2 Nyakati 3 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

2 Nyakati 3:1-17

Solomoni Ajenga Hekalu

(1 Wafalme 6:1-38; 7:15-22)

13:1 Mdo 7:47; Mwa 28:17; 2Sam 24:18; Yn 2:19-21; 1Fal 6:1; 1Nya 29:19; 1Kor 6:19; Mwa 22:2Ndipo Solomoni akaanza kujenga Hekalu la Bwana katika Yerusalemu juu ya Mlima Moria, pale ambapo Bwana alikuwa amemtokea Daudi baba yake. Ilikuwa katika kiwanja cha kupuria cha Arauna,3:1 Pia anaitwa Ornani kwa Kiebrania. Myebusi, mahali palipotolewa na Daudi. 23:2 Ezr 5:11Alianza kujenga siku ya pili ya mwezi wa pili katika mwaka wa nne wa utawala wake.

33:3 Eze 41:2; 1Fal 6:2-3Msingi aliouweka Solomoni kwa ajili ya kulijenga Hekalu la Mungu ulikuwa urefu wa dhiraa sitini3:3 Dhiraa 60 ni sawa na mita 27. na upana dhiraa ishirini.3:3 Dhiraa 20 ni sawa na mita 9. 43:4 1Fal 6:3Ukumbi wa mbele wa Hekalu ulikuwa na urefu wa dhiraa ishirini, yaani, kuanzia upande mmoja hadi upande mwingine wa upana wa nyumba hiyo na kimo chake dhiraa thelathini.3:4 Dhiraa 30 ni sawa na mita 13.5.

Akaufunika ndani kwa dhahabu safi. 53:5 Eze 40:16; 1Fal 6:17Akaufunika ukumbi mkuu kwa mbao za miberoshi na kufunikwa kwa dhahabu safi na kuupamba kwa miti ya mitende na kuifanyizia kwa minyororo. 6Alilipamba Hekalu kwa vito vya thamani. Hiyo dhahabu aliyotumia ilikuwa dhahabu ya Parvaimu. 73:7 1Fal 6:29-35; Eze 41:18Akazifunika boriti za dari, miimo na vizingiti vya milango, kuta na milango ya Hekalu kwa dhahabu, naye akatia nakshi ya makerubi kwenye kuta.

83:8 Kut 26:32-33Akajenga Patakatifu pa Patakatifu, urefu na upana wake ulikuwa dhiraa ishirini, sawasawa na upana wa Hekalu. Alifunika ndani kwa talanta 1203:8 Talanta 120 za dhahabu ni sawa na tani 23. za dhahabu safi. 9Misumari ya dhahabu ilikuwa na uzito wa shekeli hamsini.3:9 Shekeli 50 za dhahabu ni sawa na gramu 600. Alivifunika pia vyumba vya juu kwa dhahabu.

103:10 Kut 25:18; 1Fal 6:23Katika sehemu ya Patakatifu pa Patakatifu akafanyiza jozi moja ya makerubi ya kuchongwa na kuyafunika kwa dhahabu. 11Urefu wa mabawa ya hao makerubi ulikuwa jumla ya dhiraa ishirini. Bawa moja la kerubi wa kwanza lilikuwa na urefu wa dhiraa tano,3:11 Dhiraa 5 ni sawa na mita 2.25. nalo liligusa ukuta wa Hekalu, bawa lake lingine, lilikuwa pia na urefu wa dhiraa tano, ambalo liligusa bawa la kerubi lingine. 12Vivyo hivyo bawa moja la kerubi wa pili lilikuwa na urefu wa dhiraa tano na liligusa ukuta mwingine wa pili wa Hekalu na bawa lake lingine, lilikuwa pia na urefu wa dhiraa tano nalo liligusa bawa la kerubi wa kwanza. 13Mabawa ya makerubi hawa yalitanda dhiraa ishirini. Walisimama kwa miguu yao, nyuso zao zikielekea ukumbi mkubwa.

143:14 Kut 26:31-33; Ebr 9:3; Mwa 3:24; Mt 27:51Akatengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na za kitani safi, na kutarizi makerubi juu yake.

153:15 1Fal 7:15; Ufu 3:12; Yer 52:21Mbele ya Hekalu Solomoni akatengeneza nguzo mbili, ambazo kwa pamoja zilikuwa na dhiraa thelathini na tano kwenda juu kwake, na urefu wa kila moja ilikuwa na taji juu yake yenye dhiraa tano. 163:16 1Fal 7:17-22Akatengeneza minyororo iliyosokotwa, na kuiweka juu ya zile nguzo. Pia akatengeneza makomamanga 100, na kuyashikamanisha kwenye minyororo. 17Akazisimamisha hizo nguzo mbele ya Hekalu, moja upande wa kusini na nyingine upande wa kaskazini. Ile moja ya upande wa kusini akaiita Yakini,3:17 Yakini maana yake Atathibitisha. na ya upande wa kaskazini akaiita Boazi.3:17 Boazi maana yake Imo nguvu.