2 Nyakati 8 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

2 Nyakati 8:1-18

Shughuli Nyingine Za Solomoni

(1 Wafalme 9:10-28)

18:1 1Fal 9:10Miaka ishirini ilipopita, ambayo katika hiyo Solomoni alilijenga Hekalu la Bwana na jumba lake mwenyewe la kifalme, 2Solomoni akajenga tena vijiji vile ambavyo Hiramu alikuwa amempa, naye akawapa Waisraeli waishi humo. 38:3 Hes 13:21; 2Sam 8:2-3Kisha Solomoni akaenda Hamath-Soba na kuuteka. 48:4 1Fal 9:14Pia akajenga mji wa Tadmori katika jangwa na miji yote ya kuhifadhia vitu katika Hamathi. 58:5 Yos 10:10; 1Nya 7:24; Hes 13:21Akajenga tena Beth-Horoni ya Juu na Beth-Horoni ya Chini, miji yenye ngome, kuta, malango na makomeo. 68:6 Yos 15:11Solomoni pia akajenga Baalathi na miji yake yote ya kuhifadhia vitu, na miji kwa ajili ya magari yake na kwa ajili ya farasi wake, chochote alichotaka kujenga katika Yerusalemu, katika Lebanoni na katika nchi yote aliyotawala.

78:7 Mwa 15:18-21; 1Fal 9:20; Ezr 9:1; Mwa 10:15Watu wote waliosalia kutoka kwa Wahiti, Waamori, Waperizi, Wahivi na Wayebusi (haya mataifa hayakuwa Waisraeli), 88:8 1Fal 9:21; 2Nya 2:18yaani, wazao wao waliobakia katika nchi, ambao Waisraeli hawakuwa wamewaangamiza: hawa Solomoni akawalazimisha kuwa watumwa katika shokoa, kama ilivyo hadi leo. 98:9 Kut 19:5; Kum 23:19; Law 25:39; Gal 4:28-31Lakini Solomoni hakuwafanya Waisraeli watumwa kwa ajili ya kazi yake, bali walikuwa wapiganaji, majemadari, maafisa wake, majemadari wa magari yake ya vita na waendesha magari ya vita. 108:10 1Fal 5:16; 9:23; 2Nya 2:18Pia walikuwa maafisa wakuu wa Mfalme Solomoni, yaani, maafisa wakaguzi 250 waliosimamia watu.

118:11 1Fal 7:8; 9:24Solomoni akampandisha mke wake binti Farao kutoka Mji wa Daudi na kumleta jumba la kifalme alilokuwa amemjengea, kwa kuwa alisema, “Mke wangu hataishi katika jumba la kifalme la Daudi mfalme wa Israeli, kwa sababu mahali ambapo Sanduku la Bwana limefika ni patakatifu.”

128:12 1Fal 8:64; 1Nya 4:1Mfalme Solomoni akamtolea Bwana dhabihu za kuteketezwa juu ya madhabahu ya Bwana ambayo alikuwa ameijenga mbele ya ukumbi, 138:13 Kut 29:38; Hes 28:3-9; Kut 23:14-16; Kum 16:16; 1Fal 9:25kulingana na mahitaji ya kila siku kwa ajili ya sadaka zilizoamriwa na Mose kwa ajili ya Sabato, Mwezi Mwandamo na sikukuu nyingine tatu za mwaka, yaani, Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, Sikukuu ya Majuma na Sikukuu ya Vibanda. 148:14 1Nya 24:1; 9:17; Neh 12:24, 36, 45; 1Nya 23:6; 2Sam 23:2; 2Nya 5:11; 31:2; 1Nya 25:1; 26:1Kwa kushika maagizo ya Daudi baba yake, aliweka migawanyo ya makuhani kwa ajili ya kazi zao, nao Walawi kuongoza kusifu na kusaidia makuhani kufuatana na mahitaji ya kila siku. Pia akaweka mabawabu katika migawanyo kwa ajili ya malango mbalimbali, kwa sababu hili ndilo Daudi mtu wa Mungu alilokuwa ameagiza. 15Nao hawakuziacha amri za mfalme alizoamuru makuhani au Walawi katika jambo lolote, ikiwa ni pamoja na zile za hazina.

16Kazi yote ya Mfalme Solomoni ilifanyika kuanzia siku msingi wa Hekalu la Bwana ulipowekwa mpaka kukamilika kwake. Kwa hiyo Hekalu la Bwana likamalizika kujengwa.

178:17 Kum 2:8; 2Fal 14:22; 1Fal 9:26Ndipo Solomoni akaenda Esion-Geberi na Elathi katika pwani ya Edomu. 188:18 1Fal 9:27; Isa 13:12; 2Nya 9:9; Mwa 10:29; Ay 22:24Naye Hiramu alimpelekea meli zilizoongozwa na maafisa wake mwenyewe, watu waliokuwa na ujuzi wa baharini. Hawa watu pamoja na wale wa Solomoni wakasafiri kwa bahari mpaka Ofiri, wakaleta kutoka huko talanta 450 za dhahabu, ambazo walimkabidhi Mfalme Solomoni.