2 Nyakati 33 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

2 Nyakati 33:1-25

Manase Mfalme Wa Yuda

(2 Wafalme 21:1-18)

133:1 2Fal 21:1; 1Nya 3:13Manase alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka hamsini na mitano. 233:2 Yer 15:4; Kum 18:9; Law 18:24-30; 2Nya 28:3; 2Fal 17:11-15Akafanya maovu machoni pa Bwana, akafuata desturi za machukizo za mataifa ambayo Bwana aliyafukuza mbele ya Waisraeli. 333:3 Kum 16:21-22; 2Nya 24:18; 2Fal 23:5-11; Kum 17:3; 2Nya 30:14; 2Fal 18:4; Yer 8:2; Sef 1:2Akajenga upya mahali pa juu pa kuabudia miungu ambapo Hezekia baba yake, alikuwa amepabomoa, pia akasimamisha madhabahu za Mabaali na nguzo za Maashera. Akalisujudia jeshi lote la angani na kuliabudu. 433:4 2Nya 7:16; 1Fal 8:29; Kum 12:11Akajenga madhabahu katika Hekalu la Bwana ambamo Bwana alikuwa amesema, “Jina langu litadumu Yerusalemu milele.” 533:5 2Nya 4:9Katika nyua zote mbili za Hekalu la Bwana akajenga madhabahu kwa ajili ya jeshi lote la angani. 633:6 Law 18:21; Kum 18:10; Kut 22:18; Law 19:31; 1Sam 28:1333:6 2Nya 28:3; Eze 23:37; 2Fal 21:6Akawatoa wanawe kuwa kafara kwa kuwapitisha katika moto katika Bonde la Ben-Hinomu, akafanya ulozi, uaguzi na uchawi, akataka ushauri kwa wenye pepo wa utambuzi na wenye kuwasiliana na mizimu. Akafanya maovu mengi machoni pa Bwana, akaichochea hasira yake.

733:7 2Nya 7:16; Za 132:14Akachukua ile sanamu aliyoichonga na kuiweka katika Hekalu la Mungu ambalo Mungu alikuwa amemwambia Daudi na mwanawe Solomoni, “Katika Hekalu hili na katika Yerusalemu niliouchagua kutoka kabila zote za Israeli, nitaliweka Jina langu milele. 833:8 2Sam 7:10Sitaifanya tena miguu ya Waisraeli iondoke tena katika nchi niliyowapa baba zenu, ikiwa watakuwa waangalifu kufanya kila kitu nilichowaamuru kuhusu sheria zote, maagizo na amri zilizotolewa kwa mkono wa Mose.” 933:9 Yer 15:4; Eze 5:7Lakini Manase akawaongoza Yuda na watu wa Yerusalemu katika upotovu, kiasi kwamba walifanya maovu mengi kuliko mataifa ambayo Bwana aliwaangamiza mbele ya Waisraeli.

1033:10 Neh 9:29; Yer 25:4Bwana akasema na Manase pamoja na watu wake, lakini hawakumjali. 1133:11 Kum 28:36; Ay 36:8; Za 107:10-11Hivyo Bwana akaleta juu yao majemadari wa jeshi la mfalme wa Ashuru, ambao walimchukua Manase kwenda kifungoni, wakaweka ndoana katika pua yake, wakamfunga kwa pingu za shaba na kumpeleka Babeli. 1233:12 2Nya 32:26; 1Pet 5:6; Yer 31:18-20; Lk 15:16-18; Kum 4:30-31; Za 118:5; Hos 5:15; Yn 2:2; Mik 6:9; Kut 10:3; Lk 18:4; 2Nya 32:16Katika dhiki yake akamsihi Bwana Mungu wake na kujinyenyekeza sana mbele za Mungu wa baba zake. 1333:13 1Nya 5:20; Ezr 8:23; Mao 3:55-56; Za 142:1-7; 9:16; Dan 4:25Naye alipomwomba, Bwana akaguswa na kule kusihi kwake na akasikiliza kilio chake, kwa hiyo akamrudisha Yerusalemu na kwenye ufalme wake. Ndipo Manase akatambua kwamba Bwana ndiye Mungu.

1433:14 1Fal 1:33; Neh 3:3; 2Nya 27:3; Neh 3:26Baadaye akajenga ukuta wa nje wa Mji wa Daudi, magharibi mwa chemchemi ya Gihoni katika bonde, hadi kufikia ingilio la Lango la Samaki na akakizunguka kilima cha Ofeli, pia akaufanya kuwa mrefu zaidi. Akawaweka majemadari katika miji yote ya Yuda iliyokuwa imejengewa ngome.

1533:15 2Fal 23:12Akaondolea mbali miungu ya kigeni na kuondoa sanamu kutoka Hekalu la Bwana pamoja na madhabahu zote alizozijenga katika kile kilima kilichojengwa Hekalu na katika Yerusalemu, akazitupa nje ya mji. 1633:16 Law 7:11-18Kisha akarudisha madhabahu ya Bwana na kutolea juu yake dhabihu za sadaka za amani pamoja na sadaka za shukrani, naye akawaamuru Yuda wamtumikie Bwana, Mungu wa Israeli. 1733:17 1Fal 22:43; 2Nya 32:12; 2Fal 15:4; 2Nya 15:17Lakini hata hivyo watu wakaendelea kutoa dhabihu mahali pa juu pa kuabudia miungu, lakini wakimtolea Bwana Mungu wao peke yake.

18Matukio mengine ya utawala wa Manase, maombi yake kwa Mungu wake na maneno aliyoambiwa na waonaji walionena naye kwa jina la Bwana, Mungu wa Israeli, yameandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli. 1933:19 2Nya 6:37; 2Fal 21; 17Maombi yake, pamoja na jinsi Mungu alivyoguswa na kusihi kwake, pia dhambi zake zote na kukosa kwake uaminifu pamoja na sehemu alizojenga mahali pa juu pa kuabudia miungu, kule kusimamisha nguzo za Ashera na sanamu kabla ya kujinyenyekeza kwake, yote yameandikwa katika kumbukumbu za waonaji. 2033:20 2Fal 21:18-20Manase akalala pamoja na baba zake akazikwa katika jumba lake la kifalme. Naye Amoni mwanawe akawa mfalme baada yake.

Amoni Mfalme Wa Yuda

(2 Wafalme 21:19-26)

21Amoni alikuwa na miaka ishirini na miwili, alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka miwili. 22Akatenda maovu machoni mwa Bwana, kama baba yake Manase alivyofanya. Amoni akaabudu na kutoa dhabihu kwa sanamu zote alizokuwa ametengeneza Manase. 2333:23 Kut 10:3; 2Nya 7:14; Za 18:27; 147:6; Mit 3:34Lakini tofauti na Manase baba yake, hakujinyenyekeza mbele za Bwana, badala yake Amoni aliongeza hatia zaidi na zaidi.

2433:24 2Nya 24:25Watumishi wa Amoni wakafanya fitina juu yake, nao wakamuulia kwake nyumbani. 2533:25 2Nya 22:1; 2Fal 21:23-24; 2Nya 25:27-28Kisha watu wa nchi wakawaua wale wote waliokuwa wamefanya hila dhidi ya Mfalme Amoni. Wakamfanya Yosia mwanawe kuwa mfalme mahali pake.