2 Samweli 22 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

2 Samweli 22:1-51

Wimbo Wa Daudi Wa Sifa

(Zaburi 18)

122:1 Kut 15:1; Amu 5:1; Za 18:2-50Daudi alimwimbia Bwana maneno ya wimbo huu wakati Bwana alipomwokoa mikononi mwa adui zake wote, na pia mkononi mwa Sauli. 222:2 1Sam 2:2; Za 31:3; 91:2; 71:3; 144:2; Kum 32:4; Za 18:2; Mit 18:10; Mt 18:10Akasema:

Bwana ni mwamba wangu,

ngome yangu na mwokozi wangu,

322:3 Mit 10:29; Yoe 3:16; Kum 23:15; 32:37; Za 14:6; 31:2; 59:16; 71:7; 91:2; 94:22; Isa 25:4; Yer 16:19; Mwa 15:1; Kum 33:17; Lk 1:69; Za 9:9; 52:7Mungu wangu ni mwamba wangu,

ambaye kwake ninakimbilia,

ngao yangu na pembe ya wokovu wangu.

Yeye ni ngome yangu, kimbilio langu

na mwokozi wangu,

huniokoa kutoka kwa watu wenye jeuri.

422:4 Za 48:1; 96:4; 145:3Ninamwita Bwana, anayestahili kusifiwa,

nami ninaokolewa kutoka kwa adui zangu.

522:5 Za 69:14-15; Yon 2:3“Mawimbi ya mauti yalinizunguka,

mafuriko ya maangamizi yalinilemea.

622:6 Za 116:3; Mdo 2:24Kamba za kuzimu22:6 Kuzimu kwa Kiebrania ni Sheol, maana yake ni Shimo lisilo na mwisho. zilinizunguka,

mitego ya mauti ilinikabili.

722:7 Mwa 35:3; Amu 2:15; 2Nya 15:4; Za 4:1; 77:2; 120:1; Isa 26:16; Za 34:15; 116:4; 116:4; Kut 3:7Katika shida yangu nalimwita Bwana,

nilimlilia Mungu wangu.

Kutoka Hekaluni mwake alisikia sauti yangu,

kilio changu kikafika masikioni mwake.

822:8 Amu 5:4; Za 97:4; Kut 19:18; Za 68:8; 77:18; Yer 10:10; Ay 9:6; 26:11; Za 75:3“Dunia ilitetemeka na kutikisika,

misingi ya mbingu ikatikisika,

vilitetemeka kwa sababu

alikuwa amekasirika.

922:9 Za 50:3; 97:3; Ebr 12:29; Ufu 11:5; Isa 6:6; Eze 1:13; 10:2; Hab 3:5Moshi ukapanda kutoka puani mwake,

moto uteketezao ukatoka kinywani mwake,

makaa ya moto yawakayo

yakatoka ndani mwake.

1022:10 Kut 19:9; Law 16:2; Kum 33:26; 1Fal 8:12; Ay 26:9; Za 104:3; Isa 19:1; Yer 4:13; Nah 1:3; Isa 64:1Akazipasua mbingu akashuka chini,

mawingu meusi yalikuwa chini ya miguu yake.

1122:11 Mwa 3:24; Kut 25:22; Za 104:3Alipanda juu ya kerubi akaruka,

akapaa juu kwa mbawa za upepo.

1222:12 Kut 19:9Alifanya giza hema lake la kujifunika:

mawingu meusi ya mvua ya angani.

1322:13 Ay 37:3; Za 77:18Kutokana na mwanga wa uwepo wake

mawingu yalisogea,

ikanyesha mvua ya mawe

na umeme wa radi.

1422:14 1Sam 2:10; Isa 30:30Bwana alinguruma kutoka mbinguni,

sauti ya Aliye Juu Sana ilisikika.

1522:15 Kum 32:23; Za 7:13; 77:7; Hab 3:11Aliipiga mishale na kutawanya adui,

umeme wa radi na kuwafukuza.

1622:16 Za 6:1; 50:8, 21; 106:9; Nah 1:4; Isa 30:33; 40:24; Kut 14:21Mabonde ya bahari yalifunuliwa,

na misingi ya dunia ikawa wazi

kwa kukaripia kwake Bwana,

kwa uvumi wa pumzi kutoka puani mwake.

1722:17 Za 144:7; Kut 2; 10“Alinyoosha mkono kutoka juu na kunishika;

alinitoa kutoka kilindi cha maji makuu.

1822:18 Lk 1:71Aliniokoa kutoka adui wangu mwenye nguvu nyingi,

kutoka adui zangu waliokuwa na nguvu nyingi kuliko mimi.

1922:19 Za 23:4Walinikabili siku ya msiba wangu,

lakini Bwana alikuwa msaada wangu.

2022:20 Ay 36:16; Za 31:8; 118:5; 22:8; Isa 42:1; Mt 12:18; 2Sam 15:26Alinileta nje mahali penye nafasi tele,

akaniokoa kwa kuwa alipendezwa nami.

2122:21 1Sam 26:23; Za 26:6; Ay 17:9; 22:30; 42:7-8; Za 24:4Bwana alinitendea sawasawa na uadilifu wangu;

sawasawa na usafi wa mikono yangu amenilipa.

2222:22 Mwa 18:19; Za 128:1; Mit 8:32Kwa maana nimezishika njia za Bwana;

sijatenda ubaya nikamwacha Mungu wangu.

2322:23 Kum 6:4-9; Za 119:30-32, 102; Kum 7:12Sheria zake zote zi mbele yangu,

wala sijayaacha maagizo yake.

