2 Samweli 12 – NEN & NIV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Samweli 12:1-31

Nathani Amkemea Daudi

112:1 1Fal 20:35-41; Za 51; 2Sam 14:4; 7:2; Mt 21:33, 45; Lk 15:11Bwana akamtuma Nathani kwa Daudi. Alipofika kwake akamwambia, “Katika mji mmoja kulikuwepo na watu wawili, mmoja alikuwa tajiri na mwingine alikuwa maskini. 2Yule mtu tajiri alikuwa na idadi kubwa sana ya kondoo na ngʼombe, 3lakini yule maskini hakuwa na chochote ila kondoo jike mdogo aliyekuwa amemnunua. Akamtunza kondoo huyo, akakulia kwake pamoja na watoto wake. Kondoo huyo alishiriki chakula cha bwana wake na kunywea kikombe chake hata pia huyo kondoo alilala mikononi mwa bwana wake. Kwake alikuwa kama binti yake.

4“Siku moja yule tajiri akafikiwa na mgeni, lakini huyo tajiri akaacha kuchukua mmoja wa kondoo au ngʼombe wake mwenyewe amwandalie mgeni. Badala yake akachukua yule kondoo jike mdogo aliyekuwa mali ya yule maskini na kumwandalia yule mgeni wake.”

512:5 1Fal 20:40; Mwa 34:7; Rum 2:1; 1Sam 14:39Daudi akawakwa na hasira dhidi ya mtu huyo tajiri na kumwambia Nathani, “Hakika kama Bwana aishivyo, mtu huyo aliyefanya hivyo anastahili kufa! 612:6 Kut 22:1; Lk 19:8Lazima alipe mara nne zaidi, kwa ajili ya kondoo huyo, kwa sababu amefanya jambo kama hilo na hakuwa na huruma.”

712:7 1Sam 14:13; Dan 4:22; 1Sam 2:35; 1Fal 20:42; 1Sam 16:13; 2Sam 7:8Ndipo Nathani akamwambia Daudi, “Wewe ndiwe huyo mtu! Hivi ndivyo asemavyo Bwana, Mungu wa Israeli: ‘Nilikupaka mafuta uwe mfalme juu ya Israeli, nilikuokoa kutokana na mkono wa Sauli. 812:8 2Sam 9:7Nilikupa nyumba ya bwana wako na wake za bwana wako mikononi mwako. Nikakupa nyumba ya Israeli na Yuda. Kama haya yote yalikuwa madogo sana, ningekupa hata zaidi. 912:9 Hes 15:31; 1Sam 13:14; 2Sam 11:15; 1Fal 15:5; Za 26:9; 51:14; Mwa 9:5-6; 1Sam 15:19; Law 26:15-16; Mit 13:13; Isa 5:24Kwa nini ulilidharau neno la Bwana kwa kufanya lililo ovu machoni pake? Ulimuua Uria, Mhiti kwa upanga na kumchukua mke wake awe mkeo. Ulimuua kwa upanga wa Waamoni. 1012:10 2Sam 13:28; 18:14-15; 1Fal 2:25; 2Sam 11:15Basi kwa hiyo, upanga hautaondoka nyumbani mwako kamwe kwa sababu ulinidharau mimi na kumchukua mke wa Uria, Mhiti kuwa mkeo.’

1112:11 2Sam 16:11, 21-22; Kum 28:30; 17:17“Hili ndilo asemalo Bwana: ‘Kutoka kwa nyumba yako mwenyewe nitaleta maafa juu yako. Mbele ya macho yako mwenyewe nitatwaa wake zako na kumpa yeye aliye wa karibu nawe, naye atakutana kimwili na wake zako mchana mwangavu. 1212:12 2Sam 11:14-15; 16:22Ulifanya kwa siri, lakini nitalifanya jambo hili wakati wa mchana mwangavu mbele ya Israeli yote.’ ”

1312:13 Mwa 13:13; 20:6; Hes 22:34; Za 32:1-5; 51:1-9; 103:12; Isa 43:25; 44:22; Zek 3:4-9; Mit 28:13; Yer 2:35; Mik 7:18-19; Law 20:10; 24:17Ndipo Daudi akamjibu Nathani, “Nimefanya dhambi dhidi ya Bwana.”

Nathani akamjibu, “Bwana amekuondolea dhambi yako. Hutakufa. 1412:14 Isa 52:5; Rum 2:24; Eze 36:20Lakini kwa sababu kwa kufanya hili umefanya adui za Bwana kuonyesha dharau kabisa, mwana atakayezaliwa kwako atakufa.”

