2 Nyakati 19 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

2 Nyakati 19:1-11

Yehu Amkemea Yehoshafati

1Mfalme Yehoshafati wa Yuda akarudi salama kwenye jumba lake la kifalme huko Yerusalemu. 219:2 1Fal 14:13; 16:1; 2Nya 12:12; 16:2-9; Ezr 7:10; 1Sam 9:9; Za 7:11; 2Nya 24:18; 32:25Yehu mwonaji, mwana wa Hanani, akapanda kwenda kuonana naye akamwambia Mfalme Yehoshafati, “Je, utawasaidia waovu na kuwapenda wale wanaomchukia Bwana? Kwa sababu ya jambo hili, ghadhabu ya Bwana iko juu yako. 319:3 1Fal 16:1; 2Nya 16:2-9; 32:25; Mit 7:11; Za 139:21-22Hata hivyo, kuna mema yaliyoonekana kwako, kwa kuwa umeondoa katika nchi nguzo za Ashera na umeukaza moyo wako katika kumtafuta Mungu.”

Yehoshafati Aweka Waamuzi

4Yehoshafati aliishi huko Yerusalemu, naye akatoka akaenda tena miongoni mwa watu, kuanzia Beer-Sheba hadi nchi ya vilima ya Efraimu na kuwageuza wakamrudia Bwana, Mungu wa baba zao. 519:5 Mwa 47:6; Kut 16:18; 18:26Akawaweka waamuzi katika nchi, kwenye miji yote ya Yuda yenye maboma. 619:6 Law 19:15; Kum 16:18-20; Mhu 5:8; Kum 1:7; 1:17; Za 82:1Akawaambia, “Angalieni kwa makini yale mtendayo, kwa kuwa hamkuhukumu kwa ajili ya mwanadamu bali kwa ajili ya Bwana ambaye yu pamoja nanyi kila mtoapo hukumu. 719:7 Kum 32:4; Ay 8:3; Kut 18:16; Rum 2:11; 9:14; Mdo 10:34; Kum 10:17; Ay 34:19; Gal 2:6; Efe 6:9; 1Pet 1:17Basi sasa hofu ya Bwana na iwe juu yenu. Hukumuni kwa uangalifu, kwa kuwa kwa Bwana Mungu wetu hakuna jambo lisilo la haki, upendeleo, wala rushwa.”

819:8 2Nya 17:8-13; 2Sam 23:3; Kum 16:18; 17:9-13; 1Nya 23:4; 26:19Pia huko Yerusalemu, Yehoshafati akaweka baadhi ya Walawi, makuhani na viongozi wa jamaa za Waisraeli ili kutoa hukumu kwa ajili ya Bwana na kuamua magomvi. Nao waliishi huko Yerusalemu. 919:9 2Sam 23:3Akawapa maagizo haya: “Ni lazima mtumike kwa uaminifu na kwa moyo wote katika kicho cha Bwana. 1019:10 Kum 17:8; Hes 16:46; Eze 3:18Katika kila shauri lifikalo mbele yenu kutoka kwa ndugu zenu wale waishio katika miji, ikiwa ni la umwagaji wa damu au mambo mengine yahusuyo sheria, amri, hukumu au maagizo, inawapasa ninyi kuwaonya kwamba wasiingie katika hatia dhidi ya Bwana, la sivyo ghadhabu yake itakuja juu yenu na ndugu zenu. Tendeni hivyo, nanyi hamtatenda dhambi.

1119:11 1Nya 28:20“Amaria kuhani mkuu atakuwa juu yenu katika jambo lolote linalomhusu Bwana naye Zebadia mwana wa Ishmaeli, kiongozi wa kabila la Yuda, atakuwa juu yenu kwa jambo lolote linalomhusu mfalme, nao Walawi watatumika kama maafisa mbele yenu. Tendeni kwa ujasiri, naye Bwana atakuwa pamoja na wale watendao vyema.”