2 Nyakati 16 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

2 Nyakati 16:1-14

Miaka Ya Mwisho Ya Mfalme Asa

(1 Wafalme 15:17-24)

116:1 Yer 41:9; 2Nya 15:9; 1Fal 15:17Katika mwaka wa thelathini na sita wa utawala wa Asa, Mfalme Baasha wa Israeli akashambulia Yuda na kuweka ngome mji wa Rama ili kumzuia yeyote asitoke wala kuingia nchi ya Mfalme Asa wa Yuda.

2Ndipo Asa akachukua fedha na dhahabu kutoka hazina ya Hekalu la Bwana na kutoka jumba lake mwenyewe la kifalme na kumpelekea Ben-Hadadi mfalme wa Aramu, ambaye alikuwa anatawala huko Dameski. 316:3 2Nya 20:35; 25:7Akasema, “Pawepo na mkataba kati yangu na wewe, kama ulivyokuwepo kati ya baba yangu na baba yako. Tazama, nimekuletea fedha na dhahabu. Sasa vunja mkataba wako na Baasha mfalme wa Israeli ili aniondokee mimi.”

4Ben-Hadadi akakubaliana na Mfalme Asa na kutuma majemadari wa majeshi yake dhidi ya miji ya Israeli. Wakashinda Iyoni, Dani, Abel-Maimu na miji yote ya hazina ya Naftali. 5Baasha aliposikia jambo hili, akasimamisha kujenga Rama na kuacha kazi yake. 6Ndipo Mfalme Asa akawaleta watu wote wa Yuda, nao wakachukua mawe na miti ambayo Baasha alikuwa anavitumia huko Rama. Kwa vitu hivyo akajenga Geba na Mispa.

716:7 1Fal 16:1; 2Nya 19:2; 20:34; Za 146:3-6; Isa 31:1; Yer 17:5Ikawa wakati huo mwonaji Hanani akamjia Mfalme Asa wa Yuda na kumwambia: “Kwa sababu ulimtegemea mfalme wa Aramu nawe hukumtegemea Bwana Mungu wako, jeshi la mfalme wa Aramu limeponyoka mkononi mwako. 816:8 Mwa 10:6-9; 2Nya 13:16; 14:9; 12:3Je, hukumbuki lililotendeka kwa Wakushi na Walibia, hawakuwa jeshi lenye nguvu na magari mengi ya vita na wapanda farasi? Hata hivyo, ulipomtegemea Bwana yeye aliwatia mkononi mwako. 916:9 Ay 24:23; 1Sam 13:13; Za 33:13-15; Yer 5:21; 32:19; 1Kor 15:36; 2Nya 6:20; Ay 34:21; Yer 16:17; Zek 4:10; Ebr 4:13; 1Pet 3:12; 1Nya 21:8; Mt 5:22; 1Fal 15:32Kwa kuwa macho ya Bwana hukimbiakimbia duniani kote ili kujionyesha mwenye nguvu kwa ajili ya wale ambao mioyo yao inamtegemea kwa ukamilifu. Umefanya jambo la upumbavu na kuanzia sasa na kuendelea utakuwa na vita.”

1016:10 2Nya 18:26; Yer 20:2; Mt 14:3Asa akamkasirikia mwonaji kwa sababu ya jambo hili. Alikuwa ameghadhibika sana hata akamweka gerezani. Wakati huo huo Asa akaanza kuwatesa na kuwaonea baadhi ya watu kwa ukatili.

11Matukio ya utawala wa Asa, kuanzia mwanzo mpaka mwisho, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli. 1216:12 Yer 17:5-6; Kum 28:22Katika mwaka wa thelathini na tisa wa utawala wake, Asa alipatwa na ugonjwa kwenye miguu yake. Ingawa ugonjwa wake ulimzidia sana, hata katika kuugua kwake hakutafuta msaada kutoka kwa Bwana bali kwa matabibu tu. 13Katika mwaka wa arobaini na moja wa utawala wa Asa, alikufa na kulala na baba zake. 1416:14 Mwa 50:2; Yn 19:39-40; Mk 16:1; 2Nya 21:19; Yer 34:5Nao wakamzika katika kaburi lile alilokuwa amejichongea mwenyewe katika Mji wa Daudi. Wakamzika kwa jeneza lililowekwa vikolezi na mchanganyiko wa manukato ya aina mbalimbali yaliyotengenezwa kwa utaalamu wa mtengeneza marashi, nao wakawasha moto mkubwa kwa heshima yake.

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

历代志下 16:1-14

犹大与以色列争战

1亚撒执政第三十六年,以色列巴沙上来攻打犹大,并修筑拉玛,不许任何人进出犹大亚撒的地界。 2于是,亚撒取出耶和华殿里和王宫库房里的金银,送给大马士革亚兰便·哈达,说: 3“我们之间应立盟约,像我们的父辈间立约一样,现在奉上金银为礼,请你取消与以色列巴沙的盟约。这样,他就会从我境内退兵。” 4便·哈达接受了亚撒王的提议,派将领攻打以色列的城邑,攻占了以云亚伯·玛音拿弗他利所有的储货城。 5巴沙闻讯,就停止修筑拉玛6亚撒王率领全体犹大人,将巴沙修筑拉玛的石头和木材搬走,用它们修建迦巴米斯巴

哈拿尼先见

7那时,哈拿尼先见晋见犹大亚撒说:“因为你不倚靠你的上帝耶和华,反而倚靠亚兰王,所以亚兰王的军队已经从你手中逃脱。 8古实人与利比亚人不是一支战车骑兵极多的强大军队吗?然而,因为你倚靠耶和华,耶和华就把他们交在你手中。 9耶和华的眼目遍察天下,彰显大能来扶助那些全心归向祂的人。你做了愚蠢的事!从此以后,你必遭遇战祸。” 10亚撒听了就对先见发怒,把他囚禁在监狱里,同时又压迫一些民众。

亚撒逝世

11亚撒的事自始至终都记在《犹大以色列列王史》上。 12亚撒执政第三十九年患了严重的脚病。然而,他在病中却没有寻求耶和华的帮助,只寻求医生的帮助。 13亚撒在他执政第四十一年去世,与他祖先同眠, 14葬在大卫城他为自己凿的坟墓里。民众把他放在堆满精心调制的各种香料的床上,又点了一堆大火向他致哀。