2422:24 Mwa 6:9; Efe 1:4; Yn 1:47Nimekuwa sina hatia mbele zake,

nami nimejilinda nisitende dhambi.

2522:25 1Sam 26:23Bwana amenilipa sawasawa na uadilifu wangu,

sawasawa na usafi wangu machoni pake.

2622:26 Mt 5:7“Kwa yeye aliye mwaminifu unajionyesha kuwa mwaminifu,

kwa asiye na hatia unajionyesha kutokuwa na hatia,

2722:27 Mt 5:8; Law 26:23-2422:27 1Nya 27:9-10kwa aliye mtakatifu unajionyesha kuwa mtakatifu,

lakini kwa aliyepotoka unajionyesha kuwa mkaidi.

2822:28 Kut 3:8; 1Sam 2:8-9; Za 72:12-13; Mit 30:13; Dan 4:31; Sef 3:11; Isa 2:12-17; 5:15; Za 12:5; Mt 5:3Wewe huwaokoa wanyenyekevu,

lakini macho yako ni juu ya wenye kiburi

ili uwashushe.

2922:29 Za 27:1; Isa 2:5; Mik 7:8; Ufu 21:23; 22:5Wewe ni taa yangu, Ee Bwana.

Bwana hulifanya giza langu

kuwa mwanga.

30Kwa msaada wako naweza kushinda jeshi,

nikiwa pamoja na Mungu wangu

nitaweza kuruka ukuta.

3122:31 Kum 32:4; Mt 5:48; Za 12:6; 119:140; Mit 30:5-6; Mwa 15:1; Dan 4:37; Ufu 15:3“Kuhusu Mungu, njia yake ni kamilifu;

neno la Bwana halina dosari.

Yeye ni ngao kwa wote

wanaokimbilia kwake.

3222:32 Kut 32:31; 1Sam 2:2; Isa 45:5-6Kwa maana ni nani aliye Mungu

zaidi ya Bwana?

Ni nani aliye Mwamba

isipokuwa Mungu wetu?

3322:33 1Sam 2:2; 2Sam 7:22; Za 27:1; Kum 18:13Mungu ndiye anivikaye nguvu

na kufanya njia yangu kuwa kamilifu.

3422:34 Isa 35:6; Hab 3:19; Kum 32:13Huifanya miguu yangu kama miguu ya kulungu,

huniwezesha kusimama mahali palipo juu.

3522:35 Za 144:1; 7:12; 11:2; Zek 9:13Huifundisha mikono yangu kupigana vita;

mikono yangu inaweza kupinda upinde wa shaba.

3622:36 Efe 6:16Hunipa ngao yako ya ushindi,

unajishusha chini ili kuniinua.

3722:37 Mit 4:11Huyapanua mapito yangu,

ili miguu yangu isiteleze.

38“Niliwafuatia adui zangu na nikawaseta,

sikurudi nyuma mpaka walipoangamizwa.

3922:39 Za 44:5; 110:6; Mal 4:3Niliwaseta kabisa, nao hawakuweza kuinuka tena;

walianguka chini ya miguu yangu.

4022:40 Yos 10:24; 1Fal 5:3; Za 44:5Ulinivika nguvu kwa ajili ya kupigana vita;

uliwafanya adui zangu wasujudu miguuni pangu.

4122:41 Kut 23:27Uliwafanya adui zangu wageuke na kukimbia,

nami nikawaangamiza adui zangu.

4222:42 Isa 1:15; Za 50:22; 1Sam 14:37; 28:6; Ay 27:6; Mit 1:28Walipiga yowe, lakini hapakuwepo na yeyote wa kuwaokoa;

walimlilia Bwana, lakini hakuwajibu.

4322:43 1Fal 20:10; 2Fal 13:7; Isa 41:2; Amo 1:3; Za 7:5; Isa 41:25; Mik 7:10; Zek 10:5; Isa 5:25; 10:6; 22:5Niliwaponda kama mavumbi ya nchi;

niliwaponda na kuwakanyaga kama tope barabarani.

4422:44 Kut 11:3; 2Sam 3:1; 8:1-14; Isa 55:3-5; Kum 28:13“Umeniokoa kutokana na mashambulizi ya watu wangu;

umenihifadhi mimi kama kiongozi wa mataifa.

Watu ambao sikuwajua wananitumikia,

4522:45 Za 66:3; 81:15; Kum 33:29nao wageni huja wakininyenyekea,

mara wanisikiapo, hunitii.

4622:46 Mik 7:17Wote wanalegea,

wanatoka katika ngome zao wakitetemeka.

4722:47 Kut 15:2; Kum 32:15; Za 18:31; 89:26; 95:1Bwana yu hai! Sifa ni kwa Mwamba wangu!

Atukuzwe Mungu,

Mwamba, Mwokozi wangu!

4822:48 Hes 31:3; Za 144:2; 1Sam 25:39; Za 94:1Yeye ndiye Mungu anilipiziaye kisasi,

ayawekaye mataifa chini yangu,

4922:49 Za 140:1; 27:6aniwekaye huru toka kwa adui zangu.

Uliniinua juu ya adui zangu;

uliniokoa toka kwa watu wajeuri.

5022:50 Za 9:11; 47:6; 68:4; Rum 15:9Kwa hiyo nitakusifu, Ee Bwana,

katikati ya mataifa;

nitaliimbia sifa jina lako.

5122:51 Za 21:1; 144:9-10; 1Sam 16; 13; Za 89:20; Mdo 13:23; 2Sam 7:13; Za 89:24, 29Humpa mfalme wake ushindi mkuu;

huonyesha fadhili zake kwa mpakwa mafuta wake,

kwa Daudi na wazao wake milele.”