2 Samweli 1 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

2 Samweli 1:1-27

Daudi Afahamishwa Kifo Cha Sauli

11:1 1Sam 26:10; 1Nya 10:13; Yos 22:8; 1Sam 30:17; Mwa 14:7; Hes 13:29; 1Sam 11:11; 1Fal 20:29-30Baada ya kifo cha Sauli, Daudi alipokuwa amerudi kutoka kuwashinda Waamaleki, Daudi alikaa siku mbili huko Siklagi. 21:2 2Sam 4:10; Ay 2:12; Eze 27:30; 1Sam 20:41; Mwa 37:7; 37:29; 44:13; Hes 14:6; Yos 7:6; Ay 1:20; Mdo 14:14Siku ya tatu akaja mtu mwenye nguo zilizoraruka na mavumbi kichwani mwake kutoka kwenye kambi ya Sauli. Alipomjia Daudi, akajitupa chini ili kumpa heshima.

3Daudi akamuuliza, “Wewe umetoka wapi?”

Akamjibu, “Nimetoroka kutoka kambi ya Waisraeli.”

41:4 1Sam 4:16Daudi akamuuliza, “Ni nini kilichotokea? Niambie.”

Akasema, “Watu walikimbia kutoka vitani. Wengi wao walianguka na kufa. Naye Sauli na Yonathani mwanawe wamekufa.”

5Ndipo Daudi akamwambia huyo kijana aliyemletea taarifa, “Je, umefahamuje kwamba Sauli na Yonathani mwanawe wamekufa?”

61:6 1Sam 28:4; 31:2-4; 1Nya 10:1-3Yule kijana akasema, “Nilijipata huko Mlima Gilboa, naye Sauli alikuwa huko akiegemea mkuki wake, na magari ya vita na wapanda farasi wa upande wa adui wakawa wamemkaribia sana. 7Alipogeuka na kuniona, akaniita, nami nikasema, ‘Je, nifanye nini?’

81:8 1Sam 15:2; 27:8; 30:13, 17“Akaniuliza, ‘Wewe ni nani?’

“Nikamjibu, ‘Mimi ni Mwamaleki.’

91:9 Amu 9:54“Kisha akaniambia, ‘Nikaribie mimi na uniue! Niko katika maumivu makali ya kifo, lakini bado ningali hai.’

101:10 Amu 9:54; 2Fal 11:12“Kwa hiyo nikamkaribia nikamuua, kwa sababu nilijua kwamba baada ya kuanguka hangeweza kupona. Nami nikachukua lile taji lililokuwa kichwani mwake na utepe uliokuwa mkononi mwake nami nimevileta hapa kwa bwana wangu.”

111:11 Mwa 37:29; Hes 14:6; Yos 7:6; 2Sam 3:31; 13:31; Ezr 9:3; 2Nya 34:27; Yoe 2:13Ndipo Daudi pamoja na watu wote waliokuwa pamoja naye wakazishika nguo zao na kuzirarua. 12Wakaomboleza, wakalia pia na kufunga mpaka jioni kwa ajili ya Sauli na Yonathani mwanawe, kwa ajili ya jeshi la Bwana na nyumba ya Israeli, kwa sababu wameanguka kwa upanga.

131:13 1Sam 14:48Daudi akamwambia yule kijana aliyemletea taarifa, “Wewe ni mwenyeji wa wapi?”

Akamjibu, “Mimi ni mwana wa mgeni, Mwamaleki.”

141:14 1Sam 12:3; 26:9; 24:6; Hes 12:8; Za 105:15Daudi akamuuliza, “Kwa nini hukuogopa kuinua mkono wako ili kumwangamiza mpakwa mafuta wa Bwana?”

151:15 2Sam 4:10-12; Amu 8:20; 1Sam 22:17-18; 1Fal 2:25, 34, 46Kisha Daudi akamwita mmoja wa watu wake na kumwambia, “Nenda ukamuue!” Kwa hiyo akampiga, naye akafa. 161:16 Law 20:9; Mt 27; 24:25; Mdo 18:6; 1Sam 26:9; Lk 19:22Kwa maana Daudi alikuwa amemwambia, “Damu yako iwe juu ya kichwa chako mwenyewe. Kinywa chako mwenyewe kimeshuhudia dhidi yako uliposema, ‘Nilimuua mpakwa mafuta wa Bwana.’ ”

Ombolezo La Daudi Kwa Ajili Ya Sauli Na Yonathani

171:17 Mwa 50:10; Eze 32:2; 2Nya 35:25Daudi akafanya maombolezo haya kuhusu Sauli na Yonathani mwanawe, 181:18 Yos 10:13; 1Sam 31:3naye akaagiza kwamba watu wa Yuda wafundishwe ombolezo hili la upinde (ambalo limeandikwa katika Kitabu cha Yashari):

191:19 2Sam 23:8; Za 29:1; 45:3; 2Sam 3:38“Walio fahari yako, ee Israeli, wameuawa juu ya mahali pako palipoinuka.

Jinsi wenye nguvu walivyoanguka!

201:20 Mik 1:10; Yos 13:3; 1Sam 31:8; 18:6; Amu 16:23; Kut 15:20; Amu 11:34“Msilisimulie hili katika Gathi,

msilitangaze hili katika

barabara za Ashkeloni,

binti za Wafilisti wasije wakafurahia,

binti za hao wasiotahiriwa

wasije wakashangilia.

211:21 Mwa 27:28; Isa 18:4; Kum 11:17; 1Fal 8:35; 17:1; 18:1; 2Nya 6:26; Ay 36:27; 38:28; Za 65:10; 147:8; Isa 5:6; Yer 5:24; 14:4; 12:4; Eze 31:5; Isa 21:5“Enyi milima ya Gilboa,

msipate umande wala mvua,

wala mashamba yazaayo sadaka ya nafaka.

Kwa maana huko ndiko ngao ya mwenye nguvu iliponajisiwa,

ngao ya Sauli haitapakwa tena mafuta.

221:22 Isa 34:3, 7; 49:26; Kum 32:42; 1Sam 18:4Kutokana na damu ya waliouawa,

kutokana na miili ya wenye nguvu,

ule upinde wa Yonathani haukugeuka nyuma.

Upanga wa Sauli haukurudi bure.

231:23 Kum 28:49; Amu 14:18; Yer 4:13“Sauli na Yonathani,

maishani walipendwa na kuneemeka,

na katika kifo hawakutengana.

Walikuwa wepesi kuliko tai,

walikuwa na nguvu kuliko simba.

241:24 Amu 5:30“Enyi binti za Israeli,

lieni kwa ajili ya Sauli,

ambaye aliwavika nguo

nyekundu na maridadi,

ambaye aliremba mavazi yenu

kwa mapambo ya dhahabu.

25“Tazama jinsi mashujaa

walivyoanguka vitani!

Yonathani ameuawa

mahali pako palipoinuka.

261:26 Yer 22:18; 34:5; 1Sam 20:42; 18:1; 19:2; 20:17Nahuzunika kwa ajili yako,

Yonathani ndugu yangu,

kwangu ulikuwa mpendwa sana.

Upendo wako kwangu ulikuwa wa ajabu,

wa ajabu zaidi kuliko ule wa wanawake.

271:27 1Sam 2:4“Tazama jinsi mashujaa walivyoanguka!

Silaha za vita zimeangamia!”