake dhidi ya watu 300 ambao aliwaua, kwa hiyo naye akawa na sifa kama hao Watatu. 19Je, hakupata heshima kubwa zaidi kuliko hao Watatu? Alikuwa jemadari wao, ingawa hakuhesabiwa miongoni mwao.

2023:20 2Sam 8:18; 1Nya 27:5; Yos 15:21; Kut 15:15Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa mpiganaji hodari kutoka Kabseeli ambaye alifanya mambo makubwa ya ujasiri. Aliwaua mashujaa wawili waliokuwa hodari kuliko wote wa Moabu. Pia alishuka shimoni kulipokuwa na theluji na kumuua simba. 2123:21 1Nya 11:23Pia alimuua Mmisri mrefu mkubwa. Ingawa Mmisri alikuwa na mkuki mkononi mwake, Benaya alimwendea akiwa na rungu. Alipokonya mkuki kutoka mkononi mwa Mmisri na kumuua kwa mkuki wake mwenyewe. 22Haya yalikuwa mambo ya ushujaa ya Benaya mwana wa Yehoyada; naye pia alikuwa maarufu kama wale mashujaa watatu. 2323:23 2Sam 8:18Yeye aliheshimiwa zaidi ya wale Thelathini, lakini hakujumuishwa miongoni mwa wale Watatu. Daudi akamweka kuwa kiongozi wa walinzi wake.

2423:24 2Sam 2:18Miongoni mwa wale Thelathini walikuwepo:

Asaheli ndugu wa Yoabu;

Elhanani mwana wa Dodo kutoka Bethlehemu;

2523:25 Amu 7:1; 1Nya 11:27Shama, Mharodi;

Elika, Mharodi;

2623:26 1Nya 27:9-10Helesi, Mpalti;

Ira mwana wa Ikeshi kutoka Tekoa;

27Abiezeri kutoka Anathothi;

Mebunai, Mhushathi;

2823:28 1Nya 27:13; 2Fal 25:23; Ezr 2:22; Neh 7:26; Yer 40:8Salmoni, Mwahohi;

Maharai, Mnetofathi;

2923:29 1Nya 27:15; Yos 15:57Heledi mwana wa Baana, Mnetofathi;

Itai mwana wa Ribai kutoka Gibea ya Benyamini;

3023:30 Amu 12:13; Yos 24:30; Amu 2:9Benaya Mpirathoni;

Hidai kutoka mabonde ya Gaashi;

3123:31 2Sam 3:16Abi-Alboni, Mwaribathi;

Azmawethi, Mbarhumi;

32Eliaba, Mshaalboni;

wana wa Yasheni;

Yonathani 33mwana wa Shama, Mharari;

Ahiamu mwana wa Sharari, Mharari;

3423:34 Kum 3:14; 2Sam 11:3; 15:12Elifeleti mwana wa Ahasbai, Mmaakathi;

Eliamu mwana wa Ahithofeli, Mgiloni;

3523:35 Yos 12:22Hezro, Mkarmeli;

Paarai, Mwarbi;

3623:36 1Sam 14:47Igali mwana wa Nathani kutoka Soba;

Bani, Mgadi;

3723:37 Yos 9:17Seleki, Mwamoni;

Naharai, Mbeerothi, aliyekuwa mbeba silaha za Yoabu mwana wa Seruya;

3823:38 1Nya 2:53; 2Sam 20:26; Yos 15:48Ira, Mwithiri;

Garebu, Mwithiri;

3923:39 2Sam 11:3na Uria, Mhiti.

Jumla yao wote walikuwa watu thelathini na saba.