1512:15 1Sam 25:38; Mwa 4:7; Amo 3:212:15 2Sam 5:25Baada ya Nathani kurudi nyumbani kwake, Bwana akampiga yule mtoto ambaye mke wa Uria alikuwa amemzalia Daudi, akaugua. 1612:16 2Sam 13:31; Za 5:7; 95:6; Isa 26:16; Yer 18:8; 50:4; Amu 20:26; Yoe 1:14Daudi akamwomba Mungu kwa ajili ya mtoto. Akafunga na akaingia ndani ya nyumba yake akawa siku zote analala sakafuni usiku kucha. 1712:17 Mwa 37:35; 1Sam 1:7; 2Sam 3:35; Dan 6:18Wazee wa nyumbani mwake wakamwendea wakasimama karibu naye ili kumwamsha kutoka pale sakafuni, lakini akakataa, wala hakula chochote pamoja nao.

18Kunako siku ya saba yule mtoto akafa. Watumishi wa Daudi wakaogopa kumwambia kuwa mtoto amekufa, kwa maana walifikiri, “Wakati mtoto alipokuwa angali hai, tulizungumza na Daudi lakini hakutusikiliza. Tutawezaje kumwambia kwamba mtoto amekufa? Anaweza kufanya kitu cha kujidhuru.”

19Daudi akaona kuwa watumishi wake wananongʼonezana wenyewe, naye akatambua kuwa mtoto alikuwa amekufa. Akauliza “Je, ni kwamba huyo mtoto amekufa?”

Wakamjibu, “Ndiyo, mtoto amekufa.”

2012:20 Mt 6:17; Mwa 41:14; Ay 1:20; Rut 3:3; Za 95:6-8; 103:8-17; Mit 3:7; 16:6; Mao 3:40-41Basi Daudi akainuka kutoka pale sakafuni. Baada ya kuoga, akajipaka mafuta na kubadilisha nguo zake kisha akaenda ndani ya nyumba ya Bwana, akaabudu. Baada ya hapo akaenda nyumbani kwake kwa kutaka kwake, wakamwandalia chakula, naye akala.

2112:21 Amu 20:26Watumishi wake wakamuuliza, “Kwa nini unafanya hivi? Mtoto alipokuwa angali hai, ulifunga na kulia; lakini sasa mtoto amekufa, umeinuka na kula.”

2212:22 Yon 3:4; Isa 38:1-5Akajibu, “Wakati mtoto alipokuwa bado yungali hai, nilifunga na kulia. Nilifikiri, ‘Nani ajuaye? Bwana aweza kunirehemu ili kumwacha mtoto aishi.’ 2312:23 Mwa 37:35; 1Sam 31:13; 2Sam 13:39; Ay 7:10; 10:21; 2Kor 5:1-8; Ebr 11:10; 13:14Lakini sasa kwa kuwa amekufa, kwa nini nifunge? Je, naweza kumrudisha tena? Mimi nitakwenda kwake, lakini yeye hatanirudia mimi.”

2412:24 1Fal 1:10-11; 1Nya 22:9; 28:5; Mt 1:6Ndipo Daudi akamfariji Bathsheba mkewe, akaingia kwake akakutana naye kimwili. Akazaa mwana, wakamwita jina lake Solomoni. Bwana alimpenda Solomoni. 2512:25 Neh 13:26Kwa kuwa Bwana alimpenda, akatuma neno kwa Daudi kwa kinywa cha nabii Nathani kuwa mtoto aitwe Yedidia12:25 Yedidia maana yake Apendwaye na Bwana. kwa ajili ya Bwana.

2612:26 Kum 3:11; 1Nya 20:1-3Wakati huo Yoabu akapigana dhidi ya Raba jamii ya Waamoni na kuteka ngome la kifalme. 27Kisha Yoabu akatuma wajumbe kwa Daudi, kusema, “Nimepigana dhidi ya Raba, nami nimetwaa chanzo chake cha maji. 28Sasa kusanya vikosi vilivyobaki na ukauzingire mji kwa jeshi na kuuteka. La sivyo, nitauteka mimi, nao utaitwa kwa jina langu.”

29Kwa hiyo Daudi akakusanya jeshi lote akaenda Raba, akaushambulia na kuuteka. 3012:30 Es 8:15; Za 21:3; 132:18; 1Nya 20:2Akachukua taji kutoka kwa kichwa cha mfalme wao, lililokuwa na uzito wa talanta moja ya dhahabu,12:30 Talanta moja ya dhahabu ni sawa na kilo 34. nayo ilizungushiwa vito vya thamani. Ikawekwa juu ya kichwa cha Daudi. Alichukua nyara nyingi kutoka mjini huo. 3112:31 1Sam 14:47Akawatoa watu waliokuwa humo, akawaweka wafanye kazi kwa misumeno, sululu za chuma na mashoka, naye akawaweka kwenye kazi ya kutengeneza matofali. Akafanya hivi kwa miji yote ya Waamoni. Kisha Daudi na jeshi lake lote wakarudi Yerusalemu.

