2 Nyakati 27 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

2 Nyakati 27:1-9

Yothamu Mfalme Wa Yuda

(2 Wafalme 15:32-38)

127:1 1Fal 15:5, 32; 1Nya 3:12; Isa 1:1; Hos 1:1; Mik 1:1Yothamu alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na sita. Mama yake aliitwa Yerusha binti Sadoki. 227:2 2Nya 26:16-21; Za 119:120; 2Fal 15:35Akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana kama Uzia baba yake alivyokuwa amefanya, lakini tofauti na yeye, hakuingilia huduma za hekaluni mwa Bwana. Lakini hata hivyo, watu wakaendelea na desturi zao mbaya. 327:3 2Nya 26:16-21; 33:14; Neh 3:26Yothamu akajenga upya Lango la Juu la Hekalu la Bwana na kufanya kazi kubwa kwenye ukuta katika kilima cha Ofeli. 4Akajenga miji katika vilima vya Yuda pamoja na ngome na minara mwituni.

527:5 2Nya 26:8; Mwa 19:36; Yer 49:1-6; 2Fal 3:4Yothamu akafanya vita na mfalme wa Waamoni na kumshinda. Mwaka ule Waamoni wakamlipa talanta 10027:5 Talanta 100 za fedha ni sawa na tani 3.75. za fedha, kori 10,00027:5 Kori 10,000 za ngano ni sawa na tani 2.2. za ngano na kori 10,000 za shayiri. Waamoni wakamletea kiasi hicho hicho mwaka wa pili na wa tatu.

627:6 2Nya 26:5; 1Sam 2:30; 1Nya 12:14; 19:3; Za 34:8; 40:4Yothamu akaendelea kuwa na nguvu kwa sababu alienenda kwa ukamilifu mbele za Bwana Mungu wake.

7Matukio mengine ya utawala wa Yothamu, pamoja na vita vyake vyote na vitu vingine alivyofanya, vimeandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli na Yuda. 8Alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na sita. 9Yothamu akalala na baba zake na akazikwa katika Mji wa Daudi. Naye Ahazi mwanawe akawa mfalme baada yake.