New International Version

2 Samuel 12:1-31

Nathan Rebukes David

1The Lord sent Nathan to David. When he came to him, he said, “There were two men in a certain town, one rich and the other poor. 2The rich man had a very large number of sheep and cattle, 3but the poor man had nothing except one little ewe lamb he had bought. He raised it, and it grew up with him and his children. It shared his food, drank from his cup and even slept in his arms. It was like a daughter to him.

4“Now a traveler came to the rich man, but the rich man refrained from taking one of his own sheep or cattle to prepare a meal for the traveler who had come to him. Instead, he took the ewe lamb that belonged to the poor man and prepared it for the one who had come to him.”

5David burned with anger against the man and said to Nathan, “As surely as the Lord lives, the man who did this must die! 6He must pay for that lamb four times over, because he did such a thing and had no pity.”

7Then Nathan said to David, “You are the man! This is what the Lord, the God of Israel, says: ‘I anointed you king over Israel, and I delivered you from the hand of Saul. 8I gave your master’s house to you, and your master’s wives into your arms. I gave you all Israel and Judah. And if all this had been too little, I would have given you even more. 9Why did you despise the word of the Lord by doing what is evil in his eyes? You struck down Uriah the Hittite with the sword and took his wife to be your own. You killed him with the sword of the Ammonites. 10Now, therefore, the sword will never depart from your house, because you despised me and took the wife of Uriah the Hittite to be your own.’

11“This is what the Lord says: ‘Out of your own household I am going to bring calamity on you. Before your very eyes I will take your wives and give them to one who is close to you, and he will sleep with your wives in broad daylight. 12You did it in secret, but I will do this thing in broad daylight before all Israel.’ ”

13Then David said to Nathan, “I have sinned against the Lord.”

Nathan replied, “The Lord has taken away your sin. You are not going to die. 14But because by doing this you have shown utter contempt for12:14 An ancient Hebrew scribal tradition; Masoretic Text for the enemies of the Lord, the son born to you will die.”

15After Nathan had gone home, the Lord struck the child that Uriah’s wife had borne to David, and he became ill. 16David pleaded with God for the child. He fasted and spent the nights lying in sackcloth12:16 Dead Sea Scrolls and Septuagint; Masoretic Text does not have in sackcloth. on the ground. 17The elders of his household stood beside him to get him up from the ground, but he refused, and he would not eat any food with them.

18On the seventh day the child died. David’s attendants were afraid to tell him that the child was dead, for they thought, “While the child was still living, he wouldn’t listen to us when we spoke to him. How can we now tell him the child is dead? He may do something desperate.”

19David noticed that his attendants were whispering among themselves, and he realized the child was dead. “Is the child dead?” he asked.

“Yes,” they replied, “he is dead.”

20Then David got up from the ground. After he had washed, put on lotions and changed his clothes, he went into the house of the Lord and worshiped. Then he went to his own house, and at his request they served him food, and he ate.

21His attendants asked him, “Why are you acting this way? While the child was alive, you fasted and wept, but now that the child is dead, you get up and eat!”

22He answered, “While the child was still alive, I fasted and wept. I thought, ‘Who knows? The Lord may be gracious to me and let the child live.’ 23But now that he is dead, why should I go on fasting? Can I bring him back again? I will go to him, but he will not return to me.”

24Then David comforted his wife Bathsheba, and he went to her and made love to her. She gave birth to a son, and they named him Solomon. The Lord loved him; 25and because the Lord loved him, he sent word through Nathan the prophet to name him Jedidiah.12:25 Jedidiah means loved by the Lord.

26Meanwhile Joab fought against Rabbah of the Ammonites and captured the royal citadel. 27Joab then sent messengers to David, saying, “I have fought against Rabbah and taken its water supply. 28Now muster the rest of the troops and besiege the city and capture it. Otherwise I will take the city, and it will be named after me.”

29So David mustered the entire army and went to Rabbah, and attacked and captured it. 30David took the crown from their king’s12:30 Or from Milkom’s (that is, Molek’s) head, and it was placed on his own head. It weighed a talent12:30 That is, about 75 pounds or about 34 kilograms of gold, and it was set with precious stones. David took a great quantity of plunder from the city 31and brought out the people who were there, consigning them to labor with saws and with iron picks and axes, and he made them work at brickmaking.12:31 The meaning of the Hebrew for this clause is uncertain. David did this to all the Ammonite towns. Then he and his entire army returned to Jerusalem.